Wanawake Ni Wasanii?


...te he! hili darasa sasa linaanza kugeuka shubiri!

enhe? kumbe wanawake wa kitanzania ndivyo walivyo ee?
ndio hizo 'involuntary' behaviours au? habari kubwa hii!
 

Pretty,
Ni kweli si wote, ndo maana nikasema asilimia fulani.
Lakini kuhusu mambo ya manywele...nilishamuomba msamaha yule mama, na bahati nzuri alinielewa, pia na yeye ni member MAARUFU wa JF.
Ila kuna ukweli fulani katika mada zangu hizi za Nywele na KUDEKA... au sio Pretty?
Enjoy yr weekend.
 
...baada ya 'kushughulishwa' kote huko kipindi cha kulea mimba, kwenye DNA unakuta kumbe hata toto lenyewe sio lako, weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh....!
 
Ingawa mimi siyo mwana saikolojia lakini siamini kama wanawake wengi hufanya hivyo[ kama wapo ni kidogo sana].
Kwa bahati mbaya sisi wanaume in vigumu sana kuelewa hisia za kina mama katika kipindi hicho.
Hebu fikiria hali ya kuwa na kiumbe ndani ya mwili wake ambacho kinapitia steji mbali mbali hadi inapofika kuzaliwa. ni dhahiri naye atakuwa anabadilika kimwili na kisaikolojia na katika hali hiyo.
Siyo wanawake wote wanakuwa na tabia ya aina moja na hata mwanamke mmoja anaweza kuwa na tabia tofauti katika ujauzito wa mtoto mwingine.
Kama wewe umeoa basi lazima utakuwa ume-observe mabiliko ya tabia.
Kuna mimba nyingine mke huwa anamchukia mume utadhani amepewa mimba hiyo na mtu mwingine, na vilevile anaweza kuwa na wivu au mapenzi kwa mume kupita kiasi .
Pengine wataalam watusaidie katika hili lakini suala la usanii sidhani kama lipo.
Niliwahi kumuuliza 'wife' kuhusu hili jibu lake ni kuwa 'kwa mwanamume kuelewa hali anayokuwa nayo mwanamke mjazito inabidi naye abebe mimba. na hali hii ingewezekana kina mama wangetukimbia katika kipindi hiki ili hadi baada ya kujifungua'
UPO HAPO??????
 


ni kweli kabisa usemayo maana sitaki kuongeza maana nitaharibu jibu analo mwenyewe
 
...baada ya 'kushughulishwa' kote huko kipindi cha kulea mimba, kwenye DNA unakuta kumbe hata toto lenyewe sio lako, weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh....!
Mbu! Astaghafirluh!
Yaani unamwita mtoto toto lenyewe! Mbona kila leo wanawake wanaletewa watoto ambao waume zao wamezaa nje na kutegemewa kuwalea kwa mapenzi tele?...whats good for the goose is good for...... malizia basi!
 
Mbu! Astaghafirluh!
Yaani unamwita mtoto toto lenyewe! Mbona kila leo wanawake wanaletewa watoto ambao waume zao wamezaa nje na kutegemewa kuwalea kwa mapenzi tele?...whats good for the goose is good for...... malizia basi!

....naaam, toto halisikii la muadhini wala mnadi swala, ...tundu, bishi, halafu halifanani nawe kwa ukucha, sura wala kichwa... lipo lipo tu, na mwanaume pamoja na doubts zote mke anang'ang'ania mtoto anafanana nawe, aarrrhhhh...

Heko kwa mvumbuzi wa DNA, lazima ni mtu wa peponi tu huyu!
 
Kwa kweli hamwafanyii haki wanawake, hiyo hali hata mungu kashasema mwanamke anapochua mimba anakua kwenye uangalizi mkubwa kwani ni hatua ngumu mnoo. Wala sikutegemea kama kuna mtu angeanzisha mjadala juu ya hilo. Kama wanafanya usanii hembu muulize mama yako akuthibitishie kuwa ni usaniii. Tuwaonee huruma wanawake jamani hata kama anafanya usanii kwa ajili ya ujauzito huoni tu kuwa huyo ni mgonjwa wa saikolojia iliyo sababishwa na mimba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…