Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,826
"HAKI SAWA" ni msemo au wazo lililoletwa na wanaharakati wa haki za wanawake hapa ulimwenguni ili kutengeneza msingi wa mfumo mpya ambao unalenga kumtetea mwanamke kutokana na aina tofauti za maonezi yanayompata katika jamii inayomzunguka.
Kimsingi .... lengo la kusema usawa wa haki baina ya mwanamke na mwanaume ulikuwa na nia nzuri ya kuwaamsha wanawake kukumbuka na kusimamia haki zao za kimsingi kama binadamu na sio kupimana ubabe na mabavu na jinsia ya kiume. Kwa hali ilivyo sasa ni tofauti na malengo yaliyotarajiwa........ kampeni ya haki sawa ambayo ililenga kumtetea mwanamke kutoka katika uonevu wa mfumo dume wa miaka na vizazi kadhaa vilivyotangulia......imegeuka kuwa ulevi na sumu kali kwa wanawake wachache ambao tayari wameshaanza kuona madhara ya kujioverdose na hii kampeni bila kufuata vipimo.
Kampeni ya haki sawa imeweka hisia mbaya za kibaguzi,ki-extremist na ki-radical ndani ya fikira,mawazo na akili za baadhi ya jinsia ya kike dhidi ya jinsia ya kiume.
Haya ndiyo yalikuwa malengo na nia ya kampeni ya HAKI SAWA kwa wanawake.
1.Kumtoa mwanamke katika fikra na mawazo kuwa yeye si kiumbe chenye thamani kama mwanaume na kumjenga kujitambua kuwa yeye ni binadamu na anazo haki za kimsingi juu ya maisha yake.
2.Kumtoa katika aina tofauti za uonevu kama kufanya kazi kama mtumwa ama punda bila ridhaa yake,kupewa adhabu au kudhalilishwa na jinsia yake au ya kiume aidha kwa kupigwa au kutukanwa pasipo uzito wowote wa kosa,kunyang'anywa stahili zake,kulazimishwa kuingia kwenye mahusiano n.k.
3.Kumpa sauti ndani ya jamii ili na yeye aweze kutoa mawazo au busara zake ndani ya jamii husika kwa maana na yeye ni binadamu kama mwanaume na ana uwezo wa kufikiri,kuchambua,kutafakari na kutatua migogoro yeyote ambayo ipo ndani ya uwezo wake.
4.Kutambua na kutimiza majukumu yake ya asili ya kimahusiano, kifamilia nakijamii pia.Anayohaki ya kusimamia utekelezaji wa hayo majukumu bila kikwazo chochote au kuingiliwa na jinsia yake au tofauti.Mfano wa jukumu na wajibu wa asili kwa mwanamke ni kupanga uzazi na ulezi wa watoto na familia kwa ujumla, jukumu na wajibu wa kupanga lishe ya familia etc.
5.Haki ya kumzuia mwanaume kufanya vitendo vya kuharibu uhusiano wake na famalia.Mfno....mwanamke anayoruhusa na haki ya asili ya kumzuia na kumkemea mwanaume asithubutu kuanzisha uhusiano na mwanamke mwingine.
6.Mwanamke anahaki ya kushea na kutumia vitu au mali za mpenzi wake bila kuzifuja au kuzitapanya kwa maendeleo ya wote.
7.Mwanamke anayohaki ya kufanya shughuli au kazi yeyote ambayo itamuingizia kipato kitakachomsaidia kuiendeleza familia yake bila kuathiri mahusiano yake na mwanaume au kuteteresha familia au uhusianowake.
8.Mwanamke anayo haki ya kujiongezea ufahamu kwa kujipatia elimu iwe ya afya,kiuchumi,biashara...n.k. ili impe nafasi kama binadamu wengine kuweza kutatua changamoto zinazoweza kumkabili.
Na list inaendelea...kutokana na muda nimezitaja hizo chache ila zipo nyingi zaidi ya elfu hivi.
Sasa balaa linakuja ni jinsi wanawake hususani wa kiafrika kugeuza hii harakati kuwa vita dhidi ya mwanaume badala ya chombo cha ukombozi.
Mabalaa yenyewe yapo kwenye sura zifuatazo;
1.Wanawake wengi wanaona kukaa au kuishi na mwanaume ni kero au ni mzigo heri kuwabadili kama nguo pale inapobidi.
2.Asilimia kubwa ya wanawake wa sasa especialy wa mjini wanafanya maamuzi yao kwa hisia za kimapokeo...mfano ni mwanamke anaweza kuanza kumdharau mwanaume wake bila sababu ya msingi kisa tu amepata hamasa ya kuwa wanaume ni wakorofi na dawa yao ni dharau.
3.Tabia ya wanawake kuhisi ni sahihi kuishi bila mwanaume maisha kumepelekea single mothers kuongezeka na kuathiri makuzi ya kiakili ya watoto,ambayo matokeo yake ni watoto ukubwani huanza tabia kama...ushoga na usagaji,unyanyasaji,wavulana kushindwa kufanya maamuzi mazito,kutokujali,utoaji mimba ,umalaya n.k.
4.Kuporomoka kwa maadili kwenye jamii na taifa kwa ujumla kutokana na usimamizi m'bovu wa makuzi ya watoto...coz mwanamke au mwanaume hakuumbwa kumlea mtoto pekee yake.
5.Msongo wa mawazo, stroke,vichaa,vifo vya mapema.
6.Influence mbaya kwa wanawake wengine walio na maadili mazuri kwasababu wanawake ni ngumu sana kuvumilia kuwa kwenye upweke pekee yao...hivyo kujiridhisha na kujifariji ni pale anapoona wenzake nao pia wasiwe katika amani kama yeye ili apate amani kwa kuwashawishi wenzake kuharibu ndoa zao au kutokuheshimu mahusiano yao na kushiriki vitendo visivyo na tija kwenye maisha.
7.Ulevi
8.Dharau,majivuno,kutokujielewa.
9.Kutokufahamu majukumu halisi ya jinsia ya kike....kwa mfano kulea mtoto,kutunza familia,kumshauri na kumtunza mwanaume,kulinda familia isisambaratike.
Tabia hizi pamoja na nyinginezo nyingi ambazo zimetokana na mapokezi mabaya ya HAKI SAWA.....zimepelekea wanaume wengi kuwaona wanawake kama chombo cha starehe na kutowathamini katika kuanzisha familia.Kwa mwanamke anayezijua haki zake na kutimiza wajibu wake bila kuvuka mipaka haya maswahibu yanayowaliza wanawake wengi ni nadra sana kumkuta.
Naomba kuwasilisha nakaribisha michango yote.Akina dada naombeni mchangie bila kuvuta hisia za kijinsia tumieni utashi wa kufikiri kwa kina na kwa usawa.Kama imekuuma hapa ndio mahala pa kujifunza.....kama haijakuuma naomba uwasaidie wanawake wenzako kujitambua tuijenge jamii yetu ya kitanzania iwe mfano wa kuigwa.