Wanawake tabia hii iacheni

Chozilaurithi

Senior Member
Apr 13, 2018
120
55
Siku hiyo mume alirudi nyumbani ghafla huku akiwa anahema na kutokwa jasho alipofika nyumbani mke akamuuliza.
“mmewangu mbona leo umerudi nyumbani mapema kulikoni kuna tatizo gani? “
Mme akajibu “mke wangu mama amefariki fanya haraka ujiandae twende kwenye msiba”
Kwa wanawake wa mjini jinsi walivyo alimwambia mumewe hivi “hapana mume wangu siwezi nikaenda kwenye msiba nikiwa hivi ngoja niende saluni kwanza nijiandae ndo twende”
Kweli yule mwanamke alienda saluni akaseti nywele zake kwa kuvaa wigi, akajiweka hadi mikope ya bandia.
Alivyorudi nyumbani akawa anapanga nguo kwenye begi kwa ajiri ya safari ya kuelekea kwenye msiba mara akamuuliza mume wake.
“jamani kwani mama yako kafariki na nini mbona imekuwa ghafla tu?”
Mume akamjibu “hapana mke mama yangu nimetoka kuongea naye sasa hivi kwenye simu kumpa hizo habari za msiba aliyefaliki ni mama yako”
Basi yule mwanamke alivyoambia hivyo akaanza kuangua kilio na kugalagala chini mara akamwambia mumewe.
“jamani fanya haraka nipeleke kwenye msiba sije nikachelewa nikakuta washazika?”
Mume akamjibu “ngoja kwanza nijiandae niende saluni nikanyoe ndevu”

MKUKI KWA NGULIWE KWA BINADAM MCHUNGU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
manina mbwanda kalambwanda.
 
Back
Top Bottom