Wanawake: Nahitaji ufafanuzi wenu katika jambo hili……..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake: Nahitaji ufafanuzi wenu katika jambo hili……..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jun 11, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Picha hii haihusiani na habari hii

  Hivi inakuwaje?


  Baadhi ya wanawake wanapowafanyia waume au wapenzi wao jambo zuri, hufanya hivyo huku wakihesabu na kutarajia wapenzi hao waone, watambue na pengine baadae kuwalipa kwa njia nyingine.

  Kwa mfano.

  Mke ana kawaida ya kumuwekea mume au mpenzi wake maji ya kuoga bafuni, anamwandalia chakula vizuri, anamnyooshea nguo zake au anazikagua nguo zake kwa umakini na kuzirekebisha pale zinapokuwa na kasoro na mengine yanayofanana na hayo. Badala ya kuchukulia au kujua kwamba huo ni wajibu wake, hufanya hivyo kama deni.

  Mume anapomkosea, mke huacha kufanya au kumfanyia mumewe mambo hayo kwa maelezo kwamba, haoni sababu ya kufanya hivyo kwa sababu mumewe hana shukurani…………..

  Nimekuwa nikisikia malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wanaume wenzangu wakilalamikia jambo hili, na wanadai kwamba kwa upande wao hata wanapoudhiwa na wake zao kamwe hawasitishi utaratibu wao wa kuacha kodi ya meza lakini wanawake zao huwasulubu kweli kweli wanapoawakosea.

  Hebu fungukeni hapa ili tujue namna nzuri ya kuwa-handle…………………
   
 2. Elijah

  Elijah JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,671
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  dawa ni kutojizoesha kabisa kupigiwa pasi,kuwekewa chakula mezani na kuwekewa maji bafuni
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,846
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi frankly speaking hakuna mwanamke mwenye akili timamu na mtashi na mwenye hekima pia ambaye mumewe akimuudhi ataacha kutimiza wajibu wake juu ya mumewe.

  ila kuna kosa moja tu ambalo huwa lina waputoff akina mama incluiding me, yaani wewe mume wangu umekuja utokako nikakukuta unashombo la mwanamke mwingine wallah! nguo yako utafua mwenyewe. na kuipiga pasi mwenyewe manake huniheshimu mimi.

  sikiliza wanaume mna mambo ya ajabu sana, wake zenu tunavumilia sana. kwani wewe hujawah kuskia mwanaume akidai mimi nafuliwa chupi na mke wangu lakn jana nimeifua mwenyewe? ulimuuliza kwanin?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  gfsonwin nakubaliana na wewe, lakini hapo kwenye BOLD naamini wanaume wengi tunaopanda daladala tutakuwa victim..........Hivi mfano nimekaa siti moja na mdada aliyejikandika vipodozi na pafyum kali, akiniambukiza hayo manukato si nitakuwa kila siku nahenyeshwa jamani...!
  Duh! wanaume tunapambana na mikasa..............
   
 5. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  DU KWA KIASI NINAVYOMPENDA MUME WANGU NA ANVYONIPENDA MZEE MTAMBUZI, HATA AKANIUDHI NIKIENDELEA KUFANYA MEMA ATAJIRUDI TU,SIWEZI ACHA MUME WANGU KATIKa HALI ISISVYO SABABU NI SAWA NA MIMI.MZEE MTAMBUZI NAKUBALIANA NA HOJA YA KO WAPO WANAWAKE WENGI WA NAMNA HIYO,NA JE UKAACHA KUUCHEZEA UWANJA WAKO ,YANI UKAJITOA JE HUONI WAKATI UKIRUDI TENA UANJANI UTAONEKANA KICHEKESHO,CHEZA SIKU ZOTE ZA MVUA ,JUA AU MWEZI ILA MAJI YASIZIDI CHUMVI,UNAWEZZA ACHA KUMSAFI AKARUDI JIONI AMEPIGIWA PASI NA ZA SIKU TATU MELENI chezea wanaume weye!
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,846
  Trophy Points: 280
  hee mtambuz asikwambie mtu harufu ya perfume inazungumzika. labda ungenijibu swali nililokuuliza mwishoni. huu ni ukweli labda wengine watapona kuna wanaume wasio jiheshimu hata chembe. mwanaume anarudi kwake chupi imeliwana shahawa, hapo mwanamke apate jibu gani?

  kwamba alitoka kwa Anet so zile za mwishon ndo zinamalizikia, kasababu ya haraka. akiivua hadi aibu anaona. walah hata miye sifui. wanaume mjiheshimu kosa la kutembea nje ya ndoa lina uma sana na mara nyingi hutupelekea kusema yanini nimfulie wakati kuna wanao mvua?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  gfsonwin nilishindwa kujibu hilo swali kwa sababu niliamini kwamba kuna wakati huwa wanaume wanapenda kuwasaidia wake zao, na kwa mkabala huo, huenda siku hiyo aliona amsaidie mkewe kujifulia chupi yake, sasa kipi cha ajabu hapo?
  Swali hapo ni je kutarajia malipo kwa kila mnachowafanyia waume zenu.... ni haki?

  Binafsi nina mfano, katika vitu ambavyo mama Ngina huwa anachukia ni pale ambapo najua nitachelewa kurudi nyumbani halafu nisimjulishe hata kwa SMS, mpaka anipigie au anitumie SMS kutaka kujua kulikoni....
  Hata nikimjibu kuwa nitachelewa, nikirudi nyumbani nitaandaliwa kila kitu kama kawaida, lakini muda huo nitakuwa napewa vidonge vyangu, nitakuwa nahudumiwa huku nikipewa dozi...............
  Kwa kujua suluba hiyo huwa nawahi kujisalimisha, natuma SMS mapemaa ......... (Sorry honey, will be back home a little bit late today..............) ...................LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,846
  Trophy Points: 280

  sasa hapa @mtaambuzi unakuja kwenye mstari wangu, haya twende sasa unajiskiaje pale ambapo mpaka usemwe ndipo unarekebisha tabia ambayo inamkwanza mwenzio? Kuchelewa kurud nyumbani kabisa ni kosa la kinidhamu ila tusiliongelee manake litaamsha mambo humu.

  lakin kwanini hutoi taarifa? pia kwani unapochelwa kurud home unategemea miye mkeo nnile na nani mezani? hivi kama baba utajifunzaje tabia za wanao kama tu hata kula nao mezani hujawah? wewe kutoka majira kurudi kombra kila siku?

  Kwa mwanamke mwenye hekima sana na busara atavumulia na kuendelea kutimiza wajibu wake kama ambavyo wengi tunafanya ila kwa asiyekuwa na hekima siyo siri umemvunja moyo sana. Makosa mengine ni ya kwenu halafu hapa mnatuangushia kuwa tunataka ujira kweli hii ni haki yetu siye kunyanyasika katika ndoa?

  Anyway kuna kosa ambayo yanumiz mwanamke hata kama utafanya nini lakin you can not control pain. mwache kama ndo njia yake ya kurelease pains ila nanyie msituudhi.
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  gfsonwin kwa hiyo unataka kusema kwamba ni haki mwanamke kususa kumhudumia mumewe iwapo mume atakua amemkose?
  Naona tunarudi pale pale kwamba mnawahudumia waume zenu mkitarajia malipo au kufanyiwa jambo fulani kama fidia...
  Mbona wanaume hawasitishi huduma kwa familia kama bakora ya kuwashikisha adabu pale mnapowakosea?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,846
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi usisahau kuwa mwanamke bado anayo ile dhana ya unyonge bado. Hawez kusimama na ukujibu au hata kukwambia direct kuwa umemkosea. huwaga anabakia akiwa amenyongea tu. sasa na yeye kama njia ya kurelezi tension basi anasusa kufanya kazi zaake kitu ambacho mimi huwa nasema ana ahrisha tu kwani ukweli ni kwamba baada ya muda laazima aje azifanye tena anakuta zimeshalunidkana.

  siyo kitu kizuri lkn kwa kuwa chanzo ni baba husika basi alaumie yeye na siyo mwanamke. Wala tutimizapo wajibu wetu siyo kwamba tunatarajia ujira lahasha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu ambacho hua kinanikatisha tamaa kama kumfanyia mtu kitu halafu yeye haonyeshi appreciation! Honestly binafsi hua nachoka kumfanyia jambo mtu asiyekua na shukrani!
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  although am a man ngoja na mie ntupie neno hapa...
  mapenzi mengi ya kuona hasa kwa sabau tyme(umri) imefika ndio yana haya mambo..kuna majukumu ya msingi ambayo lazima kila mtu ayatimize hasa katika jamii zetu za kibantu

  tatizo watoto wetu wa siku hizi mapenzi ni kusema WAAAAAAAO au KUCHART FACEBOOK au kutuma ka SMS kaoja kabla ya kulala baaasi..hawajui chochote hawa watoto(ma bibie)
  sory kama ntakua nimewaudhi humu baadhi ya watu maana najua wengi wana tabia hizi
   
 13. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tunarudi palepale na kulekule. Hivi kutimiza wajibu wako unadai shukrani? When you love; do you love to give or receive?
  Hayo mambo ndio yanayovuruga mapenzi.
  Nilimsaidia dada mmoja. Tulipoachana aling'ang'ania namba yangu ya simu, nilipomgoma akaanza ooh au nyumbani ..., nilipompa namba yangu imekuwa taabu, bado anadhani naweza kuendelea kumsaidia hadi nimemweka namba yake kwenye rejected numbers.
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kwa sababu wanafanya hayo kwa sababu ya mapenzi, napogombana ule munkari wa mahaba unapungua/kuisha ndo maana huduma zinasitishwa
   
 15. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nikimpata mume labda ntakuwa na jibu kwa sasa kila mtu anafua, kupika, kulala kwao.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Wanawake wanapend kuwa 'appreciated' one in a while hata kwa wajibu wake wa kila siku, inaongeza hamasa lol
   
 17. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi nyie wanaume kwanini mnafanana lakini??!??!!!!????!!!!mna maudhiiii, kwanza muache kuchanganya kitu kinaitwa WAJIBU na HIARI ndio tutaelewana.............hapo kwenye red huo sio WAJIBU wa mwanamke bali ni mapenzi/hiari ya huyo mwanamke kufanya hayo uliyoyataja na pengine kufanya zaidi ya hayo.
  Niliwahi kuambiwa hivi we mwanamke kwanini leo hujanifulia boxers zangu unafikiri nilikutolea mahari ya nini???!!!!hivi kweli unafikiri mimi nitakua na moyo wa kuendelea kufanya hivyo tena wakati nilikua nafanya kwa mapenzi na sio lazima!!!!!
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  wapo wanaokuwa wapole na wanatimiza wajibu wao bila taabu
  lakini dah.....revenge yake iko kwa kukutafutia vidumu tu
  so bora wanaogoma na kununa
  angalau utajua 'now kakasirika umbembeleze'
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mbalu huyo hapo kwenye Bold ambaye anapika na kulala kwao, ngoja uingie kingi maji utaita MMA na sumni utaita THUMNI
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aisee mnaniudhi na hili neno lenu la WAJIBU daah hamjui tu....kwani kabla hamjaoa nani huwa anawawekea maji bafuni? Na kama mnatumia shower inakuaje???
  We The Boss na Mtambuzi hamuwezi kuwawekea wake zenu maji ya kuoga?!na kama mnaweza kufanya hivyo ina maana ni wajibu wenu???
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...