Umejitongozesha kwangu kipindi cha Xmas 🎄, unataka nikutumie nauli utoke kwenu Dar uje Dodoma. Mwanamke mwenyewe tumekutana mtandaoni, huu ni ufala.
Nauli sijakutumia, nikakudanganya nafanya maarifa uje tusherehekee mwaka mpya pamoja, nauli sijatuma.
Ukweli ni kwamba mshahara haunitoshi, maisha ya hapa JamiiForums tunaigiza sana. Mimi ni bahili hadi sitaki kuoa. Nioe kwa kipato kipi? Mwaka wa kumi niko kwenye ajira, sina gari wala uwanja.
Dada usijisumbue sana, mimi hali yangu ya kifedha ni tofauti na muonekano wangu wa nje. Unadhifu huficha mengi