kula kwa tindo
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 1,330
- 323
Watoto wa kiume siku hizi hovyo sana, wanataka miteremko tu ndo maana utaskia 'natafuta jimama linilee...'
Heshima ya mwanaume kazi/kuwajibika...ebo!
Mtaishia kulia lia hivi hivi na kubebesha wengine lawama...
Kajisemea AshaDii, tunakoelekea ni kama wanaume hawatakuwepo! Tunashindana tu kupaka lipgloss na mawimbi na rasta za uzi vichwani
Eiyer unashangaza....
Yaani hutambui hata biblia imesema asiyefanya kazi na asile?
Sasa huyo mume jobless wa kazi gani?
Sitaki kuamini kama wewe fikira zako zote zinakomea kwenye malezi ya familia tu!! Sasa suluhisho lako ni kwamba, tafuta mtoto wa kike(i don't know how)........mlee kama utakavyo then akikua muoe!!!
Husna,usichokijua ni kuwa malezi ni msingi wa mtoto YOYOTE!Ni kama vile nyumba,uimara wake unategemea msingi namna ulivyojengwa,mtoto akiwa na malezi imara hawa watu wa pembeni hawataweza kumbadili huyu mtoto,akiwa na malezi ya kijinga hivyo hivyo,ni kama kuku anapotaga mayai,anaeweza kuzuia yale mayai yasiwe viza ni kuku mwenyewe,akizembea kwenye kuyaatamia yatakua viza tu.Kumbuka yeye hakuyatotoa yakiwa viza!
Punguza jazba kipipi!!
Muinjilisti,inaonekana wewe ndo hujui unaoongea,malezi ya mama na baba ndo nayazungumzia hapa,ni mwehu peke yake atakaeamini hg atamlea mtoto kama mama,wewe wazazi wako hukulelewa nao hilo ni tatizo kubwa na linatuhusu wengi sana,hao unaodai wamehusika kwenye malezi yako kiukweli ni baada ya wazazi kutokuwepo inakua kama vile unapomfuga paka nyumbani kwako ukamnyima chakula ataenda kula majalalani na chakula chakula cha majalalani sio salama!Malezi wazazi kwa mtoto ni ni muhimu sana,hawa watu wengine wamekuja kuonekana kama wanahusika baada ya mama kuyakimbia majukumu yake sasa mtoto anazoa kila kinachokuja mbele yake!
kuna dada mmoja anasoma chuo kikuu 2po nae mtaa mmoja kwa yeye kama huna gari hana tym na ww kwa sasa anao kama watatu na wte wana magari.
Asilimia kubwa ya wanawake wanawaza kuwa na wanaume wenye fedha nyingi, magari mazuri nakadhalika, je ni wanaume wanangapi walivyo navyo hivyo vitu na je, hao wenye navyo wanakidhi idadi ya wanawake wenye uhitaji wa wanaume wenye hivyo vitu. Mwisho wa siku mwanamke kama huyo anahitaji huyo bwana awe wake peke yake huku akiwa kasahau kuwa kampendea mali alizonazo ambapo nyuma yake kuna wanawake wengi wenye kuhitaji bwana mwenye sifa kama za bwana wake.
hebu fanya utafiti wako vizuri maana nijuavyo mimi asilimia kubwa ya wadada wana magari yako WENYEWE, saa ngapi atataka mume mwenye nalo wakati ana la kwake? Ungesema hivi "Asilimia kubwa ya wanaume wanawaogopa wanawake kwa vile wana magari yao wenyewe"
Muinjilisti,sijui kama wewe ni muinjilist kweli ama umelitumia hilo jina kama ID tu,but naamini wewe ni mkristo,what do u mean unaposema mfumo dume according to bible perspective?Unajua au unaimba tu kwa sababu wanawake wenzako wanaimba?Unanishangaza!Unataka kuniambia Biblia inaruhusu mama aende kuzurula huko?Usiniambie anaenda kutafuta hela,hilo sio jukumu lake kwani aliambiwa ATAZAA KWA UCHUNGU sio kula kwa jasho,jukumu la kulea ni la mwanamke kwa mujibu wa maandiko!Hayo mambo yako ya globalaizesheni,ubeijin na haki sawa kamuulize kwanza Mungu kwani kama ni mfumo dume yeye ndio muanzilishi.Nashangaa kwanini huoni umuhimu wa malezi ya mama maybe ni kwa sababu ulilelewa na HG,wanawake wamesababisha matatizo makubwa tangu wayatelekeze majukumu yao!Kumbuka pia mimi sio mwenye thread hii!