Wanawake tuache ubinafsi!

Judithkaunda

Member
Aug 21, 2022
90
228
Hii ndiyo dunia niliyoambiwa kuwa uyaone!

Wakati wengine wakikesha kwenye ibada na kwenye vilinge vya waganga kutafuta ndoa, wengine ndoa zimewashinda wanatamani kuachika.

Lakini wanawake tuache ubinafsi!
Wakati unafikilia kuachana na mumeo unajifikilia mwenyewe tu, "Nikitoka hapa nikapange chumba nifanye kazi niishi maisha yangu mazuri au nitakwenda kuishi kwa bwana angu mwenye uwezo nikale bata (kuenjoy)." Hivi umeshafikilia wakati huo mtoto/watoto wako watakuwa kwenye mazingira gani? Vaa viatu vya mtoto wako halafu fikiria ungekuwa ni wewe ukapewa nafasi ya kuchagua unapotaka kuishi, ungechagua wapi?

▪️Ukaishi kwa bibi na babu.
▪️Ukaishi kwa ndugu.
▪️Ukaishi na mama bila baba.
▪️Ukaishi na baba na mama wa kambo au,
▪️ Uendelee kuishi na baba na mama yako.
Ni wapi ungechagua?

Wote tunajua nyumbani ni nyumbani haijalishi pakoje na mcheza kwao hutunzwa. Nia yangu unielewe kwamba hapo ndipo nyumbani kwao mwanao, hiyo ndiyo sehemu yake ya kujidai.

Tuache kuwaadhibu watoto wetu kwamakosa ya baba zao, ni kweli unaweza kumlea mwenyewe lakini anahitaji uwepo wake haijalishi baba yake yukoje, hata kama mlimpata kwa bahati mbaya, siyo kosa lake usimnyime haki mwanao.

Ni kweli anaweza akawa si mume mzuri lakini akawa baba bora kwa mwanao. Dunia imechafuka na matukio ya kikatili yameongezeka, hata wajomba siku hizi hawaaminiki, hivi utakuwa na amani ukiwa mbali naye?

Kama tatizo ni mume kuwa na wanawake wengine hilo ni tatizo la wanaume wengi, wameumbiwa tamaa lakini haimaanishi hakupendi. Huoni kama ni bahati katika wanawake wote kachagua kukuoa wewe, hata wewe ni shahidi siyo kwamba wewe ni mrembo sana lakini anaijua thamani yako na kwanini uko hapo.

Ndiyo maana pamoja na yeye kukusaliti lakini mkiachana wewe ndiyo umevunja ndoa yako kwasababu maamuzi yanatoka kwako. Wakati wewe unahisi mateso kuwa hapo, huwezi kuamini kuna wenzako wanatamani hiyo nafasi, wanasubili tu utikise kiberiti dada kitakulipukia.

Ni kweli wanaume wazuri wako wengi sana, lakini waoaji ni wachache mno. Tulia dada mlee watoto wenu, kama ni kazi au biashara anzia hapo ulipo. Usivunje mji wako wafikilie wanao.
 
Hii ndio Dunia niliyoambiwa kuwa uyaone.

Wakati wengine wakikesha kwenye ibada na kwenye vilinge vya waganga kutafuta ndoa, wengine ndoa zimewashinda wanatamani kuachika.
Kwenye historia ya Dini zote haijawahi kutokea mwanamke mwaminifu Hata Mmoja lo linapokuja suala la vishawishi na Ahadi za Maisha mazuri.

Wanaweke pasipo na Sheria Kali kamwe hawawezi kutulia kwenye ndoa ya mume Wakati Kila Siku kuna Vijana mahandsome wanaozaliwa na kukua. Mwanamke hua anamtamani na kuwa na wivu Mpaka mtoto wake na kaka yake Wa kuzaliwa endapo ni Handsome na ana uwezo Wa kifedha na umaarufu . Ndio MAANA wanawake hawaishi kugombana na mawifi na wake Wa watoto wao . Kisa wanawaonea wivu na kuhisi kuwa wao ni Bora zaidi.

Lakini pia Wanawake wameumbwa na tamaa kubwa sana ya Kila kitu Kizuri na kuwa juu ya Kila kitu. Tukrejea Edeni na uumbaji.
Mungu alimuumba mwanamke awe msaidizi Wa Mumewe SIO bosi Wala Sawa Bali msaidizi. Yaani mwanaume KAZI yake ni KUFANYA jambo Fulani lakini anasaidiwa na Mwanamke Lakini pameibuka mafundisho ya uasi yanayosema kuwa mwanamke KAZI yake ni kupewa Kila kitu na Mwanaume na vya Mwanaume ni vya kwake na vyakwake ni vya kwake Mwenyewe.

Hii ni dhana TOFAUTI na nakusudi ya uumbaji Wa mwanzo ambapo mwanaume alikua ndiye mtawala Wa familia. Shetani akajua tamaa ya Mwanamke ya kuwa juu ya mwanaume na kupata Kila kitu Kizuri bila kumtegemea Wala kuwa chini ya mwanaume. Shetani akamdanganya kuwa akila tunda lile atakua kama Mungu. Shetani alijua kuwa mwanamke alikua anatamani kuwa Bosi ili amdhibiti Adamu na Adamu asiwe karibu na Mungu mana alikua anaona kama Adamu anamsikiliza Mungu zaidi KULIKO alivyokuwa anamsikiliza Hawa.

Hawa ALIKUA na wivu Kila aalipoona muda Mwingi Wa Adam anawaza kuhusu maagizo ya Mungu . Hawa akaona kama hapewi kipao Mbele. Kwa aliposikia kuwa atakua kama Mungu basi aliona ni Fursa ya kuwa juu ya Adam na kuwa na Maamuzi yake binafsi.

Ni kosa kubwa kuwafundisha Mabinti kuwa Wanaume sio waaminifu .
Ukweli unafichwa. Wanaume wachache sio waaminifu ila wengi ni waaminifu.
Tatizo linakuja kuwa Mwanaume Mmoja asiye mwaminifu anachepuka na kundi kubwa la wanawake wasio waaminifu. Mfano familia ya watoto Kumi waliozaliwa wanaume tupu ni TOFAUTI na familia ya watoto Kumi wanawake.

Wale wanawake wanaweza mpaka kushea mabwana na kugombania mwanaume Mmoja TOFAUTI na familia ya Wanaume Kumi. Ikitokea dhiki kidogo kwenye familia hizo mbili na muda mfupi familia ya watoto Kumi Wa Kike kuona wakiwa wameanza mapema sana kubadilisha wanaume au akatokea mwanaume Mmoja mwenye uwezo na Six-pack ataweza akatembea nao wote. TOFAUTI na wanaume Kumi ikitokea Mmoja akapata Demu basi wengine tisa watamheshimu na hawawezi Hata kuwa hahabari naye. Kila MTU hua anamchungaa sana mtoto Wa kike mana anashawishika haraka na kuharibika.

Dereva mmoja MWANAUME anayesafiri kwenda Kongo anaweza kuwa na wanawake 20 Kwa MAANA Kila kituo atakacholala anaweza kuwa na Mwanamke na wengi ni wake za watu na wachumba za watu. Hapo ni wanawake 20 wamechepuka na Mwanaume Mmoja . Sasa hapo Hao wanawake wakikutana kijiweni wanasimulia kuwa Wanaume SIO waaminifu akimwazia Yule Mmoja kumbe wote 20 wanasimulia Habari ya mwanaume Mmoja asiye mwaminifu.

Ndio MAANA Hata kwenye makanisa yanayotoa mapepo wanawake wengi Wana mapepo ya ngono.

Kwa huyo jamii ikitaka kuwaokoa Watoto ambao Kwa kweli Kwa Sasa wengi Wanabaki bila Wazazi Kwa Wazazi kutengana au kuuana ni Lazima wanawake wajitambue na kuacha tamaa. Wengi Siku hizi wanawaza starehe zao WENYEWE . Tendo la ndoa limekua kama ulevi Kwa Wanawake. MTU anawaza kukutana na mwanaume Azini Naye mpaka uwake moto na akiamka asubuhi Mwili umechoka kama Hangover ya pombe na anajisikia kiungo kinauma. Sasa huo ni ulevi na kukosa kiasi. Akisimulia wenzake basi inakua kama MTU anayesimulia kuwa alikunywa pombe Mpaka akatapika na asubuhi akaamka akiwa anaumwa kichwa . Huu ni ulevi.

Kama wanaume walivyo walevi na kutelekeza familia zao Kwa Sasa wanawake wameshikwa na ulevi Wa ngono na wanatelekeza familia zao.
 
Hii ndio Dunia niliyoambiwa kuwa uyaone.

Wakati wengine wakikesha kwenye ibada na kwenye vilinge vya waganga kutafuta ndoa, wengine ndoa zimewashinda wanatamani kuachika.
Me walafi wakija PM kugombania nafasi za kutangaza nia ya kukuwowa tafadhali nijuze niwe CHAWA wako kukusaidia kubaini matapeli, maana si kila Me ni Mume bali wengine ni wachakati vipochi manyoya tu, cc Zero IQ & Mzabzab...
 
Back
Top Bottom