ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Hao wakaka binafsi nawatafsiri kua ni watu wasio na kazi za kufanya, wanakurupuka bila kuwaza waongee nini tena wengine hudiriki hata kutumia kauli mbovu zisizo na kichwa wala miguu utadhani wamelazimishwa kujibu ama kutoa mada.
Mada zimekua ni wanawake tu, wake up you men, you are wasting your time kupiga madomo na majungu yasiokua na maana.
Huu mjengo ni kwaajili ya ushauri wa kimaendeleo mambo ya majungu kapige na mkeo.
amu unazidi tu kunikosha roho!!eee hiivi jamani maisha ya mtandaoni yanawasumbua sana eee??thread yaovyo soma ipotezee.wanatukana achana nao maisha yanakwenda bibie.Relax bibie bana afu kama mengine yanagonga ikulu kudeal na mijitu mizima inayosimamisha tena online ni ngumu jamani.
Ustahili Yesu kuabudiwa, Ustahili Yesu kuinuliwa, Unastahili Yesu kusujudiwa aaaaah aaaah unastahiliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
habarini marafiki
Hata nashindwa nianzie wapi jinsi hili jukwaa lililovyoharibiwa
na kuvurugwa, kisha kupondwapondwa kwa watu wachache
wenye kutaka kujitafutia umaarufu wa kijiefu humu mjengoni
Imenibidi nisema japo kwa kuhemahema kwani nimeborekaje?
yaani mpaka tunaona twende kuamba ngoma, kule siasani
kwa ajili ya kuvunjwa kwa miiko / mila na tamaduni za MMU
kinachoniudhi zaidi ni hawa MAKAKA, WANAUME, wasivyo na
haya kazi yao kubwa humu ni kusema hovyo utafikiri wametiwa
MORTA kwenye midomo yao kuwasema WANAWAKE SANA
tumewakoseani mpaka mnajisasambua kama KARANGA kwa
kuandika mambo ambayo mnatudhalilisha na kutuboa sisisi
Kwani hayako mambo mazuri ambayo yapasa kusifiwa na kuandikwa
humu mjengoni? kazi yenu kuzungumzia mambo ya kijinga yasiyofaa
na kusema DADA zetu jirekebisheni hivi mara vile yaani kero sana
Na wengine wanathubutu kuandika WANAWAKE wa KABILA fulani
bwana hawapaswi kuolewa? hiyo yote ya nini MKAKA huna jipya
la kuongea mpaka utaje kabila sijui nini vile; mmeniboa ndo maana
nimeona niweke uzi huu kuwasema kwa tabia hiyo siyo njema, kwani
watanzania tunapendana na tunajaliana na kuheshimiana punguzeni
mafitiniti hayo hayampendezi Mungu kabisa TUPENDANE NA TUJALIANE
Yangu ni hayo mwenye jicho la kuona ameona, na mwenye masikio
amesikia na mwenye kusoma hapa ameshasoma na message sent
Nawasilisha
Ladyf
samahani kama nitawakwaza wanawake wenzangu
lakini,threads za kulalamikia tabia za hawa wenzetu zimekua nyingi mno
kama ni watu wanaosikia,kuelewa na kujirekebisha watajirekebisha tu
tusihangaike na maneno yao
lets move on jamannnnnnnnnnnnnnnnnnnnniiiiiiiiiiiiiiiiii
forgive n forget
Tulishaambiwa tuwachukulie tuu, kwa ni stress za uchumi zimewabana. Hata Mimi nawaona huku mitaani kweli wanakula kwa JASHO haswa!! Wanatia huruma kwa kweli. wengine unawaona wanavocheza na miguu yetu na Kucha salon. huku siye tumenyoosha miguu biz na iPads, rav 4 imepack pembeni almost 3 to 4 hrs inakusubiri.
Inatia Joto Hasira!!!! Tuwasamehe bureee
Hao wakaka binafsi nawatafsiri kua ni watu wasio na kazi za kufanya, wanakurupuka bila kuwaza waongee nini tena wengine hudiriki hata kutumia kauli mbovu zisizo na kichwa wala miguu utadhani wamelazimishwa kujibu ama kutoa mada.
Mada zimekua ni wanawake tu, wake up you men, you are wasting your time kupiga madomo na majungu yasiokua na maana.
Huu mjengo ni kwaajili ya ushauri wa kimaendeleo mambo ya majungu kapige na mkeo.
Tatizo hao wanaowasema wanawake kila siku kwa mabaya hawana kingine cha kupost kazi yao ni lawama 2. Umaskini wa kufikiri ndio chanzo they can not think of something else better to say.