Inaweza kuwa kweli wanapenda magari au watu wenye magari lakini pia kwa upande mwingine kwa mazingira ya kwetu kibongo kibongo usafiri ni shida hivyo ukiwa na gari uwezekano wa kuombwa lift unakuwa mkubwa sio kwa kina dada wala kina kaka ila mara nyingi vijana wengi kabla ya kusimama huwa anamfanyia tathmini mrembo na kama analipa anasimama na kama amesimama na mwanaume anapita kama hawajaona hata kama wameomba wote na kwa kuwa safari ni ndefu kidogo ni rahisi kwa wewe ukiwa na gari kurusha ndoano tofauti na kama umemkuta dada humjui hakujui alafu utake kuongozana nae lazima atakupa za uso but ukiwa na gari kuombwa lift ni lazima tu iwe mwanaume au mwanamke atajaribu kukusimamisha(hapa gari inakuwa kama tool ya kutongozea), kwa mzingira kama haya utakuta lengo la kwanza lilikuwa lift lakini kadri unavyomzoea kwa kuchukua contact mnahamia upande mwingine tena wa mahusiano hasa ukizingatia mwanzoni utavyo-adjust budjet ya mafuta kwa kuongeza fungu kwa ajili yake kwa kumfuata popote alipo but ukimpata mwisho wa siku unaanza kupanga na root ambazo zitaku-favor katika matumizi sahihi ya mafuta
Sababu nyingine gari wakati mwingine inaleta imani kwamba huyo jamaa ana shughuli ya kufanya mjini hivyo kwa wale wanaoangalia criteria hizo inakuwa rahisi kuwa attracted. Hata kina kaka nao siku hizi huwa wanapenda wadada wenye magari alafu yeye anajifanya kujaza mafuta na kupeleka garage kumbe kudunduliza kumemshinda