Wanawake muwe mnaeleweka mnataka nini hasa

Wanawake muwe mnaeleweka mnataka nini hasa

Kuwa katika mahusiano na mwanamke anayetegemewa na ndugu zake kipesa au anaonekana kuwa ndiye mwenye 'akili',anayeoongozwa na Mama au dada zake au yule wa mwisho nayo ni changamoto. Ukiwa na ugomvi ndani basi familia nzima iko nyuma yake hata kama yeye ni mkosefu.

Alafu hutumia mtoto au watoto kukupa wakati mgumu.
 
Mimi ninge kushauri usipoteze mda na hao wa dudu hata kuoa usieoe tena ni wale wale, tafuta pesa ulee mwanao tu, utaenjoye maisha uko unako elekea unatafuta stress bure sie tunajutia kwanini tuliingia huo ujinga majitu gani yasio kua na shukurani.
Dah ndugu unamachungu.
 
Wanaume wenyewe hamjielewi !!
Kamq mwanamke anataka uhuru wa kuchati na x wake,,,au kugawa namba kwa mtu tena wamekutana kwenye interview na mwanaume wake yupo...unadhani sentensi yako iko sahihi...!!
 
Kuwa katika mahusiano na mwanamke anayetegemewa na ndugu zake kipesa au anaonekana kuwa ndiye mwenye 'akili',anayeoongozwa na Mama au dada zake au yule wa mwisho nayo ni changamoto. Ukiwa na ugomvi ndani basi familia nzima iko nyuma yake hata kama yeye ni mkosefu.

Alafu hutumia mtoto au watoto kukupa wakati mgumu.
For sure..kaka, usemayo ni kweli kabisa. Na huyo alikuwa ni wapili kuzaliwa kwao, na wamezaliwa girls wawili tu. Yeye ndio mkubwa
 
Habari wanajamvi.
Juzi Kati nilileta infor humu kuhusiana na mwanamke nilietaka kumuoa,
Mambo aliyo nifanyia na mpaka ikabidi suala la ndoa life,
Yeye aendelee na maisha yake na Mimi na maisha yangu.
Japo kuwa alibaki na mtoto wangu. Mimi niliamua kukaa kimya kabisa.
Sababu nikishatoka Tena kwa style hiyo aliyo nifanyia kutaka kunichonganisha na ndugu zake.
Niliondoka mazima katika maisha yake na nikasema abadani sitothubutu Tena kurudi na hata kumtext Wala kumpigia simu.
Nashukuru Hilo nilifanikiwa.
Sasa mwezi was tano tangu uanze kumekuwa na missed calls nyingi Tena za mfululizo.
Kwa bahati mbaya nilikuwa sipokei simu hizo...Bali nilikuwa naishia kuuliza WEWE NANI?
Cha kushangaza text hiyo ilikuwa haijibiwi.
Sasa juzi Kati hapa namba hiyohiyo ikanitumia ujumbe mfupi wa maneno ukisema..,.



."Hello sir ulikuwa unajisifia kuwa unaoa, vipi umeshaoa au hela ya shela umekosa"

Nilifahamu Ni yeye kutokana na maneno sir, unajisifia na kuoa.

Sanabu Ni kuwa nilipoachana nae nilifuta kila kitu.
Na sikumwambia kitu chochote Wala kumtukana ama kumtambia Jambo baya.

Nakumbuka tu kipindi anazingua kwa maneno ya kejeli mm niliishia kumwambia kuwa....

"Ubaki ama uondoke bado Mimi maisha yataendelea tu na haimaanishi ukiondoka nitakosa wa kuoa"

Nashukuru mola nina mpenzi mzuri anaenipenda A to Z na hana tabia mbovu na Mola akijalia by mwakani tunaweza badili status zetu.

Sasa, huyu binti anashida gani Tena mpaka aanze kunitumia text za ajabu hizo...

Kibaya zaidi Mimi Sina muda wa kujibu txt zake na sijawahi waza Kama nitajibu ujinga Kama anaoufanya.

Mwenzenu ndio huyo kaanza kutuma text za hovyo wakati hapo alipo Ni degree holder, badala ya kufikilia namna ya kusaka pesa maisha yaendelee anafikiria namna ya kunitumia text za ajabu ili nimjibu hovyo awaambie familia yake waje juu

Et ooohhhh...,
" kwanini unamjibu ovyo mwenzako"

Jamani ukipendwa pendeka, hata Kama kwenu wanauwezo kiasi gani utabaki kupendwa Kama mwanafamilia na sio upendo wa kulala mkiwa uchi.

Aache ujinga akae alee mtoto....asubiri nije nimlipie ndio anipe nimuone sikui itakuwa mwaka gani.
[6/7, 1:47 PM] Mwiza: NDOA ZA UKEWENZA KWA MUJIBU WA WAKURYA:

Wakurya ni jamii inayojihusisha na kilimo pamoja na ufugaji ingawa kufuga ni sehemu kubwa Sana kuliko kilimo .

Wakurya wanaishi kwa Koo na wanatambuana kwa Koo mfano Waryachari,Waryanchoka,wanyabhasi,watimbaru,wasweta ,waireghe n.k .

Wakurya halisi wanaishi milimani ni wafupi na Wana miili iliyojengeka vizuri ,miili mikavu yenye nguvu.Wapo baadhi ya jamii ya wakurya warefuu Tena warefu haswa kama watimbaru na wasweta.

KUNA AINA TATU ZA NDOA ZA KIKURYA .

1.Ndoa za mwanaume na mwanamke ,hizi ni ndoa za kawaida kama watu wengine na jamii nyingine.

2.NYUMBA NTOBHU

Hii ni aina ya ndoa ambayo mwanamke anaoa mwanamke mwenzie.

Msininukuu vibaya na kuihusisha ndoa hii na usagaji ,someni kwa utulivu .
Ikiwa umeolewa na hukuzaa ukaachika au tu hujaolewa mpqka ukafika kwenye umri flani km 35+ hujapata mtoto ,basi jamii yako itachanga ng'ombe na kukujengea boma ambapo hao ng'ombe baadhi utawatumia kwa kuchumbia na kutoa mahari ili upate mke ambae lazima awe chini ya miaka 20 .

Mke huyu ataishi kwenye boma lako lakini kwenye kijumba Cha peke yake (Kuna kuwaga na vimisonge flan vinajengwa)

Utawajibika kumtunza kwa chakula mavazi n.k yeye atakuita mama.

Kuna namna mbili za kuruhusu huyu mke kukuzalia watoto .

1.Sheria za kimila zinaruhusu jumping point mwanaume yoyote bila kujali kaoa au kaolewa atakuwa anakuja kulala na MKE wako mpaka atakaposhika ujauzito,baada ya kupata mimba huyo bwana haruhusiwi kukanyaga hapo teeena...hata mtoto akizaliwa hapaswi kujihusisha nae vinginevyo wazee wa kimila watamuadhibu kwa kulipa faini ya ng'ombe ,mbuzi au kuchapwa viboko na km ni mkaidi atapigwa mapanga.

2: Unaweza kumuacha MKE huru akatafuta mimba anapojua yeye ,Yani ilimradi aje na mimba.
Mtoto akizaliwa ataitwa kwa majina ya ukoo wako na atakuwa ni mtoto wako halali ,hii Sheria iliwekwa ili kupunguzia wanawake wagumba upweke .

Kwa upande wa wanaume kama hazai mke ANAPASWA kutafuta mimba na kuleta watoto ,ukuryani kitanda hakizai haramu mfano mume ameenda kutafuta akarudi akakuta MKE ana mimba au ana mtoto basi huyo mtoto ni Mali yake wanaamini watoto NI assets.


Ila ukifumwa unatembea na mke wa mtu hilo ni swala lingine tena lenye utata mkubwa.

NDOA YA WAKE WENGI .

Wanaume wa kikurya huwa wanaoa wake wengi kulingana na utajiri alionao hasa jamii za wafugaji .

Wake wanaenda kwa umri kwa hivyo MKE mkubwa anakuwa ni yule wa kwanza na anakuwa ni mkubwa kweli ,wanaweza kuwa wake labda 10 ...Hawa tisa woote watamuita mke mkubwa mama na anaefuata ni mama mdogo na kila mke atakuwa na kijumba chake.

Wakurya wanawake hawafundwi zaidi ya kutahiriwa tu na kufundishwa ukakamavu , na mkurya huwa akiolewa anakuwa amehama ukoo hivyo hawezi rudi kwao kwa sababu yoyote na hata akiachika bado ataishi hapo atajengewa kibanda nje ya boma.

KAZI ZA MKE MKUBWA: Kuwafunda wake wadogo kila mmoja anaekuja pale atakaa kwa mama (mke mkubwa) kabla ya kuanza kuhudumia mume ,atakaa kwa muda akifundishwa mume anapenda nini (chakula na Mambo mengine ya kitandani) .

Atafundishwa kutokuwa na wivu na kuheshimu wake wengine walimtangulia.

MKE mkubwa pia ana kazi ya kuwalea wake woote watakaojifungua kuwakanda maji na kuwaangalia watoto wao mpaka watakapo maliza uzazi .

..
MKE mkubwa anakuwa ni kiongozi ,mama wa mji ,wajukuu wote wanakaa kwake ,vikao vyote vinafanyika kwake na ikiwa Hawa wengine watagombana yeye ndio hakimu .

Mke mkubwa akiamka asubuhi anagawanya kazi Nani ataenda kuchunga ,kukamua na kuchekecha mazima au Nani atapika chakula na ni chakula gani ...

Ukuryani ukewenza it's all about discipline hakuna kugombana ,mnaheshimiana kulingana na mlivyokuja .

Ikiwa mke ana umwa au Yuko period na NI zamu yake kulala na mume basi atajiwahisha kwa mama kutoa taarifa mapema ili mama achague mke wa kulala na mume kwa siku hiyooo...Sasa huu ukewenza huku mjini mi mwenyewe ulishaga nishinda .

Ameandika Ghaty Matiko
Amependa kushea andiko hili kupitia ukurasa huu.
Mwenye maswali mtauliza atakuwepo kujibu.

Ghaty ahsante kwa shule 🙏🥂
[6/7, 3:25 PM] Mwiza: 𝐇𝐎𝐖 𝐓𝐎 𝐌𝐀𝐊𝐄 𝐘𝐎𝐔𝐑 𝐇𝐔𝐒𝐁𝐀𝐍𝐃 𝐇𝐀𝐏𝐏𝐘:

1. Feed him
2. Sleep with him
3. Leave him in peace
4. Don't check his phone (Msgs)
5. Don't bother him with his movements
6. Clean the house
7. Wash his clothes
8. Always pray for him.

So what's so hard about that?

𝐇𝐎𝐖 𝐓𝐎 𝐌𝐀𝐊𝐄 𝐘𝐎𝐔𝐑 𝐖𝐈𝐅𝐄 𝐇𝐀𝐏𝐏𝐘:

It's really not too difficult but... To make a wife happy, a husband only needs to be:

1. a friend
2. a companion
3. a lover
4. a brother
5. a father
6. a master
7. a chef
8. an electrician
9. a plumber
10. a mechanic
11. a carpenter
12. a decorator
13. a stylist
14. a sexologist
15. a gynecologist
16. a psychologist
17. a pest exterminator
18. a psychiatrist
19. a healer/prayer
20. a good listener
21. an organizer
22. a good father
23. very clean
24. sympathetic
25. athletic
26. warm
27. attentive
28. gallant
29. intelligent
30. funny
31. creative
32. tender
33. strong
34. understanding
35. tolerant
36. prudent
37. ambitious
38. capable
39. courageous
40. determined
41. true
42. dependable
43. passionate

𝐖𝐈𝐓𝐇𝐎𝐔𝐓 𝐅𝐎𝐑𝐆𝐄𝐓𝐓𝐈𝐍𝐆 𝐓𝐎:

44. give her compliments regularly
45. go shopping with her
46. be honest
47. not stress her out
48. not look at other girls

𝐀𝐍𝐃 𝐀𝐓 𝐓𝐇𝐄 𝐒𝐀𝐌𝐄 𝐓𝐈𝐌𝐄, 𝐘𝐎𝐔 𝐌𝐔𝐒𝐓 𝐀𝐋𝐒𝐎:

49. give her lots of attention
50. give her lots of time, especially time for herself
51. give her lots of space, allow to visit her family members and your relatives.

𝐁𝐔𝐓 𝐌𝐎𝐒𝐓 𝐎𝐅 𝐀𝐋𝐋 𝐈𝐓 𝐈𝐒 𝐕𝐄𝐑𝐘 𝐈𝐌𝐏𝐎𝐑𝐓𝐀𝐍𝐓:

52. To learn not to ask for change when u give money for shopping. Whatever u give out becomes rightly hers no matter how big the note is.
.........
𝐓𝐎 𝐌𝐀𝐊𝐄 𝐀 𝐖𝐎𝐌𝐀𝐍 𝐇𝐀𝐏𝐏𝐘 𝐈𝐒 𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐈𝐎𝐔𝐒 𝐁𝐔𝐒𝐈𝐍𝐄𝐒𝐒 😄😀😃😜🌹 Send this to everyone on your list. Make a happy home. Wishing you all a 𝐇𝐀𝐏𝐏𝐘 𝐅𝐀𝐌𝐈𝐋𝐘.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom