Wanawake na mikopo/vicoba

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
16,607
Reaction score
27,607
Wanawake mnapewa pesa za matumizi yaani mahitaji ya nyumbani wewe unachukua pesa unapeleka kwenye vicoba sijui marejesho.

Mara ulichukua mkopo Brac basi pesa ya matumizi inaishia huko, huku nyumbani unabakia kuhangaika kutafuta na kukopa pesa kwa watu za chakula mnavyofanya sio vizuri kabisa.

Wengine mnaingia huko kwenye vicoba hamna hata shughuli au biashara mnategemea peza za matumizi za waume zenu, inakuwaje uingie huko kwenye mikopo au vicoba halafu huna kitu cha kukuingizia pesa?

Kuna huyo mama kapata mgeni wanaishia kumuomba mgeni mara hiki mara hiki kisa tu pesa kapeleka kwenye vicoba, umeme unaisha inabidi mgeni anunue, wengine hadi ada za watoto mnapeleka huko.

Hivi hivyo vicoba imekuwa fasheni kiasi kwamba usipokuwemo ni vibaya mno, basi kuwa kibiashara ili usihangaishe watoto ukipeleka marejesho unatoa pesa kwenye biashara yako.

Kuna mwingine nae hapa kaniomba pesa sijui arejeshe huko kwenye vicoba vyao nimemwambia sina, mtu hana biashara unajiingizaje huko.

Mnakosea sana kuwa na kitu cha kukuingizia pesa ndio ufanye hivyo vicoba vyako na uchukue mikopo, mnachukua mikopo ya Brac roho zinakuwa juu juu hamna hata raha wala furaha.

Kina baba shtukeni pesa za matumizi zinapelekwa vicoba na kurejeshwa kwenye mikopo, watoto wanakuwa hawali vizuri.
 
Wanawake kwa kweli wanaongoza kuchakachua bajeti za nyumbani, wengi ukisafiri ukamwachia hela ya matumizi hahaaaa menu haifanani kabisa na hela uloacha, inakuwa chini ya kiwango, kwa siye wapenda mapochopocho tunajua tu hapa tiyari hela ishapangiwa matumizi mengine.
 
Mama Sabrina kwa upande wangu vikoba sio kitu kibaya kwa wanawake walio na kazi na hata wasio na kaz.

Kwa walio na kazi kwao haina tatizo hata kidogo kwa vile wana uhakika na pesa ya marejesho na wala hawatumii za matumizi kwa ajili ya nyumbani.

Kwa hao wasio na kazi nao pia wapo sahihi kujiunga na vikoba ila TATIZO lao moja hawatushirikishi wanaume zao kwa baadhi yao lakini ndyo maana waweza acha pesa nzuri tu ya matumizi mwisho wa siku mnakula dagaa kwa kwenda mbele.

Cha msingi wawe wanatushirikisha tuone kama kuna uwezekano wa kumuongezea bajeti ili iweze kukidhi na vikoba vyake.
 
Wanawake wengi sana hupenda kuchukua mkopo bila mpangilio. Yaani hana kitu chochote cha kufanya na huo mkopo Wala hajui ataulipaje. Anachukua tu kwasababu upo. This is extremely stupid!! Mtu anakopa anaenda kununua vitenge, hivi huyo mume ukimwambia akusaidie kurejesha akikuuliza umefanyia nini hela utasemaje?
 
Hahahahahaha, kabisa mkuu
 
Hakuna ubaya kuwa kwenye vikoba ,,ila kwanini apeleke pesa ya matumizii watoto wanakuwa wanakula kwa kubahatisha mi ningekuwa ,wanaume nakuwa nanunua kila kitu ndani hadi nyama najaza kwenye friji,,,ndio maana kuna baba mmoja niliona anafanya hivi ananunua kila kitu samaki akinunua ananunua hata 30 hataki mchezo kwenye chakula na wanae
 
Ndio muwe mnahakikisha chakula kipo ndani maana hivi vicoba vinawatia wehu wanawake
 
Hapo ndipo wanawake wanapofeli .
 
Hapo ndipo kwenye tatizo haswaaaaaa,
 
Yaan unachukia mkopo halaf hujui utaurudishaje akili za matope hizo kabisa,,kuchukua mkopo kunahitaji akili
 
Hahahaa. Umeongea kweli tupu Mumy. Kimtaani mtaani walio vikoba wengi ni wale wasio hata na shughuli ya kufanya. Nishawahi jiuliza siku moja wanatolea wapi hiyo hela nikaja kugundua ni ile ya kubana matumizi pale waume zao wanapoacha pesa iwe ya kula au ya kununua vitu vya jumla vya nyumbani.

Kwa upande mwingine nawapongeza kwa kujiongeza japokuwa wengi wakipata hizo hela zinaishia kwenye kununua madera na vitu visivyo vya maana na sio kuifanyia japo biashara ili ipate kujizalisha kwa kutegemea kesho atabana nyingine. Lol
 
Hajar nawe upo kwenye vikoba?? Njoo utoe maoni yako hapa Tafadhari kwa heshima na taadhima.
Hapana bado sijajaribu kuingia huko.

Ila wapo wengine wanavitendea haki kwa kweli na hao ni wale wanaovitumia vile ipaswavyo yaani wanakopa huku wana biashara pembeni yaani kila wakichukua basi anaongeza kwenye mtaji. Hongera kwao.
 
Hapana bado sijajaribu kuingia huko.

Ila wapo wengine wanavitendea haki kwa kweli na hao ni wale wanaovitumia vile ipaswavyo yaani wanakopa huku wana biashara pembeni yaani kila wakichukua basi anaongeza kwenye mtaji. Hongera kwao.
Yesi yupo dada yangu mmoja hiv wa hiari wakati nimemaliza chuo tu nikaenda fild hapo akanipokea mwisho nikapewa na kazi jumla hapo hapo.

Sasa alikuwa na vikoba mpaka sometimes anachanganyikiwa jinsi ya kurejesha lakin mwisho wa movie akanunua kiwanja, akaanzisha biashara ya tgo pesa na mpesa, akaanzisha na biashara ya icecreem kwenye kile kibaiskeli.

Hao sasa ndiyo wanaitumia vyema vikoba.
 
kipi bora mwanamke anayeweka hela kwenye vikoba au anayecheza biko?
 
nazijua vizuri sana hizi shughuli za vicoba na hapa nilipo muda si mrefu naelekea nmb kuwashawishi ili wawape wateja wangu mkopo waweze kujiendesha vizuri na mimi kama mdhamini wao.
kiukweli waache wacheze hata kama watoto wanakula utumbo badala ya dagaa kwa kuwa hii ni hatua ya awali ya mama kujifunza uwekezaji kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
pia inamwongezea mwanamke ujasiri na uwezo wa kuelewa mambo mengi kwa kukutana na wanawake wenzie ambao wako tayari kumsaidia wakati wa shida.
si kweli kuwa watoto hawali vizuri hapana bali hawali kwa urafi kwa kile kisichohitajika!
ukiwa na mwanamke anayecheza vicoba chakula chenye chumvi nyingi na pilipili kinakuhusu ili unywe maji ya kutosha na mara nyingi nyumba hizi hawana magonjwa kama sukari hasa kwa watoto.
mengi nitajadili kadri tunavyozidi kubishana wacha nijipange nikafanye kazi niliyolipwa.
vicoba oyee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…