Kuna usemi unasema "UKITAKA KUJUA UZURI/UBAYA WA BINADAMU YEYOTE MPE PESA" amini usiamini pesa inatoa sura ya binadamu yeyote iliyojificha mfano, uchoyo, ushirikina, husuda, upendo, heshima etc.....huyu mwenzetu amepata pesa ameonyesha tabia zake za asili.....Ushauri mwambie jamaa asiangalie wema aliomfanyia kwani maudhi yanaweza kuujeruhi moyo wake ila achukue virago vyake kwani hapo sio kwake akatafute maisha mbele na aache kulialia hayo ni mambo madogo ila kwa kutokuwa na kipato cha kutosha anawaza pakufikia......Pia inawezekana huyo msichana anaogopa kuukaribisha umasikini kwani jamaa haonyeshi juhudi za dhati za kutafuta kazi.