vposterior
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 732
- 1,231
Wadau leo nilienda kuswali basi tayari nimejipanga katika safu kusubiri imamu atuongoze kuswali mara kaingia jamaa akasimama pembeni yangu na yeye amekuja kufanya ibada. Lahaula jamaa ananuka harufu mbaya sana ya sigara yaani hadi kero, kwa kweli ilibidi nikatishe ibada na nikachomoka kwenye ile safu nikajiunga upande wa pili.
Sasa nimejiuliza sana mbaba huyu ana mke na wanalala kitanda kimoja hali inakuwaje kwa huyo mama na wengine wanakuwa walevi pia basi ni vundo juu ya vundo.
Duuh poleni sana wanawake ambao sio walevi wala wavutaji lakini mmeolewa au mnaishi na hao watu.