Wanawake na mbinti wa mitandaoni tuendelee kujipodoa tu

Wanawake na mbinti wa mitandaoni tuendelee kujipodoa tu

Ikohumo

Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
6
Reaction score
15
siku za nyuma nilileta uzi wangu humu ambao ulisema "natafuta baba atakaye kuwa baba wa mtoto wangu"
Walijitokeza wanaume wengi wao walikuwa mbali na mkoa niliopoa, ila kuna mmoja tulikuwa wilaya moja. Huyu ndiye nilimuona anafaa sana.
Alinitumia picha zake ila mimi sikumtumia nikamwambia nitakutumia picha kabla ya siku moja kuonana.
Ilikuwa siku ya ijumaa nikatoka kazini nikaenda kijijini huko nilipiga picha nyingi nikiwa nalima, nakamua, niko kisimani kama mjuavyo maisha ya kijijini wale walioishi kijijini wanajua na picha hizo nilipiga nikiwa na mwanangu.
Siku ilipowadia akaniomba picha nikamtumia aisee alinipotezea nikawa nampigia simu hapokei, anapokea siku akijisikia, nikutuma msg hajibu na anajibu kwa kujisikia, nilimbembeleza tu basi tufamiane tu inatosha tupo wilaya moja hilo akakubali na akanipangia siku ya kukutana naye, nikasema sawa.
Siku hiyo niliuvua hiba yangu ya ualimu nikauvaa usekretali, nikaenda na mtoto wangu, aliniuliza mara mbili mbili ni ww au ni mwingine, nikamjibu zoom hizo picha uone ni sisi au ni wengine. Tukapiga story sana baadaye tukaagana kila mtu akarudi alipotokea sasa ni zamu yake. Sipokei wala sijibu msg zake, J tumeshajuana hiyo inatosha
Wanawake ukituma picha jipondoe tu, ila ukiwa na malengo ya kumtafuta mtu wa maisha hebu jiweke katika hali ambayo atakupenda hivyo hivyo asikupende sababu za picha ulizojipaka make up.
 
Hahahaha umenichekesha saana,ila hiko kipomo chako hapana aiseee !!!!! Hata kama mim ndo nngekua huyo kaka ningekimbia aiseee picha unakamua khaaaaa......
 
[emoji848]
tapatalk_1540037290463.jpeg
 
Ni Mara ngapi tuwakumbushe kuambatanisha picha katika nyuzi kama hizi Ili kuleta msawaziko wa akili.ingefaa na sisi tuone hizo picha ili kukamilisha jumbe Yako
 
Acha ku fake maisha, be Real

Mbona hujiamini na status ya kazi yako, wapo wengine hawapendi mke anaepiga kazi so uki fake huna kazi akakuelewa halafu akkajua huna kazi anaweza kukutema vile vile
 
Kwa mwandiko huu, wewe haukua na haja ya kupata baba wa mwanao, bali ulikua kwenye utafiti wa kujua jinsi wanaume wanavyo weza wakakupokea ama kuku kubali kwasababu ya muonekano.
Haya sasa, ebu tuambie nini kinafuata baada ya hapo...[emoji53] [emoji45]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom