Wanawake Ni Wasanii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake Ni Wasanii?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PakaJimmy, Jul 31, 2009.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Awali nilikuwa naambiwa, lakini baadaye nikaja kuhakikisha kwamba Wanawake pindi wawapo wajawazito huwa wasumbufu saana, na wanadeka ajabu!

  Mwanamke mmoja akaja kunambia kwamba huwa wanafanya hayo mambo makusudi, maana ni nafasi yao ya pekee ya kutesa, kuomba kila watakacho, na kuwaonyesha mabwana zao kwamba ile shughuli ya kubeba mimba ni ya pekee, maana wanajua kwamba wanaume hawana uzoefu, na wala hawatakaa waijue!

  Ni kweli mara chache huwa wanaumwaumwa, lakini asilimia kubwa huwa ni matatizo ya kupangwa na yanaandaliwa na kupikwa kitaalam!

  Je wanaJF, tudhibiti vipi hii hali ya kuonewa na hawa raia wa kike?

  WoS,Nyamayao,Penina na wengineo, kwanini mnakuwa wasanii kiasi hicho?
   
  Last edited: Jul 31, 2009
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Usiwahukumu kabla ya kuwasikiliza kwa kuwauliza mbona wanakuwa wasanii?
   
 3. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwakweli sidhani kama wanafanya makusudi wote, lakini wachache nadhani wanapanga lakini asilimia kubwa ni kweli khali ile inawafanya wanafanya mambo ambayo si ya kawaida
   
 4. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Usanii tu
   
 5. M

  Msindima JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wewe PakaJimmy ulifanya utafiti kabla ya kuandika hii thread? Au umecollect data kwa huyo aliekwambia nakuamua kupost huku kabla hujatafuta wanawake wengine na kuwauliza? Hivi nikuulize mfano labda mke wake ameambiwa na dr apumzike kipindi chote cha ujauzito asifanye kazi ngumu na ukiangalia kweli unaona kabisa hali yake haiko normal utasema ni usanii? Complication za mimba zinatofautiana kwa kila mwanamke waweza kuta mimi nikiwa kwenye hali hiyo siumwi na ninaendelea na kazi zangu mpaka naenda kujifungua je hujawahi sikia wengine wanaumwa mpaka anakua chini ya uangalizi wa dr sasa hapo utasema ni usanii? huyo aliekupa hayo maelezo yawezekana yeye huwa ana-act kuwa ni mgonjwa pindi awapo kwenye hiyo hali ili tu amsumbue mumewe.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Msindima,

  Nadhani umesoma harakaharaka thread hii!
  Nilichosema ni kwamba asilimia kubwa huwa wanafanya hivyo na si wote.
  Kuna Exceptional cases za wanaoumwaumwa na wale wanaokuwa 100%bed-rest.

  Kuhusu kufanya utafiti hadi kufikia hapo, unless wewe ni mtu unayetoka sayari ngeni, ndo unaweza ukawa hujakutana na hali hii! Lakini kikawaida, sisi tunaona huku maofisini jinsi wanawake wajawazito wanavyopanga saundi kwa waume zao!

  Pia swali bado linakuja palepale, je watu hawa watadhibitiwa vipi?
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,145
  Likes Received: 577
  Trophy Points: 280
  kuna wengine akisikia harufu ya ubwabwa anakasirika, akiona mtu ana pembua mchele anatishia kuumwaga. wapo wachache ila wengi huwa hali zao zinawafanya wanakuwa hivi

  wenye ujauzito wa kwanza huwa wasumbufu sana
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Umenichekesha kweli,hata mimi niko ofisini lakini sijawahi kukutana na mazungumzo kama hayo ya wanawake wanaopangia wanaume wao sound,na wanawake wenzangu wote ninaofanya nao kazi sijawahi kumsikia akiongea hayo maneno,utakuta mtu ni mjamzito na anapiga kazi mpaka siku ya mwisho,sasa hao wanowapangia sound waume zao nadhani kuna kitu labda hawakukipata kabla ya ujauzito kwa hiyo anapopata ujauzito anaona hiyo ndo opportunity ya kupata hivyo vitu.

  Kuwadhibiti sijui kama inawezekana labda mume husika ajue hapa napigwa changa la macho hapo anaweza kudhibiti hiyo hali.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  He,
  Hivi kumbe na wewe ni mwanamke Msindima, Ha ha haaa!

  Nisamehe, lakini huo ndo ukweli!

  Mnadekedeka sana nyie kipindi hicho na mnakomoa.....`nitumie tax, siwezi kupanda dala2......mi nimeshindwa kula ugali..... wadogo zako wananiudhi, si waende kijijini?......bwana tafuta nyumba nyingine, hii imenichosha.... na mengine meeengi!

  Usipotimiza mnanuniana wiki!
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,466
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 0
  Huyo aliyekuambia, ana lengo gani na wewe au mwenzio?
  Asikuambie mtu, kubeba tumbo miezi 9, kutaabiika kipindi chote hicho, kukosa usingizi hadi asubuhi hasa miezi 3 ya mwisho, kusikia kichefuchefu miezi mitatu au minne ya mwanzo mfululizo, heartburn, pressure, kuvimba miguu na mengine mengi... ambayo kila mama mjamzito anayapitia, ukiacha matatizo mengine makubwa.... hapo bado hujafikia kilele yaani uchungu na kujifungua.Sasa wewe pata picha, unapoumwa malaria siku mbili tatu tu unakuwa hoi..... bado wanawake wanajifanya? USANII??? JIBU UNALO MWENYEWE.
   
 11. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 1,297
  Trophy Points: 280
  Hi siyo kweli kuna jamaa yangu alipata hiyo mimba ya kwanza hakuwa na tabia ya aina yoyote si yakutapika wala kuchagua vyakula au kutopenda hata kumwona mumewe.

  Kwa hiyo inategemeana tu na huyo mubeba mimba.
   
 12. M

  Msindima JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmhhh PakaJimmy sio wote kaka wanaodeka na ukiona hivyo jua tu ana lake jambo eti ndugu zako waende kijijini elewa kuwa alikuwa hawapendi sasa ndo amepata kisingizio cha kuwaondoa ndugu zako,umenikumbusha dada mmoja alikuwa jirani yetu alipopata ujauzito si akaanza madeko mume wake akitoka kazini ooo unanuka jasho kaoge ... kaoge, baba wa watu anaenda kuoga,mara nataka hiki baba wa watu akawa anajitahidi kumtimizia kila alichokua anataka,yule baba siku moja nadhani alikuja kugundua ni usanii si akaamua kutembeza kichapo tangu siku hiyo hakusikia tena oo unanuka mara kaoge ndo ikawa mwisho wa vimadeko madeko.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  WoS

  Unadhani kila mwanamke ni lazima anayapitia yote hayo?
  Si wote, maana wanawake wengine anakuwa mjamzito, lakini watu wengine wa nje mtakuja kujua siku mnaambiwa amejifungua!

  Na hayo matatizo mengine makubwa ni yapi? Si uyataje?

  Maumivu ya Homa kwa mwanaume ndo unayafananisha na hali ya ujauzito?
  Hivi kwa vile Ujauzito ni miezi 9, basi ndo inaonekana shida kubwa kwenu nyie akina mama, hv hamjui sisi wanaume tunakuwa na matatizo ya miaka nenda rudi?
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,346
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mwanamke anaposhika ujauzito kuna kuwa na mabadiliko katika chachu za ke za mwili haswa zile zinazolinda na kukuza mtoto anapokuwa tumboni nazo zinaitwa eastrogen na progestrone, hasa katika hatua ya mwanzo wa mtoto kujitengeneza katika zile wiki kumi na mbili za mwanzo .huko kwenye ubongo pia kunako hifadhi chachu za kunusa na hmu ya chakula nako kunakuwa na mabadiliko kutokana na chachu hizi mbili nyingine kuongezeka kutema na nyingine kupungua ,kunakuwa na hali ya kupata magonjwa ya asubuhi chefuchefu na kutapika tapika kila wakati,na mwili kulegea na kujisikia vibaya.

  Mtoto anapokuwa wakati mwingine anaweza kukandamiza mishipa mikubwa inayopeleka damu kwenye viuongo hasa nyonga ,miguu na kifua na ubungo kwa hiyo kuna wakati wanashindwa kulala vizuri,kukaa hata kutembea na wakati mwingine pressure ya mimba inapanda inayoweza kuleta kifafa cha uzazi.
  Ni vizuri wanaume wakajua mambo mengi yanaletwa kwa sababu za kibaolojia na wanawake wengi huwa wanavumilia sana na ndio maana wengi haswa wale wafanyakazi na wakulima au wanawake wa vijijini hujitahidi kuendelea na kazi zao kama kawaida japo kwa kujishurutisha mno kwani miili yao inakuwa haina afya nzuri sana kutokana na mabadiliko ya mtoto tumbonina chachu(hormones) za mwili kuwa katika hali ya kulinda mtoto na kumkuza akiwa tumboni
  wapendeni wake zenu wanapokuwa wajawazito,shika shika tumbo laza sikio lako tumboni mkumbatie mama hii ianasaidia sana mtoto kupata taarifa akiwa tumboni mama akifurahi mtoto anafurahi pia.hii inapelekea mtoto kuzaliwa na afya njema.
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,981
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0

  heshimu kila mwanamke isee, ile safari cdhani kama kuna mtu anaweza kuifoji, mngejua shida/mateso tunayopitia ucngeyasema haya,kumdekea mr wangu mpaka msimu wa mimba tu?
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ...inawezekana ukweli eeh?

  ...iweje mtu adai hindi la kuchoma tena saa sita za usiku? mbaya zaidi ukimshawishi asubiri mpaka majogoo anaangusha bonge la kilio!...
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,981
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0

  sorry Paka umeoa?mana uckute tunamuelewesha mtu kama Fidel hapa hatutaelewana.
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ...ndio maana manesi huwashushua wale wanaojifanya 'too posh to push!'...
   
 19. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,155
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kuambiwa kuwa mwanamke akiwa na ujauzito anakuwa na mambo yafauatayo
  1. Kumpenda mumewe, yaani kila saa anataka akae nae
  2. Kumchukia sana mumewe, yaani saa nyingine anatamani hata kummeza, hataki kabisa kumuona, ila akitoka tu mbele ya macho yake anasikia kummis
  3. Kumpenda mtu mwingine yeyote sasa kasheshe pale anapompenda mwanumme mwingine wakati anamchukia mumewe halafu ukute mume hana hili somo, patachimbika
  4. Kama alikuwa na mtoto mwingine anaweza kumchukia pasipo sababu au kumpenda pasipo sababu (hii mimi nimeishuudia live, jirani na home when i was 17 yrs old)
  5. Mengine ni yale ya kula aina fulani ya vyakula na vingine kuvichukia

  Nawasilisha
   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,155
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Waambie binamu
  Ila matatizo ya kutafuta pesa na siyo ya kijinsia, tueleweke kwa hilo hasije akatokea MwanajamiiOne hapa akauliza matatizo gani, nimeshaweka clear Nyamayao maana na wewe huchelewi kuuliza dada
   
Loading...