Wanawake na Ndg wa upande wa mwanaume

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,513
10,404
Jamani wanaume wengi wanalalamika kuhusu tabia ya baadhi ya wanawake ya kutotaka kuishi na ndugu wa upande wa mwanaume. Wengi wa wanawake wa jinsi hii wanapenda tu wakae na ndugu zao, lakini siyo wa mwanaume. Eti sababu huwa ni nini hasa? Naombeni mawazo yenu jamani, kama ilishajadiliwa naombeni link za sredi hiyo nipate mawazo ya wadau.
 
Inategemea!sasa kama mmeoana hata mwaka haujaisha then umejaza ndugu zako kumi ndani ya nyumba mkeo anakosa hata privacy na wewe(mume) inachosha sometimes!
 
Upande wake ni rahisi kucontrol kuliko upande wa mume, maana kila kitu kinakuwa sensitive.
 
Mimi kama sitaki ndugu wa mume wangu waje na wangu wasije tuwasidie wakiwa mbali lakini hii ya kuleta wa kwako wa mwenzako unakataa siyo vizuri, unatafuta maneno mwenyewe.
 
Mimi kama sitaki ndugu wa mume wangu waje na wangu wasije tuwasidie wakiwa mbali lakini hii ya kuleta wa kwako wa mwenzako unakataa siyo vizuri, unatafuta maneno mwenyewe.

Ndo suluhu hiyo......alternativeni matatizo tu hata ukileta dhahabu ndo iwe kitafunwa watasema wanataka copper.....ukileta watakuambia ya wapi........?????Ukijibu utasikia huko wachawi......bora silver

Kama vipi mkae wenyewe na ma kid wenu baaaasii........na wasaidizi wawili uwajali kama ndugu inatosha...watakuheshimu na wala hutojuta na watoto wako wataenjoy sana kuliko kununiwa na mtu kisa umekuta anaangalia katuni wakati wa taarifa ya habari ukamuambia muangalie hiyo NEWS kwanza
 
ndugu walikua nasi..sasa waniweza...wamegeuka maadui namba moja..ongopa sana kusaidia ndugu..wengine hawana shukrani
 
Ndo suluhu hiyo......alternativeni matatizo tu hata ukileta dhahabu ndo iwe kitafunwa watasema wanataka copper.....ukileta watakuambia ya wapi........?????Ukijibu utasikia huko wachawi......bora silver

Kama vipi mkae wenyewe na ma kid wenu baaaasii........na wasaidizi wawili uwajali kama ndugu inatosha...watakuheshimu na wala hutojuta na watoto wako wataenjoy sana kuliko kununiwa na mtu kisa umekuta anaangalia katuni wakati wa taarifa ya habari ukamuambia muangalie hiyo NEWS kwanza

well said,kuishi na ndugu ni kujitafutia lawama,huwa hawaridhiki hata uwape dunia..
 
Sio wote ni baadhi yao tu,, kuna wanawake wengne wanapenda sana ndugu wa upand wa mwanaume eeeh na kuna wengne hawatak kabisa kusikia ndugu upand wa mwanaume utakuta mfano akija kutembelea pale ndugu wa mwanaume atawapikia dagaa mpaka wakome,,ila wakija ndugu zake ni mwendo wa kuwalisha vyuku kwa kwenda mbele..'
 
Nadhani ndo namna ya kuwaambia waondoke, siwapendi
 
kiukweli maranyingi ndugu wa mume wanajidaigi wanahaki na wanamamlaka juu ya mali (zenu) ambapo wao wanaamini ni za ndugu yao, kuepusha shari ndugu wa pande zote wakae kwao muwasaidie wakiwa huko huko, HERI UKAE NA MTU BAKI KULIKO NDUGU.
 
inategemea na tabia ya ndugu...
mwingine akija kwako anajifanya yeye ndo mwenye nyumba....
hafuati taratibu za nyumba husika...
ukimuelekeza maneno yatasambazwa ukoo mzima kuwa mke mbaya..
na upate mwanaume mashkolamageni atasikiliza ndugu zake.....
ukija kushtuka hakununuliwi kitu ndani mapaka adiscuss na nduguze,..............
mkipanga anaenda kutaarifu nduguze wanapangua......................

au unakuta ndugu hashiriki kazi hata moja ..............
anataka mpaka maji ya kuchambia atengewe...................
nani anataka hizi kero........

ingawa kuna ndugu wachache wastaarabu
hadi wakiaga unatamani warudi........................

na pia kuna wanawake wachoyo....na watata hawa wakiona wageni/ndugu wa mume wanuna...........................

solution ikiwezekana ndugu wote wawe wa mke au mume wasaidiwe huko huko walipo.............
maana undugu lawama..............

kiukweli maranyingi ndugu wa mume wanajidaigi wanahaki na wanamamlaka juu ya mali (zenu) ambapo wao wanaamini ni za ndugu yao, kuepusha shari ndugu wa pande zote wakae kwao muwasaidie wakiwa huko huko, HERI UKAE NA MTU BAKI KULIKO NDUGU.

Nimependa hapo pekundu
 
Ndoa ni ya watu wawili na si ya ukoo!
Si ndugu wangu wala wa mume ambao watakaa labda watoto ambao ni yatima. Wengine kama ni kusaidia wasaidie huko waliko; hii huepusha magomvi ndani ya familia!
 
Me sometimes nahisi ni roho mbaya tu. Kama msaidiwa hana sehemu nyingine ya kusaidiwa je?
Akileta nyodo za kitoto ni jukumu langu na mume wangu kumuweka sawa aelewe kuwa yeye pale ni second best, the first best is wife/mama wa nyumba.
 
inategemea na tabia ya ndugu...
mwingine akija kwako anajifanya yeye ndo mwenye nyumba....
hafuati taratibu za nyumba husika...
ukimuelekeza maneno yatasambazwa ukoo mzima kuwa mke mbaya..
na upate mwanaume mashkolamageni atasikiliza ndugu zake.....
ukija kushtuka hakununuliwi kitu ndani mapaka adiscuss na nduguze,..............
mkipanga anaenda kutaarifu nduguze wanapangua......................

au
unakuta ndugu hashiriki kazi hata moja ..............
anataka mpaka maji ya kuchambia atengewe...................
nani anataka hizi kero........

ingawa kuna ndugu wachache wastaarabu
hadi wakiaga unatamani warudi........................

na pia kuna wanawake wachoyo....na watata hawa wakiona wageni/ndugu wa mume wanuna...........................

solution ikiwezekana ndugu wote wawe wa mke au mume wasaidiwe huko huko walipo.............
maana undugu lawama..............

Kweli atachukiwa kwa tabia hiyo - hapo pekundu
 
wapendwa kwa family zetu za kiafrika kuishi na utitiri wa ndugu ni mambo ya kawaida ingawa kwa kweli ni mzigo wa mavi! maana hakuna namna utaondokana nao salama, katika kuishi kwangu na ndugu wengiiii wa pande zote mbili nimejijengea ndugu maadui wengi kuliko ndugu marafiki! ndugu lawama jamani, na sio wote wanaokuja kuhitaji msaada kula wale ndugu wamechoka tu kukaa huko waliko wanaamua kuja kukaa kwako wakifika wanaishi kama paka wa hotelini hawajigeuzi labda wakati wa kula ukiiuliza wamekuja kupumzika!! tena na midomo mireeefu na housegirl wako wanakufukuzia kwa midomo yao, watoto wako wanabadilishiwa maisha anachotaka aunt ndio na mwanao atakachoangalia kwenye TV mara watoto walale chini mgeni alale kitandani to mention a few lakini eeeh kwa kweli mnaaoolewa sasa mkiweza hebu kaeni mke na mume tu na watoto wenu muone raha ya maisha! mie ck hizi watoto wakubwa wako shule/chuo naishi na mume tu na houseboy sitaki ndugu kabisa maisha raha mustarehe utadhani tumeoana jana
 
Back
Top Bottom