Sio kweli mpwa,. kumbuka unaposema mwanamke ni kama mtoto unamjumuisha na mama ako mzazi.. Muasisi wa msemo " mwanamke ni kama mtoto " alimaanisha hivi.
1. Ukiwa na mtoto ,mtoto wako hatakiwi kuwaza atakula nini, atavaa nini, etc. Wewe baba yake unapaswa kuwaza kwa niaba yake. Vivyo hivyo, mwanamke wako hatakiwi kuwaza atakula nini wala atavaa nini, atapata wapi hela ya kwenda saluni nakadhalika. Wewe mume unatakiwa kuwaza kwa niaba yake.
2. Mtoto anatakiwa kulindwa. Mwanamke wako pia anatakiwa kupata ulinzi kutoka kwako kama mume. Ulinzi wote kuanzia ulinzi wa kifedha hadi ulinzi wa kimwili.
3. Mtoto anatakiwa kupewa upendo wa hali ya juu sana, vivyo hivyo hata mke unatakiwa kuishi nae kwa upendo wa hali ya juu sana....
Katika tabia na hulka nyinginezo, kitu pekee ambacho mwanamke anafanana na mtoto, ni kimoja tu. THEY ARE SO EASY TO TRUST AND THAT IS BECAUSE THEY ARE TOO LOYAL BY NATURE...