Wanawake ni watu wa kuogopwa sana dunia hii

Polisi jamii

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
2,604
1,381
Onyo: Usisome Post hii kama umewahi kutendwa na Mwanamke, utaugua Presha na stress usijue la kufanya
Nazungumza na wanawake wote bila kujali umri
Nasema hivi, ninyi ni Mama zetu, ni wake zetu pia. Vilevile ni dada zetu na shangazi zetu kwa upande mwingine Lakini wanawake Mungu anawaona mjue
Jamaa yamemkuta, yamemkuta ndivyo unavyoweza kusema, Siri ya Mtungi kweli ajuae Kata, Hakika Moyo wa mtu ni kichaka. Kikulacho ki-nguoni mwako kweli, Wanasema “Usiusemee moyo” eti unapendwa... Zaidi ya yote naweza tu kusema kuwa Wanawake Mungu anawaona. Japo naamini si wote wa aina hii.
Wacha nianze hivi nifuate hapa Tirirka:
Jamaa yetu mmoja anazo pesa nyingi sana, alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe alioa mwanamke aliyeamini ni mzuri sana, Wakati wakiwa wachumba kama ilivyo ada kwa wadada wengi huwaambia wenza wao kuwa “Tusishiriki tendo la ngono hadi tuoane” Kumbe wakati huo huyo mdada anako kajamaa kamoja sehemu nyingine anakokaamini na kukapenda sana tena kwa dhati. anachokifanya ni kutafuta Maslahi kwa huyu mkaka.
Jamaa akavumilia, mwanzo mwisho, huku akisema moyoni kuwa “Kuku wako utamshikiaje Manati?” Alijitahidi sana kuonesha kuwa anajali, lakini yule dada asivyo na adabu, aliendelea kufanya Ngono na rafiki yake anayehisi kumpenda huku mipango ya Ndoa Ikipangwa kwa huyu anayeitwa “Mchumba”, Mipango ikakamilika, ikawa Mwezi, Ikawa wiki, mara ikawa siku na hata saa na baadae dakika na sekunde halisi ya kufunga ndoa ikafika. Ndoa ikafungwa John na Jane (Si majina halisi) wakawa mke na mme. Lakini ujue na kukumbuka Jane alikuwa na Mpenzi aitwae Joseph, (Si jina halisi)
Kumbe kipindi kile siku ilipokwisha kukaribia kuoana, Jane akahakikisha anabeba Mimba ya Joseph, kwahiyo Jane alifunga Ndoa akiwa na Mimba ya wiki moja 'aliyopachikwa' na Joseph. Kipindi cha Fungate (Honey moon) John akajitahidi kufanya alichokiweza akijiaminisha kidume cha mbegu, kumbe Ukweli aliujua vema Jane kuwa tayari anacho Kiumbe. Ikawa wiki, hata mwezi, Jane akaonekana ni Mjamzito, naye John akamshukuru Mungu sana. Ikafika Miezi Tisa ambayo hata hivyo John asingeweza kugundua lolote. Basi Mtoto akazaliwa wa Kiume, akafanana na yule jamaa (Joseph) ambaye hata hivyo John hamjui.....
Jane na Joseph waliendelea na mawasiliano, Jane alihakikisha wakipanga kuzaa na Mmewe, siku za hatari anamfuata Joseph, anatimiza lengo la Jane, mara mimba ya Pili ya Joseph ikilelewa na John ambaye naye alijiaminisha ni ya kwake. Mara Mtoto wa Pili akazaliwa akifanana na mtoto wa kwanza naye alikuwa wa kike. John akiamini ni wanae, vile vile Joseph akijua fika kuwa Jane amezaa watoto wake wawili (Judicar na Judith), ikawa hivyo, John alijitahidi kuwahudumia watoto wale akiamini ni wake. Mara wakapanga tena kuzaa mtoto wa tatu. Kama kawaida yake Jane akamfuata Joseph, wakafanya walichokikusudia
John akalea Mimba akiamini ni yake, Akazaliwa Mtoto wa tatu wa kike aliyeitwa jina Justina. watoto wakaendelea na maisha, huku Jane akiendelea kumpa taarifa za kukua kwa watoto wale ndugu Joseph, akawa anawapiga picha kila hatua, Wakaendelea kuchati na Joseph, wakipanga mpango mzuri wa kuwakutanisha watoto wale watatu na mmoja ambaye Joseph alizaa na mkewe halali wa ndoa. John wala hajui lolote, Kilichomshangaza John ni ukali wa mwanamke kwa mmewe kushika Simu.
Ndipo siku moja Mkewe Jane alipojisahau na kuacha simu Mezani, akiwa bize kufanya Usafi, na tayari alishaaga kwa mmewe kuwa baadae angetoka kwenda sehemu na kuruhusiwa. Sasa wakati akiwa bize, Joseph akatuma meseji kwa Jane, bahati njema siku hiyo John aliisoma Meseji "Hakikisha unawapiga picha wakiwa pamoja wote watatu.” John akashangaa, ikambidi ajibu “Hapana kwa leo ni ngumu” Joseph akajibu tena “Jitahidi bwana si unajua nataka nizweke picha pamoja nataka wanangu wafahamiane…”
John aka-MUTE, wala hakuonesha ghadhabu yoyote kwa mkewe, alipomaliza kazi akamwambia mkewe, “Mama Judicar, Andaa watoto tutoke mara moja” Wakaenda straight hadi Hospital Jane akashangaa John anataka kupima DNA, Maajibu yalikuja watoto wote watatu si wa kwake, Ndipo John akamwambia Mkewe, “Jane tafadhali soma hizo meseji zako zilizotoka kwa Lizzie…” Kumbe Jane alimsave Joseph kama Lizzie, Ebhana eeeee wadada Mungu anawaona.
Jane ikabidi akiri, na kumweleza ukweli Mmewe, kuwa “Nilishindwa, sikutaka kabisa kuchanganya watoto kuwa na baba tofauti” John alipofika home, akamwambia Jane ampigie simu Joseph, kuwa aje kumchukua waelekee kwenye miadi yake na amwambie Mmewe hayupo. Akafanya hivyo, Joseph alipokuja, Jane alimkaribisha Ndani, Ndipo John akatoka chumbani kuja sebureni, na kusema maneno yafuatayo:
“Ndugu yangu umenikosea sana, yaani umenivua nguo kabisa, lakini nashukuru kuwa haya mambo yamejulikana mapema, sasa Mchukue huyu mwanamke, na watoto wako nenda kwa Amani….”
Joseph hakuamini aise, kweli wakaondoka, na wala Jane hakuonesha kuomba Msamaha, wakaondoka, John hakupata usingizi kabisa siku mbili mfululizo, akaona njia pekee ya kupata Usingizi, ni kukandamiza Mvinyo kwa wingi, na kwakuwa alikuwa na Mali nyingi basi alifanya hivyo na kuwa Mlevi wa kupindukia, Lakini Mali zake zikaonekana kuanza kutapakanywa, ndipo Rafiki zake na nduguze wakaamua kumshauri atulie ikiwezekana Aoe mke mwingine, Weee jamaa hataki, nduguze wakamkumbusha kuhusu kufilisika hilo la kuacha Pombe akalikubali lakini chini ya usimamizi mkali.
Now ametulia, akili imerudi na sasa amekuwa mtulivu sana wa akili na mali zake zimerudi mahala pake, Lakini hataki kusikia kiumbe aitwae “Mwanamke” ameathirika kisaikolojia kabisa. Hadi sasa ana Miaka Mitano tangu kimkute kisanga hiko. Lakini wanawake ninyi ambao mnafanya aliyoyafanya Jane, Mungu anawaona, yaani hiki kisa kimeniuma sana kwa kweli, Jamaa ukimwambia habari za Wanawake hataki kabisa, anashangaa kabisa akisikia kuna watu wameoa wake Zaidi ya mmoja.
Maswali:
a) Je umejifunza nini katika story hii ya ukweli kabisa?
b) Je Unahisi Jane na Joseph waifanya vema kuondoka pale
c) Je Ingekuwa wewe Ungefanyaje?
d) Je unadhani John alikuwa sahihi kumfukuza Jane na watoto?
e) Je Wewe unashika simu ya mke/mme wako muda wowote upendao?
f) Ni kwa kiasi gani mn
ashirikiana ki uwazi katika matumizi ya simu na mwenza wako?
 
Tumuombe mola atuepushe na haya
Hatari sana,laiti undani Wa ndoa ungewekwa wazi naamini watu wangeuwana sana. Kama hujui endelea kutokujua na uking'ang'ania kujua zaidi utaona dunia ni mbaya mno. Kikubwa tuheshimiane sana. Ebu jiulize mwanaume umeuza mechi Mara ngapi na huyo mwanamke kama kanasa mimba nani kasingiziwa? Mwanamke ana siri mno na nzito sana na akiamua kufunguka ndunia itajaa damu. Hebu nikuulize unajuwaje kama huyo unayemwita baba na baba yako?una uhakika au umeaminishwa? Hawa wanawake daaaa!!!!
 
usi generalize mkuu, sio wanawake wote wapo hivyo. kusema wanawake ni watu wa kuogopwa duniani kwa kisa cha mtu mmoja (au wachache) ni kuwavunjia heshima.

pia wapo wanaume makatili kuliko huyo mwanamke.

tatizo sio jinsia ya mtu. tatizo ni tabia na hulka ya huyo mtu.
Umemaliza. Amen.
 
Kusema ule ukweli tukitoa na udhaifu wa wanawake na sisi wanaume pia tunachangia... Mtu unjua kabisa huyu mtu ameolewa na anafamilia yake ya nini kumwaga mbegu zako ndani yake.. kwanini unakubali kuona mwanaume mwenzako akifanywa mjinga???
 
Wanawake wengi ni matatizo,
 
usi generalize mkuu, sio wanawake wote wapo hivyo. kusema wanawake ni watu wa kuogopwa duniani kwa kisa cha mtu mmoja (au wachache) ni kuwavunjia heshima.

pia wapo wanaume makatili kuliko huyo mwanamke.

tatizo sio jinsia ya mtu. tatizo ni tabia na hulka ya huyo mtu.

Mkuu naweza kubaliana na wewe ila wakati mwingine hapana mkuu,ao wazuri chukua wew tu usimwamini mwanamke asilimia mia atakuja kukuua
 
Kusema ule ukweli tukitoa na udhaifu wa wanawake na sisi wanaume pia tunachangia... Mtu unjua kabisa huyu mtu ameolewa na anafamilia yake ya nini kumwaga mbegu zako ndani yake.. kwanini unakubali kuona mwanaume mwenzako akifanywa mjinga???

Mwanamke kwa nn asieshimu ndoa yake,..
 
Onyo: Usisome Post hii kama umewahi kutendwa na Mwanamke, utaugua Presha na stress usijue la kufanya
Nazungumza na wanawake wote bila kujali umri
Nasema hivi, ninyi ni Mama zetu, ni wake zetu pia. Vilevile ni dada zetu na shangazi zetu kwa upande mwingine Lakini wanawake Mungu anawaona mjue
Jamaa yamemkuta, yamemkuta ndivyo unavyoweza kusema, Siri ya Mtungi kweli ajuae Kata, Hakika Moyo wa mtu ni kichaka. Kikulacho ki-nguoni mwako kweli, Wanasema “Usiusemee moyo” eti unapendwa... Zaidi ya yote naweza tu kusema kuwa Wanawake Mungu anawaona. Japo naamini si wote wa aina hii.
Wacha nianze hivi nifuate hapa Tirirka:
Jamaa yetu mmoja anazo pesa nyingi sana, alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe alioa mwanamke aliyeamini ni mzuri sana, Wakati wakiwa wachumba kama ilivyo ada kwa wadada wengi huwaambia wenza wao kuwa “Tusishiriki tendo la ngono hadi tuoane” Kumbe wakati huo huyo mdada anako kajamaa kamoja sehemu nyingine anakokaamini na kukapenda sana tena kwa dhati. anachokifanya ni kutafuta Maslahi kwa huyu mkaka.
Jamaa akavumilia, mwanzo mwisho, huku akisema moyoni kuwa “Kuku wako utamshikiaje Manati?” Alijitahidi sana kuonesha kuwa anajali, lakini yule dada asivyo na adabu, aliendelea kufanya Ngono na rafiki yake anayehisi kumpenda huku mipango ya Ndoa Ikipangwa kwa huyu anayeitwa “Mchumba”, Mipango ikakamilika, ikawa Mwezi, Ikawa wiki, mara ikawa siku na hata saa na baadae dakika na sekunde halisi ya kufunga ndoa ikafika. Ndoa ikafungwa John na Jane (Si majina halisi) wakawa mke na mme. Lakini ujue na kukumbuka Jane alikuwa na Mpenzi aitwae Joseph, (Si jina halisi)
Kumbe kipindi kile siku ilipokwisha kukaribia kuoana, Jane akahakikisha anabeba Mimba ya Joseph, kwahiyo Jane alifunga Ndoa akiwa na Mimba ya wiki moja 'aliyopachikwa' na Joseph. Kipindi cha Fungate (Honey moon) John akajitahidi kufanya alichokiweza akijiaminisha kidume cha mbegu, kumbe Ukweli aliujua vema Jane kuwa tayari anacho Kiumbe. Ikawa wiki, hata mwezi, Jane akaonekana ni Mjamzito, naye John akamshukuru Mungu sana. Ikafika Miezi Tisa ambayo hata hivyo John asingeweza kugundua lolote. Basi Mtoto akazaliwa wa Kiume, akafanana na yule jamaa (Joseph) ambaye hata hivyo John hamjui.....
Jane na Joseph waliendelea na mawasiliano, Jane alihakikisha wakipanga kuzaa na Mmewe, siku za hatari anamfuata Joseph, anatimiza lengo la Jane, mara mimba ya Pili ya Joseph ikilelewa na John ambaye naye alijiaminisha ni ya kwake. Mara Mtoto wa Pili akazaliwa akifanana na mtoto wa kwanza naye alikuwa wa kike. John akiamini ni wanae, vile vile Joseph akijua fika kuwa Jane amezaa watoto wake wawili (Judicar na Judith), ikawa hivyo, John alijitahidi kuwahudumia watoto wale akiamini ni wake. Mara wakapanga tena kuzaa mtoto wa tatu. Kama kawaida yake Jane akamfuata Joseph, wakafanya walichokikusudia
John akalea Mimba akiamini ni yake, Akazaliwa Mtoto wa tatu wa kike aliyeitwa jina Justina. watoto wakaendelea na maisha, huku Jane akiendelea kumpa taarifa za kukua kwa watoto wale ndugu Joseph, akawa anawapiga picha kila hatua, Wakaendelea kuchati na Joseph, wakipanga mpango mzuri wa kuwakutanisha watoto wale watatu na mmoja ambaye Joseph alizaa na mkewe halali wa ndoa. John wala hajui lolote, Kilichomshangaza John ni ukali wa mwanamke kwa mmewe kushika Simu.
Ndipo siku moja Mkewe Jane alipojisahau na kuacha simu Mezani, akiwa bize kufanya Usafi, na tayari alishaaga kwa mmewe kuwa baadae angetoka kwenda sehemu na kuruhusiwa. Sasa wakati akiwa bize, Joseph akatuma meseji kwa Jane, bahati njema siku hiyo John aliisoma Meseji "Hakikisha unawapiga picha wakiwa pamoja wote watatu.” John akashangaa, ikambidi ajibu “Hapana kwa leo ni ngumu” Joseph akajibu tena “Jitahidi bwana si unajua nataka nizweke picha pamoja nataka wanangu wafahamiane…”
John aka-MUTE, wala hakuonesha ghadhabu yoyote kwa mkewe, alipomaliza kazi akamwambia mkewe, “Mama Judicar, Andaa watoto tutoke mara moja” Wakaenda straight hadi Hospital Jane akashangaa John anataka kupima DNA, Maajibu yalikuja watoto wote watatu si wa kwake, Ndipo John akamwambia Mkewe, “Jane tafadhali soma hizo meseji zako zilizotoka kwa Lizzie…” Kumbe Jane alimsave Joseph kama Lizzie, Ebhana eeeee wadada Mungu anawaona.
Jane ikabidi akiri, na kumweleza ukweli Mmewe, kuwa “Nilishindwa, sikutaka kabisa kuchanganya watoto kuwa na baba tofauti” John alipofika home, akamwambia Jane ampigie simu Joseph, kuwa aje kumchukua waelekee kwenye miadi yake na amwambie Mmewe hayupo. Akafanya hivyo, Joseph alipokuja, Jane alimkaribisha Ndani, Ndipo John akatoka chumbani kuja sebureni, na kusema maneno yafuatayo:
“Ndugu yangu umenikosea sana, yaani umenivua nguo kabisa, lakini nashukuru kuwa haya mambo yamejulikana mapema, sasa Mchukue huyu mwanamke, na watoto wako nenda kwa Amani….”
Joseph hakuamini aise, kweli wakaondoka, na wala Jane hakuonesha kuomba Msamaha, wakaondoka, John hakupata usingizi kabisa siku mbili mfululizo, akaona njia pekee ya kupata Usingizi, ni kukandamiza Mvinyo kwa wingi, na kwakuwa alikuwa na Mali nyingi basi alifanya hivyo na kuwa Mlevi wa kupindukia, Lakini Mali zake zikaonekana kuanza kutapakanywa, ndipo Rafiki zake na nduguze wakaamua kumshauri atulie ikiwezekana Aoe mke mwingine, Weee jamaa hataki, nduguze wakamkumbusha kuhusu kufilisika hilo la kuacha Pombe akalikubali lakini chini ya usimamizi mkali.
Now ametulia, akili imerudi na sasa amekuwa mtulivu sana wa akili na mali zake zimerudi mahala pake, Lakini hataki kusikia kiumbe aitwae “Mwanamke” ameathirika kisaikolojia kabisa. Hadi sasa ana Miaka Mitano tangu kimkute kisanga hiko. Lakini wanawake ninyi ambao mnafanya aliyoyafanya Jane, Mungu anawaona, yaani hiki kisa kimeniuma sana kwa kweli, Jamaa ukimwambia habari za Wanawake hataki kabisa, anashangaa kabisa akisikia kuna watu wameoa wake Zaidi ya mmoja.
Maswali:
a) Je umejifunza nini katika story hii ya ukweli kabisa?
b) Je Unahisi Jane na Joseph waifanya vema kuondoka pale
c) Je Ingekuwa wewe Ungefanyaje?
d) Je unadhani John alikuwa sahihi kumfukuza Jane na watoto?
e) Je Wewe unashika simu ya mke/mme wako muda wowote upendao?
f) Ni kwa kiasi gani mn
ashirikiana ki uwazi katika matumizi ya simu na mwenza wako?
Hapa tatizo lipo pande zote japo zaidi kwa mwanamke. Kwanza wewe kama mwanaume unakuwaje na mahusiano na mke wa mtu? Hili ni tatizo la kwanza kwa sisi wanaume, kamwe tusijaribu kutamani na kuwa na mahusiano na wake wa wenzetu kwani hili ni kosa kubwa mno, wanawake wapo wengi sana na wazuri pia ni wengi mno wenye uwezo mbalimbali kwa hiyo hakuna kisingizio kwa hilo. Pili tatizo lingine ni kwa huyo mwanamke aliyemdanganya mumewe na kuendelea na mahusiano na mtu ambaye si mume wake, amefanya dhambi kubwa kwa makusudi isiyosameheka mbele ya MUNGU.
 
Hatari sana,laiti undani Wa ndoa ungewekwa wazi naamini watu wangeuwana sana. Kama hujui endelea kutokujua na uking'ang'ania kujua zaidi utaona dunia ni mbaya mno. Kikubwa tuheshimiane sana. Ebu jiulize mwanaume umeuza mechi Mara ngapi na huyo mwanamke kama kanasa mimba nani kasingiziwa? Mwanamke ana siri mno na nzito sana na akiamua kufunguka ndunia itajaa damu. Hebu nikuulize unajuwaje kama huyo unayemwita baba na baba yako?una uhakika au umeaminishwa? Hawa wanawake daaaa!!!!
Nimejifunza kuwa wakati mwingine hata pesa haitoshi kukupa furaha kwenye mapenzi!

Nimejifunza kuwa kuna hatari sana iwapo utatongozea kupitia sifa yako hasa pesa na madaraka!

Nimejifunza kuwa binadamu ni fumbo, wakati mwingine hata yeye hajijui na wala anachotaka hakijui vizuri!

Nimejifunza kuwa mpenzi asotaka uguse simu yake anakuwa anaficha machafu yake!

Bado naendelea kujifunza.......
 
Back
Top Bottom