wanawake sa ingine mnajifedhehesha!

Umeolewa,una kazi nzuri,mme ni mfanyibiashara,mambo yake yamechanganya,nice house,gari,watoto shule za bei mbaya etc , lakini kila kukicha unahisi ana mahawara.The fact kwamba mmeo ni mhangaikaji kila wakati bize kwenye simu. Mume ana matatizo TRA,anayemsaidia ni mdada,anapigiwa simu wakati mko pamoja sebuleni,anapokea na kuongea na huyo mdada,mke anasikia sauti ya kike kwa mbali,presha inapanda inashuka.Anavizia mzee amekwenda toilet anachukua simu ya mmewe na kuscroll last number received,anai note,anai set simu yake kwenye sms na kumwandika mama wa watu ujumbe huu:
"Nani wewe unampigia simu mume wangu (anamtaja kwa jina),malaya mkubwa wewe,kwanza una ukimwi,mkome mme wangu...etc etc". Upande wa pili mama wa watu anapokea ujumbe huo wakati yeye ndo anahangaika kwa nia njema kumsaidia jamaa mambo yake ya kodi......just imagine,halafu ni mama mtu mzima ana heshima zake.
Yaani....nimechoka kabisa.

Pole mpiganaji ndowa inataka subira!
 
Hivi unafikiri wanawake hawana akili eeeh.. Au kwa sababu wanakaa kimya kwa kuwaogopa basi unajua hawaelewi kinachoendelea.

Mimi mke wangu hapokei simu yangu, wala mm sipokei yake, tunaaimiana, ila anasema siku ya kuja kumfuma huyo mwizi wa mali zake ndipo atakapoamua cha kufanya. Kwa kazi mm ni mfanyabishara yeye ni mtumishi wa umma, kila mtu ana wadau wake sasa mkianza wivu hapo huyu atamwaga ugali yule atamwaga mboga.

Hayo tena si maisha ya ndoa.
 
Mtambuzi umenena hapo ukute Bishanga alikuwa anaongea kwa sauti flani hivi ambayo bi mkubwa akawa anasikilizia ila approach aliyotumia mke si nzuri kwani alitakiwa ku deal na mume wake na si yule mwanamke.
 
Last edited by a moderator:
sijui Bishanga kapigwa na mwiko, mbona kapotea?

njoo mwaya, nakuonea huruma kweli, na huyu mkeo lazima tumchape, yaani kakuharibia japo si sana.

Sasa jipange kwenda kuomba msamaha huyu mbibi wa TRA tu ili aendelee kukusaidia, ila msipigiane simu saa za usiku.
Umeni miss eh?
 
pole sana bishanga,
kwa nini mkeo hajiamini?
Ina maana miaka yote mliyoishi pamoja hajakujua tu?
Au umeweka mazingira ya kutoaminika kwa mkeo?

Hebu keti zungumza na mkeo kuhusu swala hilo, na athari alizokusababishia, na wewe kama una mambo chobingo au mazingira ambayo sio aminifu yaache.....

Pole sana

BADILI TABIA,una akili sana wewe!
 
Last edited by a moderator:
hilo nalo neno kongosho....
Au bishanga ana small hausi zake mkewe anazisaka? Dhahama imemuangukia bibi wa tra? Haiwezekani mkewe akurupuke tu kama hakukuwa na 'mazingira ' yasiyoeleweka.....z
BT na wewe unachukua akili za shankumpempe kongosho?
 
Pole bishanga, inawezekana hukujijengea uaminifu kwa mkeo tangu awali, humu jf tu pia huaminiki(joke). Jifunze kumshirikisha mkeo hizo mambo yako hata kama si kwa kumtaka ushauri hata kwa kujiongelesha pia si vibaya.

Cathy,@apsrin hajambo?
 
Mkeo hawezi kukudoubt tu from no where bila sababu! Kuna mazingira fulani umeyajenga kiasi cha kumfanya mkeo ashindwe kujiamini..japokua mkeo amefanya approach ambayo sio nzuri lakini na wewe unapaswa kurekebisha nyendo zako Bishanga
 
Last edited by a moderator:
Umeolewa,una kazi nzuri,mme ni mfanyibiashara,mambo yake yamechanganya,nice house,gari,watoto shule za bei mbaya etc , lakini kila kukicha unahisi ana mahawara.The fact kwamba mmeo ni mhangaikaji kila wakati bize kwenye simu. Mume ana matatizo TRA,anayemsaidia ni mdada,anapigiwa simu wakati mko pamoja sebuleni,anapokea na kuongea na huyo mdada,mke anasikia sauti ya kike kwa mbali,presha inapanda inashuka.Anavizia mzee amekwenda toilet anachukua simu ya mmewe na kuscroll last number received,anai note,anai set simu yake kwenye sms na kumwandika mama wa watu ujumbe huu:
"Nani wewe unampigia simu mume wangu (anamtaja kwa jina),malaya mkubwa wewe,kwanza una ukimwi,mkome mme wangu...etc etc". Upande wa pili mama wa watu anapokea ujumbe huo wakati yeye ndo anahangaika kwa nia njema kumsaidia jamaa mambo yake ya kodi......just imagine,halafu ni mama mtu mzima ana heshima zake.
Yaani....nimechoka kabisa.

Papaa Bishanga mutu mukubwa,mutu ya ndizi pole sana okusanga nini? mawasiliano muhimu katika ngazi yoyote ya mahusiano kufichaficha ishuu zako kumesababisha ahisi una mahawara
 
Back
Top Bottom