gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,673
\Sijui huwa mnapata muda wa kusoma na kuchanganua kabla ya kutuma post kwa ushabiki. Nilipoongelea suala la kuosha sufuria ni mfano lakini nikauweka katika mazingira ya nyumba ya kupanga uswazi, nakuuliza utajisikia raha mumeo akisugua masufuria nje uani kavaa kaptura anasugua ukoko kwa mchanga nawe mkewe upo tena si mgonjwa? Ukinijibu hapo nitajua naongea na mwanamke gani. Otherwise mie nitajisikia vibaya sana na aibu kubwa siku nitakayomkuta mke wangu yupo darini anahangaika kufix waya za umeme labda awe ndo kazi zake. Au mke yupo busy kusimamia mafundi wanapofyatua matofali, lazima nitamuomba akapumzike nimsaidie hata hivyo nikusahihishe kuwa mke wangu hata bei ya kitasa cha mlango hajui, anachofahamu ni kunipa report kuwa kitasa kimeharibika. Kitasa kipi ni durable ye hajui ni kazi yangu. Kumbuka kama ni nyumba, gypsum nimepiga mwenyewe na fundi yeye alishangaa kwani anadhani najua sheria tu, hata gari kumwaga oil sijawahi kupeleka kwa fundi spanner ninazo ndugu yangu. Am a man by nature not by birth!
Bondspot nafaham kuwa wewe ulikuwa unatolea mfano tu na mimi nikaupeleka kama mfano tu kwani yote ni katika hali ya kujenga na kuelimishana tu. Binafsi sidhan kama kuna mama atakaa ndani amwache mumewe aoshe vyombo nje mwanamke wa kiafrika kam hakuna sababu ya msingi kama vile ugonjwa.
pia siyo kweli kwamba mwanamke hawez kusaidia kwenye majukumu mengine hata kama ni ya baba, mfano dhahiri huwa napenda mume wangu anshirikishe hata kwenye majukumu yake mathalan tunajenga basi niende naye kununua ama kuchagua vifaa vya ujenzi na siyo aende peke yake. Hata kuniambia nenda site kasimamie ujenzi pia najiskia fahari kuwa moyo wa mume wangu unaniamin kiasi cha kunituma kwenye jukumu kubwa kama hilo so to me collaboration ni muhimu sana ndani ya familia na wala siyo kuweka mgawanyo wa kazi wa kinyonyaji.
Last edited by a moderator: