Wanawake na ofisi za waume zao.

Wanawake na ofisi za waume zao.

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,522
Reaction score
14,005
Wadau MMU!

Leo naomba niseme kidogo juu ya baadhi ya WANAWAKE wanaosumbua wafanyakazi kwenye OFISI za WAUME zao,nimekuwa nikishuhudia wanawake wengi wakisumbua wafanyakazi kwenye sehemu ambazo waume zao wanazimiliki hasa sekta binafsi,pia hata kwenye AJIRA ikiwa mwanaume ana cheo kikubwa basi hata MKEWE akifika ofisini kwa mumuwe huanza kutojali kama pale ni ofisini mara ataanza kumfokea sekretari kwa kumkataza kuingia ofisini kwa mumewe kukiwa bado kuna mgeni mwingine,pia hujitokeza KERO kwa madereva ambao hupewa kazi ya kuwapeleka nyumbani,saloni,sokoni nk wengi hutumia vibaya nafasi za waume zao na kugeuka KERO kubwa kwa wafanyakazi wa ofisi husika,wafanyakazi wanafikia hatua mpaka kufikia harua ya kufikia kuacha KAZI kwa kero toka kwa mke wa bosi wake,wanawake wengine huanza hata kutafuta michepuko ofisini kwa waume zao hasa MADEREVA.Hayo yote hupelekea ufanisi wa kazi kupotea na kufanya wataalamu kuacha kazi kwa kero za wake wa MABOSI.

Badilika mtoto wa kike,kazi ya mumeo ni yake,heshimu watu ili nao wakuheshimu sio kwa kuwa mumeo ameajiri watu au kuwa na cheo kikubwa iwe chanzo cha kunyanyasa watu..!!
 
Inatokea sehemu nyingi, hata huku nina mifano hai kadha wa kadha. Wanawake wabadilike kwa kuwa wanachangia kuvunjika kwa mahusiano mazuri kati ya ofisi na ofisi ama ofisi na wateja.
 
Naogopa kuchangia akina kongosho watanitoa macho, ila wanaboa kweli sijui wana ugonjwa gani masikini
 
Abiria chunga mzigo wako A.K.A mahaba nichanganye kama bunge la katiba,kama unampenda utamlinda,hyo ni njia mojawapo ya kumlinda
 
Wanawake wengi ni malimbukeni na wapenda sifa,wanapenda sana kunyenyekewa na kuwapelekesha wafanya kazi,
Biashara/Miradi mingi imekufa kwa sababu ya hao akina Eva,mwanaume ukiwa huna msimamo kwenye Biashara/Miradi yako tegemea kufa kibudu.
 
Hii swala liko kwa wanawake wachache ambao ni malimbukeni na wasio na busara. Kwa asilimia kubwa wanawake hawako hivyo. Nimefanya kazi na watu mabosi wengi ambao wake zao walikuws wanaheshimu sana wafanyakazi na hata wakija ofisini hufuata vigezo ba masharti kama wageni wengine
 
1.ukimkuta mwajiri ni mtu na mkewe.M/ke ndio mwenye shida.
2.Ukimkuta mwenye nyumba ni mtu na mkewe.Mama ndio mwenye shida.
3.Ukimkuta baba na mama mkwe.Mama mkwe ndio mwenye shida.
4.....
5.....
6.....
 
Inakera mke kumfata fata mume mahali pa kazi.... Kila mara unakuta mke kaja pasi na sababu sasa bahati mbaya au nzuri secretary awe kifaa kuliko mke wa bosi..

Mmaaaamamaaaa... Utajuta!

Ila kuna mabosi utakuta mke hakanyagi ofisini kwake isipokuwa kwa dharura!
 
Wengi wao ni ulimbukeni wa maisha sanjari na ukosefu wa elimu,hujiona wao ni babu kubwa ile mbaya.

1.ukimkuta mwajiri ni mtu na mkewe.M/ke ndio mwenye shida.
2.Ukimkuta mwenye nyumba ni mtu na mkewe.Mama ndio mwenye shida.
3.Ukimkuta baba na mama mkwe.Mama mkwe ndio mwenye shida.
4.....
5.....
6.....
 
Kwanza mke wangu hajui hata jengo la ofisi yangu linafananaje kwa nje
 
Back
Top Bottom