Wanawake tutafute elimu na pesa tuuporomoshe mfumo dume

Wanawake tutafute elimu na pesa tuuporomoshe mfumo dume

Wanaume tunapenda wanawake waelewa (sio wajuaji), ambao hutumia akili kupata wanachotaka. Na uelewa ni pamoja kufahamu kuwa tuko kwenye ngalawa moja, tukikorofishana ngalawa yenu itazama.
Kwa hiyo FaizaFoxy Ni muelewa au mjuaji?
 
Ili iweje sasa mbadili na jinsia muwe wanaume kuna vtu vngne vpo automatically women will always be women same applies to men
 
Wanawake design yako ndio nyie mkipata pesa mnaota mapembe na kudhani mnaweza kuwa kichwa cha familia.
Swala la kunyanyasika hakikisha unaolewa na mwanaume sahihi mwenye kujua kuwa mwanaume anapaswa kumpenda mkewe, huku wewe ukitambua unapaswa kumuheshimu mumeo.

Pesa sio kila kitu kwenye ndoa kwa pande zote.
 
@Nazjaz,Naomba ufafanuzi je mfumo dume umejumuisha mambo gani hasa? Itapendeza ukiyataja au kuyaainisha yote ndio nami niweze kuchangia
 
Ingawa huwa tunapingana sana. Ila kiasili (hii asili labda imetokana na malezi) mwanamke ni mtu wa kuhitaji sehemu ya kuegemea. Unayasema haya sababu labda hauna pesa za kutosha. Ukipata pesa za kutosha ndio utaona kumbe pesa nayo si kitu utahitaji watu ile nyumba iwe nyumbani.

Hao watu atakuepo mwanaume unaempenda kwa dhati. Huyu mwanaume nae ili uishi nae kwa upendo nafasi yake kama baba wa familia lazima itambulike. Sio kwa sababu una pesa ndio unataka uwe baba-mama.

Hata mama Samia alisema yeye akirudi nyumbani anapiga goti kwa mumewe, je hana hela, au hana elimu huyu mama?

Asili ya mwanamke ni kutunzwa na asili ya mwanaume ni kutunza na kulinda. Sasa ukitaka mfumo jike utawale utaishi maisha ya upweke mno.

Ukitaka kupingana na asili utaishi maisha ya upweke sana. Utakua na hela lakini huna watu. Watu watakuogopa ikiwemo ndugu na rafiki zako.
 
Kadri mwanamke anavokua modern(kuwa na elimu formal na kipato) ndivo anavozidi kuwa tegemezi. Tafuta nadem wawili mmoja afanye kazi benki au taasisi yoyote kubwa na mwingine awe wa kawaida let say mama ntilie then anza kurecord aina ya mizinga yao. Huyu wa benki ambae kwa hisia za haraka uliamini angeweza kujitegemea ndio anakua na mizinga mikubwa kuliko mama ntilie
 
Back
Top Bottom