Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Salaam!
WanaJF, wanawake (mabinti, wadada, wamama, visister du) wanapenda sana magari. Hii tabia imeenea na kuambukizwa sana mijini, tukianza na Dsm , Moshi, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Arusha. Hawa wa Arusha wao wanapenda sana "SUBARU FORESTER zenye turbo", mpaka kuna kagroup fulani kanaitwa SUBARU KASKAZINI. Cha ajabu siyo mafundi na hata tu kuendesha wengine hawajui.
Mwanaume au kavulana kakishanunua tu gari, kinakamata wasichana sana. Utakuta gari yenyewe ni Starlet, Vits, Passo, Ist namba A au B tena za mkopo. Njemba mjini zinamiliki vigari vidogo vidogo ambavyo wanawake wanapenda sana. Wanakula bata na visichana vizuri sana mjini.
Mwanamke kuwa na mwanaume mwenye gari hata kama nyumba za kuishi. Ni heri apande gari, kulala itajulikana mbele kwa mbele. Siku hizi mwanamke akishapata tu kazi, anakopa na kununua kigari chake ili amtambie mwenzie mjini. Ukishakuwa na gari, kwisha habari yake. Sijui ni nini hii tabia jamani.
Maisha mpaka uwe na gari ya kutembelea? Maisha mpaka bwana wako amiliki gari? Na wengi wamekuwa washauri wabaya kwa waume zao, huwashauri kununua magari badala ya kuwekeza kiuchumi.
Wanawake acheni tabia ya kupenda penda sana magari, mnatuudhi sana sisi ambao tunamiliki Boksa. Wanaume wote ni sawa. Acheni ubaguzi.