Wanawake: Nahitaji ufafanuzi wenu katika jambo hili……..!

Wanawake: Nahitaji ufafanuzi wenu katika jambo hili……..!

Wanawake mwalimu wao kipofu na watakuwa wapofu tu. Wengi hapa wanakataa hawana wajibu kwa mume. Then wao ndo wa kwanza kukimbilia mwanaume mwenye mali, elimu, nk! Tunawasikia wakisema humu wanataka mwanaume mwenye pesa yake 'chop my money' wengi tu humu. Unadhani mwanaume anapokununulia simu ya dola 1000 anakupa gari japo ki-Opa, unaenda kununua viatu na nguo hata bikini Mariedo ni kwa mpango upi? Unataka akufanyie hayo na aje kujifulia boxer? Utafua na mpaka ukatike vidole na washing machine sinunui hata kama inauzwa laki saba! Utafua ma-jeans hadi ujue moto wake! In short kama ni mapenzi kwa nini jukumu liwe kwa mwanaume tu ila when it comes to a lady, mnaleta visingizio. Hakuna cha unyonge, siku hizi usawa mmeupata vizuri tu, kazi mnazo na elimu za kuwatia kiburi cha kusema huwezi kumtumikia mwanaume ilhali mwanaume anahitajika kufanya kila kitu kwa kiumbe mwanamke! Jaribuni kufahamu mapenzi hayana mipaka! Ukifanya hayo, in short mie sitapata shida ya kukimbilia videmu vinavyotega waume za watu na utapata kila utakacho, hata nyumba ya wazazi wako tutajenga mpya, what a great reciprocal love!
Bondspot natofautiana na wewe kwa 100% kama kweli unampenda utamjali and thats it. Sioni eti kisa umeninunulia gari ndio unitesee na kunisimangia. Hakuna sababu yyte ya wewe kunipa gari ilihali unakuja kunikomoa eti nikufulie majins hadi vidole vichubuke that is none sense.

to me uwajibikaji ndani ya ndoa uko kwa pande zote na zaid ukimuelemea baba mama ni mlezi tu ambaye kwasababu ya wajibu huo inamlazimu akumbane na kazi za ndani haina ubish manake huwez ukalea watu wakala meza chafu au wakalala pachafu au wakavaa nguo chafu.

kwakua unawalea utahakikisha hayo yote umeyatimiza na wala humlazimish mwenz wako kuyafanya bali yeye kwa kuyaona kuwa ni majukumu mengi na yasiyoisha basi aweza kukusaidia kwa upendo. Jamni kumbuka kuwa sisi ni wanawake na tunaish nanyie as our life mates, lazima tuish kama binadamu wala si kwa kuviziana.

inaniuma kuona kuwa kuna mwanaume msomi kama wewe unadiriki kusema kua ukimnunulia mkeo gari basi ajue atakufulia jins hadi mikono ichubuke. mwanamke yeyote mwenye busara toka mwanzo nilisha sea hawez akashindwa kutimiza wajibu wake hata siku moja.
 
Last edited by a moderator:
kwa kweli, ila plz plz unapowalea watoto wako wafunze kazi zote, wakumbushe hakuna kazi za kike wala za kiume....

you are very right BADILI TABIA, mimi nawalea kama watoto na kama binadam kama baba yao huwa anapika why them? nafikir tena wanaume wakiwa na tabia ya kufaya house works kwa nia ya kumsaidia mama japo siku moja moja basi ujue kuwa watoto nao watakua hivyo hivyo wawe wa kiume au wa kike.
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama wataweza,hili ni suala la kimaumbile zaidi!
Eiyer nakupongeza sana wewe kwan umeliona hili swala katika mtazamo mpana zaid. Mwanzoni nilisha mwambia Mtambuzi kuwa mwanamke kususa kufanya kazi fulan za ndani siyo kwamba anamuadhibu mtu la hasha bali ni njia mojawapo ya kurelease tension katika nafsi yake. ukweli ni kwamba wapo wanawake wengine unakuta mume kamuudhi na kwakua hawwez kumjibu au kusema basi atatafuta mtu mnynge pale ndani ili amwangushie hasira zake na wahanga wa haya huwa ni watoto au ma house maids.

siyo kitu kizur lkn ni jambo ambalo lipo na mtu kama huyu unapaswa umuelimishe kisaikolojia na siyo kuanza kumfanyia visa vingine.
 
Last edited by a moderator:
Eiyer nakupongeza sana wewe kwan umeliona hili swala katika mtazamo mpana zaid. Mwanzoni nilisha mwambia Mtambuzi kuwa mwanamke kususa kufanya kazi fulan za ndani siyo kwamba anamuadhibu mtu la hasha bali ni njia mojawapo ya kurelease tension katika nafsi yake. ukweli ni kwamba wapo wanawake wengine unakuta mume kamuudhi na kwakua hawwez kumjibu au kusema basi atatafuta mtu mnynge pale ndani ili amwangushie hasira zake na wahanga wa haya huwa ni watoto au ma house maids.

siyo kitu kizur lkn ni jambo ambalo lipo na mtu kama huyu unapaswa umuelimishe kisaikolojia na siyo kuanza kumfanyia visa vingine.
gfsonwin kama ukisoma uzi wangu kama nilivyonukuu hapa chini, naamini utaelewa nilikuwa nahitaji ufafanuzi gani kutoka kwenu... Mimi nimeuliza swali ili sisi wanaume tujue namna nzuri ya kuwa-handle.
Na sikusema kazi za kufua na kupiga pasi ni wajibu wa mke, bali nilitoa mfano tu......... kwani binafsi naamini katika kila ndoa, wanandoa hugawana majukumu kulinga na jinsi walivyokubaliana.........

Kwa mfano.

Mke ana kawaida ya kumuwekea mume au mpenzi wake maji ya kuoga bafuni, anamwandalia chakula vizuri, anamnyooshea nguo zake au anazikagua nguo zake kwa umakini na kuzirekebisha pale zinapokuwa na kasoro na mengine yanayofanana na hayo. Badala ya kuchukulia au kujua kwamba huo ni wajibu wake, hufanya hivyo kama deni.

Mume anapomkosea, mke huacha kufanya au kumfanyia mumewe mambo hayo kwa maelezo kwamba, haoni sababu ya kufanya hivyo kwa sababu mumewe hana shukurani…………..

Nimekuwa nikisikia malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wanaume wenzangu wakilalamikia jambo hili, na wanadai kwamba kwa upande wao hata wanapoudhiwa na wake zao kamwe hawasitishi utaratibu wao wa kuacha kodi ya meza lakini wanawake zao huwasulubu kweli kweli wanapoawakosea.

Hebu fungukeni hapa ili tujue namna nzuri ya kuwa-handle…………………
 
Last edited by a moderator:
huu ni mgawanyo wa majukumu tu. kazi rahisi-rahisi ataachiwa mwanamke na kazi ngumungumu atafanya mwanaume. na kama kusaidiana iwe kote-kote mi sioni hatari kuingia jikoni kusaidia kupika. Lakini na wewe mke ukizimikiwa na gari unanipigia simu nije kulishughulikia, mlango ukiji-lock unanipigia simu nije kuufungua. kwa nini kusaidiana iwe jikoni tu au kwenye kufua nguo? Hii ni mifano michache tu. vitabu vya dini vilishatuwekea migawanyo ya majukumu sahihi kabisa lakini mwanamke wa kisasa yuko against.
 
Mtambuzi huu uzi wako utatukosesha wengine wake....wengine tutakosa unyumba na 'privileges' nyingine
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin nakubaliana na wewe, lakini hapo kwenye BOLD naamini wanaume wengi tunaopanda daladala tutakuwa victim..........Hivi mfano nimekaa siti moja na mdada aliyejikandika vipodozi na pafyum kali, akiniambukiza hayo manukato si nitakuwa kila siku nahenyeshwa jamani...!
Duh! wanaume tunapambana na mikasa..............

Suala sio vipodozi na perfume kali za kike, tatizo ni shombo la kike! Unarudi nyumbani unanuka k*** kabisa. Ikumbukwe, wanawake tunatofautiana, wengine ni wachafu na pia hawajitambui
 
kaka yangu Bondspot naomba nirud kwako kwa kuuliza maswali haya japo sijui ni kwakuchelewa au vipi, kwani swala la kusaidiana ndani ya nyumba ni baya? sawa mimi mkeo nipo ila leo umeona majukumu yameniwia mengi je waweza nisaidia huko kuosha sufuria? mbona sisi wanawake tunawasaidia majukumu yenu? au sisi ni wanyoonge?

anyway kazi ya kutunza familia ni ya baba, mama ni mlezi tu wa familia hili halina ubish. lakin mbona ninyi mnatutegemea kutunza familia? Imagine wakati mnajenga ni wazi kuwa ulikuwa unategemea bi mkubwa naye akupe sapoti kitu ambacho alikifanya kwa moyo kwani alijua nyumba ni ya familia pengine hata kusmamia ujenzi ulimtuma sasa je na sisi watu watushangae kwa hilo?

sion mantiki katika kusaidiana bali ipo katika kutotimiza wajibu, ni dhahiri kuwa mwanamke asiyetimiza wajibu wake anaikosea familia yake no matter kwamba umekasirishwa au vipi, kwani mstaarabu atatimiza wajibu wake kisha adai haki yake baadae.

Sijui huwa mnapata muda wa kusoma na kuchanganua kabla ya kutuma post kwa ushabiki. Nilipoongelea suala la kuosha sufuria ni mfano lakini nikauweka katika mazingira ya nyumba ya kupanga uswazi, nakuuliza utajisikia raha mumeo akisugua masufuria nje uani kavaa kaptura anasugua ukoko kwa mchanga nawe mkewe upo tena si mgonjwa? Ukinijibu hapo nitajua naongea na mwanamke gani. Otherwise mie nitajisikia vibaya sana na aibu kubwa siku nitakayomkuta mke wangu yupo darini anahangaika kufix waya za umeme labda awe ndo kazi zake. Au mke yupo busy kusimamia mafundi wanapofyatua matofali, lazima nitamuomba akapumzike nimsaidie hata hivyo nikusahihishe kuwa mke wangu hata bei ya kitasa cha mlango hajui, anachofahamu ni kunipa report kuwa kitasa kimeharibika. Kitasa kipi ni durable ye hajui ni kazi yangu. Kumbuka kama ni nyumba, gypsum nimepiga mwenyewe na fundi yeye alishangaa kwani anadhani najua sheria tu, hata gari kumwaga oil sijawahi kupeleka kwa fundi spanner ninazo ndugu yangu. Am a man by nature not by birth!
 
Last edited by a moderator:
Usiwe unafikiri ndani ya box! Pia jaribu kusoma vizuri uchanganue ninachokisema. Hata hivyo sijaoa ili nipikiwe, nadhani am the best cook more than my wife for sure. Hata hivyo pole kama umekwazika maana najua wanawake mtakuwa mmeshavimba sura. Ni mitizamo tu, by tha way my wife is busy more than you can imagine thats why i always try to remind her to take a break and go for lunch ana majukumu mazito sana. Ila nyumbani hajawahi kushindwa kutekeleza majukumu yake kama mke, am very happy and lucky to have a real woman like her, hata kujifungua alikataa kupigwa kisu na leo yupo poa kama kabinti. Otherwise usipate wasiwasi, kama we hayo huyawezi na mumeo hajawahi kuwa na tatizo then its fine kila mtu na ndoa yake kwani furaha yatokana na makubaliano yenu.

Yesu wanguuuuuuuuuu............you cannot be serious!!!!!!!!!!!!!! sidhani hata kama una mke wewe,sorry.
 
Yesu wanguuuuuuuuuu............you cannot be serious!!!!!!!!!!!!!! sidhani hata kama una mke wewe,sorry.

Why Yummy?

Juzi nilikwua nasikiliza hizi redio Fanya Mizaha...kuna habari ilitoka gazeti nadhani Mwananchi,kwamba kuna kautafiti kanaonyesha 80% ya operations wakati wa kujifungua zinaombwa na wenye mimba, sababu mojawapo ikiwa ni kwamba 'hawataki kuharibu' maungo yao
 
Last edited by a moderator:
@nyumbakubwa,
ingekuwa wanaume wote wana akili za kutokufanya kazi za ndani, maana wanategemea wake zao familia nyingine hata watoto wangekufa,
nishaona familia baba mfanyabiashara mama mfanyakazi, maternity leave ya mke ilipoisha, hawa waligawana majukumu, mama akienda job asubuhi shughuli zote za malezi mume anazifanya, na mama akirudi mchana baba anatoka kwenda kwenye mihangaiko yake..... waliishi hivi takriban mwezi mmoja....... hadi walipopata msichana wa kazi.

imagine huyu baba ndo angekuwa hataku "kusugua masufuria" ingekuwaje?
imagine mtoto mchanga ingekuwaje?
kila mmoja aliiadmire hii couple... na yule baba

mie nadhani ukiachilia mbali kuwa kila familia ina style zake lakini hakuna kitu kinachoitwa wajibu.... jamii imefanya kazi za ndani zionekane ni wajibu wa mwanamke.....

ila kuna MAPENZI,
kufuliwa chupi, kupigiwa pasi nakadhalika yanafanyika kwa sababu ya mapenzi, na ndo maana penzi likiisha haya mnayoita wajibu hayafanyiki tena, ndo maana migogoro inapoanza mume analalamika mkewe hatimizi "wajibu", hajui kuwa sio kwamba ule ni wajibu la hasha yale ni mapenzi.......

Kula tano BADILI TABIA yani naomba upokee na :hug:
 
Last edited by a moderator:
huu ni mgawanyo wa majukumu tu. kazi rahisi-rahisi ataachiwa mwanamke na kazi ngumungumu atafanya mwanaume. na kama kusaidiana iwe kote-kote mi sioni hatari kuingia jikoni kusaidia kupika. Lakini na wewe mke ukizimikiwa na gari unanipigia simu nije kulishughulikia, mlango ukiji-lock unanipigia simu nije kuufungua. kwa nini kusaidiana iwe jikoni tu au kwenye kufua nguo? Hii ni mifano michache tu. vitabu vya dini vilishatuwekea migawanyo ya majukumu sahihi kabisa lakini mwanamke wa kisasa yuko against.

Afadhali umesema, majukumu yapo siyo hiyari. Pia katika utekelezaji wa majukumu ndipo kuna kusaidiana utekelezaji wa majukumu. Mwanamke wa leo anadhani kuosha vyombo na kufagia nyumba ni dili sana na kufua, nadhani tukubali mgawanyo wa majukumu bila hivyo wanaume tutaambiwa tuanze kunyonyesha.
 
Why Yummy?

Juzi nilikwua nasikiliza hizi redio Fanya Mizaha...kuna habari ilitoka gazeti nadhani Mwananchi,kwamba kuna kautafiti kanaonyesha 80% ya operations wakati wa kujifungua zinaombwa na wenye mimba, sababu mojawapo ikiwa ni kwamba 'hawataki kuharibu' maungo yao

Jamani jamani acheni matani basi tunakoelekea ni balaaa.......80%!!!!!!!!!!!!!!! nilidhani hii ingekuwa kwa wale ambao hawana option zaidi ya kisu. Ila sio kitu cha kujisifia eti mke wangu alikataa kisu,ina maana hapo hosp alilazimishwa kisu yeye ndio akakataa??!!!
 
Jamani jamani acheni matani basi tunakoelekea ni balaaa.......80%!!!!!!!!!!!!!!! nilidhani hii ingekuwa kwa wale ambao hawana option zaidi ya kisu. Ila sio kitu cha kujisifia eti mke wangu alikataa kisu,ina maana hapo hosp alilazimishwa kisu yeye ndio akakataa??!!!
Yummy, amini usiamini huo ndo ukweli, wengine wanasme 'mimba imenchoisha' na wengine ndo ivo ilimradi sababu kibao! hebu kaa chini fikiria kama sio kweli idadi ya wajawazito wanaojifungua kwa operesheni imeongezeka? Sasa hivi, ni almost 48% ya cases zote za kujifungua kwen hospitali zetu, na ndo ivo 80% ya hizo wanaomba wenyewe.

Msome vizuri Bondpost apo, hajisifii, ila anastate fact kuwa kama hizi ndo stat, then mke wake kukataa kisu ni jambo jema kabisa. it is a fact kwa sababu angeweza na yeye kutaka kisu ili 'asiharibu' maungo yake...umenipata?
 
Hahaahaha kuna watu wanakimbia majukumu hapa. Bondpost unatisha, I salute lazima kwenye familia kuwe na mgawanyo wa majukumu na kila mmoja atimize wajibu wake. Inapotakiwa kusaidiana basi msaidiane kwa upendo. Mwanamke hajui majukumu yake mfano hataki kupika anataka mle chips kila siku, nyumba chafu anataka mm niinamishe mgongo yeye yuko kwenye umbea etc. mimi mwanamke wa hivi nitampeleka wapi. Wanawake zetu sikilizeni, ni hivi ukipendana na mwanaume mapenzi huwaunganisha lkn katika muunganiko huo kuna majukumu yanazaliwa na siyo hiari lazima kuna wajibu unatakiwa kuutekeleza. Ndio maana ukiona mmojawapo kama hatekelezi wajibu wake si ajabu kusikia mambo ya nyumba ndogo(kwa wanaume) au vidumu kwa wadada a.k.a mashostito. Mapenzi yanazaa wajibu automatically na sio utumwa, ni sawa na mm mwanaume nimpende mdada halafu niishie kusema nampenda bila kutimiza majukumu kama baba mfano kumpa haki ya ndoa mapaka aridhike, kuhakikisha ulinzi wake, kuhakikisha anamavazi, anakula etc. Nikijidai nampenda tu hafu hakuna majukumu lazima aote mbawa. gfsonwin, nyumbakubwa deep down in your hearts mnafahamu haya.
 
bila ubishi hii thread naipigia kura in advance..Thread of the year 2012!!
 
ni dhahiri kuwa mwanamke asiyetimiza wajibu wake anaikosea familia yake no matter kwamba umekasirishwa au vipi, kwani mstaarabu atatimiza wajibu wake kisha adai haki yake baadae.

hapa umefunga kazi dada gfsonwin .... huwa napenda sana michango yako coz huwa unaongea kama mama mwenye uzoefu na mwanamke anayejua what she is talking about... hivi mwanamke anaolewaje kama hata hajui kwamba anapaswa kutimiza wajibu fulani ndani ya nyumba in the first place? au 'wajibu' ni kwenda salon?
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin kama ukisoma uzi wangu kama nilivyonukuu hapa chini, naamini utaelewa nilikuwa nahitaji ufafanuzi gani kutoka kwenu... Mimi nimeuliza swali ili sisi wanaume tujue namna nzuri ya kuwa-handle.
Na sikusema kazi za kufua na kupiga pasi ni wajibu wa mke, bali nilitoa mfano tu......... kwani binafsi naamini katika kila ndoa, wanandoa hugawana majukumu kulinga na jinsi walivyokubaliana.........
Mtambuzi nilielewa swali uliloliuliza lakin pia sikutaka kwenda kwenye jibu direct manake ilitubidi tujue kwanza sababu zinazopelekea hayo kutokea. nasikitika kama nimekuwa mpotoshaji wa maana husika ila ukweli ni kwamba nilitaka kwamba nikupe sababu why so ndipo sasa tuanze kujua nini cha kufanya au tunataka nini.

back to the point, wanawake wote hawapendi maudhi hata kidogo, na kama walivyo ni watu ambao kwao kuwajibika ni kitu wanachokipenda sana. wanapenda basi kama mume ukikosea usijifanye mbabe na kuanza kugomba la omba msamaha yatatue yaishe muish kwa amani uone kama hata fanya wajibu wake.

unapokosea wewe kama baba na ukawajeuri hutak hata kuomba msamaha ni dhahiri unamkwaza huyu mama na utapelekea atafute mahali pa kupunguzia hasira zake na ndipo hapo anapogombana na kazi na hata watu wa nyumbani kwake. tunaamin katika maisha ya amani yasiyokuwa ya kibabe na jeuuri kama ambavyo wanaume wengi wanpenda kufanya.
 
Last edited by a moderator:
Taratibu, maana naona umekariri; wengine mamodo humu. Lol. Nikirudi kwenye uzi wako wa hapo juu; ungekuwa unampenda mkeo usingeandika uliyoandika kwenye bold. Maana sidhani kama una refer kwa mke wa jirani na kumuita michelini na maandishi mengine yenye kila dalili za hasira, ni obvious una m-describe mkeo.

Ilikuwa nisome post za watu tu,...hee! bora umeliona hili nyumba kubwa, anaonekana kuwa na hasira sana na wanawake, hata kama wanawake tuna mapungufu and all that ndo ufurike kwa hasira hivyo na huku mkewe ni mmoja wa hao wanawake duuu!
 
Back
Top Bottom