Wanawake ni viumbe wa ajabu sana

Wanawake ni viumbe wa ajabu sana

Stimboti

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2018
Posts
310
Reaction score
576
Mimi nina mke na mtoto mmoja. Hapa jirani ninapoishi kuna dada mmoja mkali yaani mzuri sana.

Sasa Kuna siku nilikutana naye dukani jioni saa moja nikamuomba namba akanipa. Baada ya kupeana namba tukawa tunawasiliana story za kawaida. Kadri siku zilivyokuwa zinaenda nikaanza kumtongoza akawa mkali na kunitolea nje akaniambia wewe una mke sitaki mazoea.

Kama ilivyo ada hakuna mkate mgumu mbele ya chai mwishowe akakubali tukaingia kwenye mahusiano. Sasa kilichonifanya mpaka niandike hapa ni kwa jinsi alivyokolea kimapenzi amefikia hatua anamuonea wivu wife. Akiniona na wife anachukia kinoma kufikia hatua hamsalimii mpaka wife kuna siku kaniuliza huyu dada kawaje siku hizi hanisalimii kabisa; nikapotezea sikumjibu kitu wife.

Sasa mdada ananisumbua ananipgia simu mpaka usiku, na nadhani lengo mke wangu ajue.

Yaani wanawake ni watu wa ajabu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usaliti ufanye wewe lawama upeleke kwa wanawake kapimwe mkojo haraka, Hayo ni madhara ukiwa unatongoza huku una mkosoa mkeo ili tu ukubaliwe ombi lako, Huyo mwanamke anamletea jeuli mkeo kwa kuwa wewe umetaka awe hivyo inaonesha ukiwa nae huwa unamkandia sana mkeo shwaini wahedi.
 
Back
Top Bottom