Wanawake tutafute elimu na pesa tuuporomoshe mfumo dume

Wanawake tutafute elimu na pesa tuuporomoshe mfumo dume

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,422
Ukiwa na elimu na pesa, mwanaume atakushinda nini?

Tabia ya utegemezi imetufanya tuwe watumwa, tudhalilishwe na kudharauliwa.

Ukiwa na elimu yako na pesa zako unatanua wigo wa uhuru wako.
Utamtoa mtu wako kwa ajili ya candle light dinner, utampeleka vacation, utamjengea mama yake nyumba huko kijijini kwao.

Pesa huleta nguvu, heshima, mamlaka na ushawishi. Ukiwa huna pesa kila siku utasimangwa na mawifi, utagombana na mama mkwe na utaishi maisha ya stress sana.

Tuvivuke vikwazo, tutafute pesa.
 
Ha ha ha, wanawake nawapenda sana; ni dada zangu, mama zangu, bibi zangu na binti zangu lakini linapokuja suala la uendeshaji mambo kiujumla hamuyawezi. Kibayolojia hamkuumbwa hivyo, mtatuharibia jamii yetu.

Mimi sipendi unyanyasaji wa wanawake, tena nitakuwa mastari wa mbele kuwatetea pale wanapokuwa wakinyanyaswa ila asikudanganye mtu ukitaka kuharibu jamii weka mfumo jike.

Mfano mmoja ni jamii ya watu weusi Marekani, jamii hii kuanzia miaka ya sitini imeharibiwa (makusudi) kwa kuuweka mfumo jike. Waliwapa wanawake nguvu kubwa ya kusikilizwa na serikali. Mwanamke akipiga simu tu polisi, hawaulizi upande wa pili wa stori, mwanaume anasekwa jela. Hii imesababisha jamii yao kukosa wanaume wa kuiangalia, matokeo yake kumeongezeka kwa wapenzi ya jinsia moja na maadili yamezidi kuporomoka.

kwa asili mwanamke hutumia hisia kufanya maamuzi hivyo wakati wa tukio kama la ugomvi mdogo, yeye hafikirii kabla ya kuamua. Haelewi kuwa akimpeleka bwana wake kwenye mikono ya sheria, kwa kosa dogo tuu, polisi watachukua hatu kali madhubuti dhidi ya jamaa. Matokeo yake familia nzima na jamii kwa ujumla inaumia.

Unakuta mdada anaona mwanaume si kitu kwa kuwa anajua "white dady" (serikali) itamsikiliza. Atajishikisha mimba, halafu atampeleka jamaa mahakamani ili mwanaume anyofolewe pesa ya matunzo (child support). Matokeo yake baba mtoto anakuwa broke na anaacha hata kwenda kumuona mtoto. Mambo kama haya yanawanyima watoto haki ya kupata matunzo ya baba na mama.

Nimetolea mfano huo kukuonesha jinsi serikali za huku zilivyofanya mambo kimkakati kuifanya jamii ya watu weusi ijimalize yenyewe (kupitia mwanamke). Hata wakati wa utumwa walikuwa wanamdhalilisha mwanaume mbele ya familia yake ili mwanamke na watoto waone baba yao alivyodhaifu. Hivyo, mama huwalea watoto katika hali ya uwoga na kutokujiamini, akiwafundisha watoto wasidiriki kumuudhi bwana wao (The Willie Lynch Letter -The Making of a Slave).

Sasa hayo mambo naona "covertly" yanaanza kuletwa Afrika bila ya wanawake wetu kujua. Mnafikiri mnatetea haki zenu kumbe mnatumika kuiharibu jamii yetu.

Amkeni!
 
Sijasoma chamoto vyoandika sababu I do not read such brabra so much. Nazjaz umesema ukweli ila nimegundua wanawake wengi wasiokuwa na elimu ya chuo kikuu au hata dipoma wameendesha familia vizuri kuliko hao ujaowasema wamesoma.

Nina dada yangu ni STD 7 amerun familia yake ya watoto 6 pamoja na kuterekezwa na mme wake aliweza kujenga nyumba yake tena nzuri kijijini, akanunua shamba kubwa ingawa mme wake alimsaidia kidogo pesa. Sasa ni mjane lakini kawalea watoto wake na anafanya biashara zake ndani na nje ya chi. Elimu ya vitabuni nimeidharau ila you need Common sense to to whatever you need to do.

Wananwake waliojikwamua hawana elimu ila ni common sense inawatuma. Watu waliosoma tunatarajia ajira au tuonekane sisi ni bora which is opposite. Mimi nimekuwa volunteer kwenye nchi nyingi bila kulipwa ila furaha ninayoipata ni zaidi ya muajiriwa. Mme wangu anathamini mchango wangu na watoto wangu wanaona fahari sana na kunipeda kwa kila niwaelezapo jinsi nilivyokutana na mzee mmoja au mtoto na nikamsaidia. Money can not buy everything.
 
Elimu haina maana ya formal education. Elimu ninayoiongelea Ni maarifa na ujuzi, hivi utaweza kuvipata popote, hata through other people's life
You are right on that. Elimu ya darasani ni upuuzi nimegundua. Nina mifano kibao ambayo haijasaidia hata kwenye familia yangu. Text book education is nothing Exposure plus common sense inatosha.
 
Kutafuta hakumaanishi tumenyimwa, kutafuta kunamaanisha kuongeza bidii zaidi
Sikatai kuongeza juhudi nachosema tuu ni kwamba tuwe waangalifu katika mambo haya ya "haki za wanawake" kwa kuwa mwanamke ametumika na wakoloni wetu kuharibu jamii.

Tunachotakiwa kufanya ni maboresho (kuondoa ukeketaji, kuzuia mimba za utotoni, kutetea mirathi n.k) huku tukiangalia maadili yetu ambayo yametulea sisi waafrika kwa miaka maelfu na maelfu.
 
Nazjaz,
Pamoja na kuwa huwa nakinzana nawe, haya mawazo ni sawia. Huwa nawahusia mabinti kuwa a lady is beautiful when educated hata akiwa nung’aembe. Uzuri wa sura hupotea bali PhD yako ipo mfukoni hadi ufe. Hata juu ya kaburi lako wataweka Marehemu aliitwa Dr nazjez
 
True unachikiongea ,wanawake ni kupambana kutafuta pesa ,bila hivo utanyanyasika sana
 
You are right on that. Elimu ya darasani ni upuuzi nimegundua. Nina mifano kibao ambayo haijasaidia hata kwenye familia yangu. Text book education is nothing Exposure plus common sense inatosha.
Unaji console tu! Inaonesha kuna pahala katika elimu ulikwama. Si wewe ni wa the Bold?
 
Nazjaz, Unatafuta mamlaka kwenye ndoa na bado unaona umuhimu wa kuwa na mume,.. Chagua moja. Mume gani atataka kuishi na mme aliyeuziwa mamlaka ya kichwa cha nyumba? Hapo ndipo mnapofeli,... Utachezewa mpka ukome na fikra potofu ulizozijenga akilini mwako. Soma usaidie familia yako na wanaokuzunguka,.. Sio upanie kuyanunua mamlaka ya mumeo...
 
Back
Top Bottom