Wanawake na matiti yao...

Wanawake na matiti yao...

Hivi kwa nini watoto wa kike
wakisha zaa huwa hawaya thamini
matiti yao??? .. Jana hv wakati
nipo kwenye gari kuna dada
mmoja hv akatoa titi lake akawa
anamyonyesha mtoto wake .. Mi
nilikaa nae siti moja nikamwambia
dada ingekuwa vizuri ungemfunika
na baby show au hata na kanga
hizo sio vizuri maana sisi
wanaume tumeumbwa tofauti
wengine wakiona matiti tu hali
inakua mbaya afu wengine pia
tunaona kinyaa kuona maziwa
hayo mtoto anayonyonya .. Daah
basi yule mdada alinikataa jicho
hilooo Yani Obtuse angle kisha
akanipiga msonyo huuuuoo
sijawahi usikia .. Aah ilinibd
nishuke kituo kinachofuata ...

Eti wanawake jamani kwanini hamthamini matiti yenu baada ya kuzaa.

hahahaha jana ulionja Chungu ya bibi yaan hapo ndo ujifunze kuachana na mambo yasiyokuhusu,unadhan wengine hatuyaoni??,tunayaona tunaacha,hata mimi jana niko kwenye daladala nimekaa na dada ambaye alikua akimnyonyesha mwanae,ila kwakua halinihusu nikamuacha,na si mara 1 mdau
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahhh mzee wa chungu cha bibi mtu mzima ilikuwa mdadi umekupanda nn hata ukapigwa msonyo labda alihisi unataka kunyonya na wewe unajua kaka hukufanya vby kumwambia ila ndio tatizo la wanawake wa ki tanzania na si waafrika wanatabia mbaya wanaona wakizaa na kunyonyesha thamani imeshuka ndio ishu yenyewe ilivo
 
Hahahahahahahah ningastuka wewe hali ilibadilika kuwa mbayaee sio!!
 
Na kuna Wanawake Wamejaaliwa akitoa ziwa kumnyonyesha mtoto ziwa limejaaa zuriii ki ukweli si vema tutembeege na Mitandio hata ya Madera ile , Mwanamke Stara Jamani ......:thinking:
 
utamaduni unabadilika lakini mbona hatuvai magome ya miti.kwanini asijifunike na kanga

Nakubali utamaduni unabadilika tuna move forward na positive things vingine tunaacha. Breast feeding ni kitu muhimu. Perception ya kuangalia maziwa kwa mwafrika haiwezi kuwa sawa na jamii zingine hasa wakati wa kunyonyesha mtoto!
 
Ki ustaarabu ukinyonyesha vizuri ufunike, ukiwa nyumbani kwako unaweza kujiachia.
 
Hqpo umeona titi, je ukioneshwa mshundundu si ndio ungezirai ndani ya daladala kwa mfadhaiko...
 
Hivi kwa nini watoto wa kike
wakisha zaa huwa hawaya thamini
matiti yao??? .. Jana hv wakati
nipo kwenye gari kuna dada
mmoja hv akatoa titi lake akawa
anamyonyesha mtoto wake .. Mi
nilikaa nae siti moja nikamwambia
dada ingekuwa vizuri ungemfunika
na baby show au hata na kanga
hizo sio vizuri maana sisi
wanaume tumeumbwa tofauti
wengine wakiona matiti tu hali
inakua mbaya afu wengine pia
tunaona kinyaa kuona maziwa
hayo mtoto anayonyonya .. Daah
basi yule mdada alinikataa jicho
hilooo Yani Obtuse angle kisha
akanipiga msonyo huuuuoo
sijawahi usikia .. Aah ilinibd
nishuke kituo kinachofuata ...

Eti wanawake jamani kwanini hamthamini matiti yenu baada ya kuzaa.

Sasa ulijuaje ni msonyo?
 
Jamani hivi shule bado hazijafunguliwa?hii thread kama ya mwanafunzi ambae hana majukumu na hajui uzuri wa familia.
 
Mimi napenda sana nikiona mwanamke anamnyonyesha mtoto.

Biologically ni kosa kumfunika mtoto wakati wa kumnyonyesha maana hataweza kupata hewa ya kutosha.

Kama wewe una tabia ya kumfunika mtoto na mtandio au na nguo yoyote ile unapaswa kuacha mara moja.

Na ukiona mtu anapata hisia kwa kumuona mwanamke anayemnyonyesha mtoto jua fika kwamba ana matatizo ya akili na mtu kama huyo anaweza kupata hisia hata akimuona mtoto mdogo akiwa uchi.
 
sioni shida mama akimshika mtoto wake vizuri na kuanza kumnyonyesha kwenye daladala. Mimi huwa nawasaidia kubeba na mizigo mingine ili isiwatinge wakiwa kwenye kazi hiyo. kinachonikera ni pale tu mama anapokuwa amemshika mtoto wake hovyo hovyo na kuanza kumnyonyesha. Ukiona mtoto analilia kunyonya maana yake njaa inamuuma. kumfunika pia kuna umuhimu wake lakini ukifuatilia sana starehe ya mtoto ni pale anaponyonya huku anauona uso wa mama yake.
 
Tunayathamini sana. Wewe tu Sema ugojwa wako uko kwenye hayo matiti.

Nyie ndo Namba moja kwenye gari Mtoto akilia utasikia, " dada si umnyonyeshe Mtoto au si wako?" Kosa langu ni lipi sasa Nikitimiza wajibu wangu kwa Mtoto ili asilie.

Kwanza Uende mzazi katembea mda mrefu Mtoto analia kafika kwenye hiace anaona ampe Mtoto haki yake, sasa amwache aendelee kulia wakati nyonyo IPO?!!
Hahahaaaa, kwa hiyo jamaa anamwambia mwanamke amnyonyeshe mtoto ili aone matiti?
 
Tamaa mmeziweka mbele sana, mtakuja kutamani hata mama zenu, dada zenu na ndugu zenu, heeee, dar na joto hili umfunike mtoto na mnguo eti kuna mtu mzima anawaka tamaa ya mama anayenyonyesha, aibu yetu kama taifa
 
matiti ndio unalia ....tena mtoto ana nyonya....
 
Back
Top Bottom