Wanawake sio waoga aisee......

Wanawake sio waoga aisee......

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
1,224
Reaction score
1,258
Habarini wana jamii forum wenzangu,
Hope ni wazima wa afya...

Jana mida fulani ya jioni nilikuwa mimi na rafiki yangu kwenye gari aina ya Noah tunatoka zetu town tunarud mitaa ya home ambako ni mbali na town.

Tukapaki gari mitaa fulani sio mbali na town tukasema ngoja tupate soda mbili tatu, sasa hapo sehemu tulipokuwa tunakunywa soda kwa pembeni kulikuwa na dada mmoja maji ya kunde mkali kinoma anachezea simu yake sijui alikuwa anachati au vipi, basi jamaa yangu akamuita dada vipi unaweza kujumuika na sisi tubadilishane maana??

Lakini jamaa yangu akiwa na imani kabisa huyo dada atakaa.Cha ajabu yule dada hakukataa akajumuika tukamkaribisha soda achukue, au kama anakunywa bia aagize, akakataa akasema ameshakunywa kipindi sisi hatujaja, basi sote zikaendelea mpaka mida ya saa moja na nusu dada wa watu akatuzoea vibaya na kutuamini kwa muda mfupi tukawa marafiki,

Akasema yeye anafanya kazi zake ndogondogo za kuuza nguo za kike, tukamwambia na sisi tuna duka la mzee la bolts na nuts tunamsaidia ila tumepanga miataa ya Uchira kama kilometa 12 kutoka moshi mjini.

Sasa baadaye jamaa yangu akamshawishi yule dada kama hatojali anaweza akaondoka na sisi twende maeneo tunakoishi akapajue kama hatajali halafu tutamsindikiza,

Kwanini yule dada asikubali,tukaondoka naye tumetembea kama kilomuta 9 hivi, jamaa yangu akasimamisha gari akamuuliza hivi wewe dada mbona unajiamini sana yaani sisi watu wenyewe hutufahamu vizuri na usiku huu unakubali kuja tunapaoishi unajuaje kama sisi ni majambazi au wabakaji??

Akacheka mwenyewe akasema nyie mtakuwa watu wazuri tu mnaonekana,jamaa akamwambia ashuke kwenye gari akampa 5000 ya nauli akamwabia nenda nyumbani wewe sio mtu mzuri hata huogopi watu.........

Mara nyingi nimekuwa nikiwaona hata wakinadada wakiambiwa panda lifti twende hawawazi wanapanda haaaaaaoooooooooooooooo ........
Kwanini wanawake hamuogopi vya watu???????
 
Hamna jema saa nyingine ingetokea amekataa mngesema wanawake mnaringa amekubali imeshakuwa shida unakuja kumlalamikia humu kwa sababu siku zote huko kusogea ndio mwanzo wa kujuana lakini.

Mbaya kama angejileta mwenyewe kumbe ulimuita. Makosa anayo ila nyie ndio mna makosa zaidi.
 
Du! umetaja Uchira aisee nimekumbuka mbali sana!
Nimemkumbuka mama yangu mzazi, Pumzika kwa amani mama yangu. mleta uzi umetaja eneo alikozaliwa mama yangu mzazi
 
Ana maana Kama mngekuwa watu wabaya basi na yeye alikuwa jinni maimuna, hamkuwa na nia mbaya, Ngekewa nayo msingefika salama, mngebanduliwa naye......akili za wanawake anazijua bibi Yao HAWA/EVA
Umetishaaaa
 
Hamna jema saa nyingine ingetokea amekataa mngesema wanawake mnaringa amekubali imeshakuwa shida unakuja kumlalamikia humu kwa sababu siku zote huko kusogea ndio mwanzo wa kujuana lakini.

Mbaya kama angejileta mwenyewe kumbe ulimuita. Makosa anayo ila nyie ndio mna makosa zaidi.
Am proud of youuuuuuu
 
Nikupitie tukanywe Soda ila mim sina Noah mama so tutapiga mdogo mdogo
 
Ukimkuta anatembea barabarani anaweza akagoma kupanda. Lakini mmekutana sehemu, mmekaa mmekunywa meongea sana hata yeye ashajiridhisha nyinyi ni watu wa aina gani.
Fact mkuu ujue mtu mbaya na mzuri utamjua kwenye maongezi tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom