Wanawake na mikopo/vicoba

Wanandoa ni jambo jema kushirikishana kwenye masuala ya mikopo. Kati yenu mwenye wazo la kukopa basi aliuze kwa mwenza wake, lipate baraka ikibidi hata kwa familia.
 
Demiss una vikoba vingapi?? Je huwa unachukua pesa za matumizi kupeleka kwenye vikoba?? Maoni yako tafadhari
Mm nina kikobaa kimoja tu tena cha wafanyakazi wenzngu na nimemshirikisha mme wangu Mshana siku nikiwa nimekwama kupeleka Hela ya kugonga ananipaaaa

Na piah ikifika zamu ya kuchukua mkopo nachukua nampa mme wangu anazungusha kwenye biashara .

Mimi ni muwazii na mme analitambua hilo
 
Safi kabisa malkia wa nguvu.
 

Shida ya wake wengi sio wawazi. Kikinuka ndio aibu inakuja kwa mume
 
Hii kitu mwenyewe huwa inanishangaza.
Unakuta mtu hana biashara wala chochote cha kumuingizia kipato na hapohapo ana mkopo vikoba hela ya,rejesho hana anaenda kukopa huko brac sijui akalipe vikoba.
Yaani ni mzunguko wa kukopa huku alipe kule sasa unafikiri bajeti ya chakula nyumbani itakuwaje?
Hapo lazima bajeti iyumbe,tunasikitisha kwakweli.
 
[emoji23][emoji23] umenikumbusha hapa mtaani kwetu kuna kundi la wadada hodari kwa mikopo ya wahindi hatari...wakishapata mikopo wanaenda tunza kwenye sherehe siku za malipo sasa utawaonea huruma..ila hawakomi
Hao ndo wadada wa mjini.
Yaani ndo maisha yao,wakope wakajionyeshe kwenye masherehe
 
Mwanamake wa aina hiyo ana hujumu uchumi wafamilia na kimgundua lazima nimtumbue
 
Yaan nakusimulia kitu nimeonaa jamani mama hana raha kisa mikopo na vicoba
 
Bora uweke wazi tu
 
Ndio mpaka inafikia wageni wamekuja anaanza kopa pesa kwa wageni ili apike chakula,tabia gani hiyo,,wafungulieni vibiashara wake zenu
 
Wanawake tunatofautiana aisee mi napenda kula,tule vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…