Wanawake: Mnapokosea kudhani mnawaelewa wanaume………!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
couple_arguing.jpg

Picha haihusiani na habari hii..........

Kuna wakati mmeshawahi kusikia watu wakilalamika kwamba mume fulani amemuacha mkewe ambaye ana tabia nzuri, mcheshi, mvumilivu, mwaminifu na mweledi (anayeelewa mambo). Ukweli ni kwamba hizo ni tabia nzuri na zinachangia sana kwenye kuimarisha ndoa, lakini bado hazina maana sana kama mke hataweza kujua namna nzuri ya kuonyesha upendo wake kwa mume.

Kuna makosa ambayo hufanywa na wanawake katika juhudi yao ya kuonyesha upendo kwa waume zao bila wenyewe kujua kwamba wanafanya makosa. Ngoja niyadadavue makosa ambayo wanawake wengi huyafanya wakijua wanawaelewa waume zao:

1. Kwa mfano, mwanaume hajipendi, mwanamke anapojaribu kuikemea tabia hiyo anakuwa anajenga ukuta mkubwa sana kati yao bila yeye kujua. Inashauriwa, badala ya kumwambia moja kwa moja mumewe kwamba aache kutojipenda, inashauriwa ni vyema akamnunulia mumewe nguo na akizivaa amsifie sana kiasi kwamba mwanaume huyo atajiona kuwa kumbe akivaa nguo za kiwango au mtindo fulani anakuwa katika hali ya kuvutia kupita kiasi. Hapo mwanaume naye atajaribu kununua aina hiyo ya nguo. Kwa wanawake ambao waume zao wana tabia ya kutojipenda kimavazi wanaweza kujaribu hata leo ili wapime matokeo ya ujanja huu.

2. Wanawake wanafanya makosa pale wanaposhindwa kushukuru juu ya yale mazuri wanayotendewa na waume zao na badala yake kulalamika kwa yale ambayo hawakutendewa. Utakuta mwanaume anajaribu kufanya hiki na kile kwa sababu ya upendo alio nao kwa mkewe, lakini mwanamke huyo hata mara moja hashukuru au kuonyesha kwamba anathamini juhudi hizo za mumewe. Lakini pale mwanume anaposhindwa kumfanyia hiki au kile iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi mwanamke hukata kama wembe kwa kauli zake za kulaani na kulalamika. Ni lazima wanawake wafahamu kwamba kwa maumbile wanaume hupenda sana kuonekana kuwa wamefanya mazuri au ni mashujaa kwa wake zao.

3. Kuna wanawake hawajui ‘asante’ kwa waume zao hawajui kuonyesha kwamba walichofanyiwa hata kama ni kidogo wamefurahi na kukikubali. Wanawake hawa kwa bahati mbaya wakati huo huo huwa hawajui kuacha kulaumu pale wanapoona hawakufanyiwa yale waliyotarajia kufanyiwa na waume zao. Mwanamke anapaswa ajifunze kusema ‘asante’ na kuonyesha kwamba ameridhika na alichotendewa na mumewe. Ajifunze pia kuacha kulalamika sana pale ambapo hakutendewa alichopaswa kutendewa.

4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo.

5. Wanawake huwa wanakosea sana pale wanapoeleza kukerwa hisia zao kwa kuuliza maswali ambayo hayana majibu, maswali ya kupita, ambayo siyo ya moja kwa moja kuhusiana na maudhi….. “unawezaje kufanya hivyo!” Ni vizuri mwanamke akaelezea kilichomkera moja kwa moja kuliko kutumia njia ya kuzunguka ya maswali yasiyo na majibu. “Sijui ndiyo nikueleweje?” Ni miongoni mwa maswali haya yasiyompendeza mwanaume.
 
1. Kwa mfano, mwanaume hajipendi, mwanamke anapojaribu kuikemea tabia hiyo anakuwa anajenga ukuta mkubwa sana kati yao bila yeye kujua. Inashauriwa, badala ya kumwambia moja kwa moja mumewe kwamba aache kutojipenda, inashauriwa ni vyema akamnunulia mumewe nguo na akizivaa amsifie sana kiasi kwamba mwanaume huyo atajiona kuwa kumbe akivaa nguo za kiwango au mtindo fulani anakuwa katika hali ya kuvutia kupita kiasi. Hapo mwanaume naye atajaribu kununua aina hiyo ya nguo. Kwa wanawake ambao waume zao wana tabia ya kutojipenda kimavazi wanaweza kujaribu hata leo ili wapime matokeo ya ujanja huu.

Nilijaribu hii lakini iligonga ukuta vibaya sana,iliishia mimi ndio niwe namnunulia nguo kila kukicha!!!!!

2. Wanawake wanafanya makosa pale wanaposhindwa kushukuru juu ya yale mazuri wanayotendewa na waume zao na badala yake kulalamika kwa yale ambayo hawakutendewa. Utakuta mwanaume anajaribu kufanya hiki na kile kwa sababu ya upendo alio nao kwa mkewe, lakini mwanamke huyo hata mara moja hashukuru au kuonyesha kwamba anathamini juhudi hizo za mumewe. Lakini pale mwanume anaposhindwa kumfanyia hiki au kile iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi mwanamke hukata kama wembe kwa kauli zake za kulaani na kulalamika. Ni lazima wanawake wafahamu kwamba kwa maumbile wanaume hupenda sana kuonekana kuwa wamefanya mazuri au ni mashujaa kwa wake zao.

3. Kuna wanawake hawajui ‘asante' kwa waume zao hawajui kuonyesha kwamba walichofanyiwa hata kama ni kidogo wamefurahi na kukikubali. Wanawake hawa kwa bahati mbaya wakati huo huo huwa hawajui kuacha kulaumu pale wanapoona hawakufanyiwa yale waliyotarajia kufanyiwa na waume zao. Mwanamke anapaswa ajifunze kusema ‘asante' na kuonyesha kwamba ameridhika na alichotendewa na mumewe. Ajifunze pia kuacha kulalamika sana pale ambapo hakutendewa alichopaswa kutendewa.

Kweli hili ni kosa,pale unapofanyiwa kitu kizuri inabidi kushukuru hata kama ni kidogo lakini amejaribu. Hakuna kitu kizuri kama kuonyesha kuwa umefurahia mume alichojaribu kukufanyia inasaidia kumpa moyo ili afanye zaidi na baadae kujenga mazoea ya kufanya hivyo vitu. Nakiri kuwa nimesikia wanaume wengi wakilalamika kuhusu hili kwamba pale wanapochelea kufanya kile mke alichotarajia maneno anayoyapata ni makali sana,na atahesabiwa na yale yote ya nyuma ambayo hakufanya kwa bahati mbaya. Kwa hapa wanawake inabidi tujifunze,hizi lawama ni nyingi sana.

4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo.

Kiukweli mimi sitakuficha nitakwambia tu kwa vizuri with a romantic tone, mpenzi wangu naomba ukiwa unaoga uweke pazia vizuri basi ili maji yasimwagike nje unaweza kuteleza ukitoga bafuni. Ila Mtambuzi wanaume mmekua mkipokea vibaya sana pale mnapoambiwa ukweli na huwa mnatoa majibu yakukatisha tamaa kabisa. Naomba nikupe mfano hai.....mume amerudi kutoka kazini amefika sebuleni anavua socks anaacha hapo chini anaenda chumbani anavua suruali anaweka chini(na tenga la nguo liko hapo chumbani analijua,analitambua na kuliona) akiingia kuoga anavua c.h.upi anaweka chini. Kweli kaka yangu huyu mtu utaacha kumwambia???!!!! baada ya kumwambia kwa wema kabisa atafanya siku mbili tatu.....mara ataendelea tena vile vile. Sasa hapo mke atakua amekosea nini???!!!!

5.
Wanawake huwa wanakosea sana pale wanapoeleza kukerwa hisia zao kwa kuuliza maswali ambayo hayana majibu, maswali ya kupita, ambayo siyo ya moja kwa moja kuhusiana na maudhi….. "unawezaje kufanya hivyo!" Ni vizuri mwanamke akaelezea kilichomkera moja kwa moja kuliko kutumia njia ya kuzunguka ya maswali yasiyo na majibu. "Sijui ndiyo nikueleweje?" Ni miongoni mwa maswali haya yasiyompendeza mwanaume.

Hiyo unawezaje kufanya hivyo au sijui nikueleweje lazma itakua imekuja after a very long discussion haiwezekani tu from nowhere mke aanze kusema unawezaje kufanya hivyo?.

Duuuh ila Mtambuzi naona umetuamulia sana wanawake safari hii......sijui yuko wapi mzee Bishanga aje kutusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Nilijaribu hii lakini iligonga ukuta vibaya sana,iliishia mimi ndio niwe namnunulia nguo kila kukicha!!!!!

Kweli hili ni kosa,pale unapofanyiwa kitu kizuri inabidi kushukuru hata kama ni kidogo lakini amejaribu. Hakuna kitu kizuri kama kuonyesha kuwa umefurahia mume alichojaribu kukufanyia inasaidia kumpa moyo ili afanye zaidi na baadae kujenga mazoea ya kufanya hivyo vitu. Nakiri kuwa nimesikia wanaume wengi wakilalamika kuhusu hili kwamba pale wanapochelea kufanya kile mke alichotarajia maneno anayoyapata ni makali sana,na atahesabiwa na yale yote ya nyuma ambayo hakufanya kwa bahati mbaya. Kwa hapa wanawake inabidi tujifunze,hizi lawama ni nyingi sana.

Kiukweli mimi sitakuficha nitakwambia tu kwa vizuri with a romantic tone, mpenzi wangu naomba ukiwa unaoga uweke pazia vizuri basi ili maji yasimwagike nje unaweza kuteleza ukitoga bafuni. Ila Mtambuzi wanaume mmekua mkipokea vibaya sana pale mnapoambiwa ukweli na huwa mnatoa majibu yakukatisha tamaa kabisa. Naomba nikupe mfano hai.....mume amerudi kutoka kazini amefika sebuleni anavua socks anaacha hapo chini anaenda chumbani anavua suruali anaweka chini(na tenga la nguo liko hapo chumbani analijua,analitambua na kuliona) akiingia kuoga anavua c.h.upi anaweka chini. Kweli kaka yangu huyu mtu utaacha kumwambia???!!!! baada ya kumwambia kwa wema kabisa atafanya siku mbili tatu.....mara ataendelea tena vile vile. Sasa hapo mke atakua amekosea nini???!!!!

5.

Hiyo unawezaje kufanya hivyo au sijui nikueleweje lazma itakua imekuja after a very long discussion haiwezekani tu from nowhere mke aanze kusema unawezaje kufanya hivyo?.

Duuuh ila Mtambuzi naona umetuamulia sana wanawake safari hii......sijui yuko wapi mzee Bishanga aje kutusaidia.
Yummy uko sahihi, lakini kumbuka kwamba nilichoeleza sio mkwamba ni formula ambayo mnapaswa nkuifata kama ilivyo, nilichofanya ni kuandika mfano wa namna unavyoweza kucheza na maneno na vitendo kulingana na namna unavyomjua mumeo.............

Kuhusu kuwaamulia wanawake, naomba uniwie radhi, lakini ninayoyaandika ni miongoni mwa malalamiko ya wanaume dhidi ya wake zao, na lengo langu ni kwasaidia wanawake wajue ni kitu gani waume zao wanataka?
lakini pia sijamlenga mtu, yule anayeona anayafanya hayo na kumridhisha mumewe, haimhusu, lakini yule mwenye udhaifu huo, basi ujumbe umfikie.........................................
 
Teh teh teh sawa mkuu nimekuelewa vyema na asante kwa kutusaidia kuwatambua jinsia yako......doh bora yani umefafanua, mie hainihusu kabisaaaaa :clap2:
 
Kitu ambacho nimegundua kwa wanaume wengi hawapendi kukosolewa/kuelekezwa wanapokosea! Baadhi ya wanaume wanataka wanachofanya wao hata kama ni madudu basi kipite bila kupingwa! Ukimwelekeza hata kwa upole na mapenzi mazito yeye ataishia kua mkali au kukutyson kabisa! Am not married but hua naiona sana hii kitu kwa wanandoa walionizunguka!
 
Nitamwambie wife asome hiii........ ki ukweli wanachukulia ni jukumu la mwanaume kufanya vitu fulan kweny family ni sawa lakin nipongeza basi kwa kutimiza majukum yangu, mfn unamnunulia nguo wife wako unafikanayo home unaambiwa hee hee hii ndio rangi gan mbona sio nzuri ungeleta ya kijani ndio bomba hata asante haipo ki ukweli wanawake wengne wanawavunja moyo wanaume kutimiza majukumu yao kwa kukosa neno asante tuuu
 
6. Kumfanya mumeo hajui kitu. Yaani kila utakaloambiwa nje utakuwa tayari kuliamni lakini analokwambia mumeo hutaki kuliamini na hivyo kutomshirikisha katika kupata ushauri. Pengine hii huletwa na dharau kuwa umeshamzowea.
 
Kitu ambacho nimegundua kwa wanaume wengi hawapendi kukosolewa/kuelekezwa wanapokosea! Baadhi ya wanaume wanataka wanachofanya wao hata kama ni madudu basi kipite bila kupingwa! Ukimwelekeza hata kwa upole na mapenzi mazito yeye ataishia kua mkali au kukutyson kabisa! Am not married but hua naiona sana hii kitu kwa wanandoa walionizunguka!
Aproaching dada yangu ndiyo inayowaponza, inawezekana mwanamke akamwambia mwanaume kwa upole na mapenzi, lakini kama ameanza na kumkosoa kifedhuli hiyo haisaidii kabisa......

Kwa mfano:

1. Kwa mfano, mwanaume hajipendi, mwanamke anapojaribu kuikemea tabia hiyo anakuwa anajenga ukuta mkubwa sana kati yao bila yeye kujua. Inashauriwa, badala ya kumwambia moja kwa moja mumewe kwamba aache kutojipenda, inashauriwa ni vyema akamnunulia mumewe nguo na akizivaa amsifie sana kiasi kwamba mwanaume huyo atajiona kuwa kumbe akivaa nguo za kiwango au mtindo fulani anakuwa katika hali ya kuvutia kupita kiasi. Hapo mwanaume naye atajaribu kununua aina hiyo ya nguo. Kwa wanawake ambao waume zao wana tabia ya kutojipenda kimavazi wanaweza kujaribu hata leo ili wapime matokeo ya ujanja huu.

Mbinu hiyo hapo kwenye bold inatumiwa sana na wanawake wanaoitwa nyumba ndogo na ndio maana huwakamata waume za watu na wala sio LIMBWATA kama mnavyodhani, kubishana kwamba wanaume ni wababe na ni wakorofi, haisaidii bali kauli njema ndio njia pekee itakayokuwezesha kufurahia mahusiano yenu kama wanandoa.........
Kama hamko tayari kukubali ukweli huu basi ni bora msiolewe, tafuteni wanaume wa kuzaa nao kisha kila mtu ashike hamsini zake, kwani maumbile hayajui kuoa wala kuolewa, bali yanajua kuzaa basi, kwani hata Mungu alisema "muende mkazaane muijaze dunia" na hakusema muende mkaoane...................
 
[h=2]Ndoa[/h]Je! Bibilia ya funza nini kuhusu ndoa?. Imeandikwa, Mathayo 19:5-6 "Asema kwasabu hiyo mtu atamwacha babye na mamaye ataambatana na mkewe na hao wawili watakua mwili mmoja? hata wamekua si wawili tena bali mwili mmoja basi aliowaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe."

Je! waume wawatendeaje wake zao?. Imeandikwa, Waefeso 5:25-28 "Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wal kunyazi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume na kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe mewenyewe."

Waume wa waheshimu wake zao. Imeandikwa, 1Petro 3:7 "Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili na kupa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu, na kama waridhi pamoja wa neema ya uzima kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe."

Je wake nao wake na waume zao vipi?. Imeandikwa, Waefeso 5:22-24 "Enyi wake watiini waume zenu kama kutii Bwana wetu kwa maana mume ni kishwa cha mkewe kama Kristo naye nikichwa cha kanisa, naye nimwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo."

Je inamaanisha ya kuwa wake wafanye kila jambo? Asha!. Imeandikwa, Waefeso 5:21 "Hali mnanyenyekea katika kicho cha Kristo."

Je tumeagizwa kutoa kupigana kwa mke na mme. Imeandikwa, Wakolosai 3:19 "Ninyi waume, wapendeni waume zenu, msiwe na uchungu nao."

Kuwa na ndoa njema nivema kutatua mafaragano au kutoelewana mara moja. Imeandikwa, Waefeso 4:26 "Mwea na hasira ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka."
Fanya ndao yako ikuwe kwa umoja na kuelewana. Imeandikwa, Waefeso 4:2-3 "Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo na kujitahidi kuuhifadhi umoja kwa Roho katika kifungo cha amani."

Je! watu wapaswa kuiona vipi ndoa. Imeandikwa, Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi kwa maana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu."
Kwa amri gani Mungu ameilinda ndoa. Imeandikwa, Kutoka 20:14, 17 "Usizini". Usitamani nyumba ya jirani yako usitamani nyumba ya jirani yako..."

Je Mungu ameamua kuvunja ndoa katika hali gani? Imeandikwa, Mathayo 5:32 "Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe isipokua kwa habari ya uasherati amefanya kuwa mzinzi, na mtu akimwoa yule aliyeachwa azini."

Je ndoa ikae kwa mda gani. Imeandkwa, Warumi 7:2 "Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokua hai, bali akifa yule mume amefunguliwa ilesheria ya mume."

Je tumeagizwa kumuoa nani? Imeandikwa 2Wakorintho 6:14 "Msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana kuna urafiki gani kati ya haki na uasi? tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?."

Malazi yamebarikiwa na Mungu wakatika ndoa. Imeandikwa, Mithali 5:18-19 "Chemchemi yako ibarikiwe nawe umfurahiye mke waujana wako ni alaya apendaye na paa apendezaye."

Ameni !!!!.........

"4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo."

Men! men..tukinyamaza kimya ni shida,tukisema ni tabu..and yes stop acting like a child and you will not be treated like one. :ranger:
 
Duuuh ila Mtambuzi naona umetuamulia sana wanawake safari hii......sijui yuko wapi mzee Bishanga aje kutusaidia.

..........hii ni namba mbaya madam Yummy na ukisikia Babu Mtambuzi ndo huyu, mwingine ni nakala tu! AshaDi mwenyewe alishaweka silaha chini, unadhani mchezo. We jiulize mtu kichwa kizima kimejaa mvi hadi leo ukienda kwake unakutana na wajukuu tu, hakuna cha Bibi wala kumsikia walau anakwambia labda Bibi yako kaenda sokoni! Kina Bibi wote walishakimbiaga zamani!
 
yule anayeona anayafanya hayo na kumridhisha mumewe, haimhusu, lakini yule mwenye udhaifu huo, basi ujumbe umfikie....................... .................. mkuu babu Mtambuzi, najitahidi kadiri niwezavyo! hakuna aliyekamilika, nina mapungufu yangu, ana ya kwake! tunarekebishana na kusonga mbele! niliolewa mdogo sana at the age of 20, at 21 tayari nna mtoto na tupo imara kama nondo za dirisha! so wale waja jamani UVUMILIVU NI MSINGI IMARA WA NDOA YOYOTE ILE!
 
Last edited by a moderator:
..........................tafuteni wanaume wa kuzaa nao kisha kila mtu ashike hamsini zake, kwani maumbile hayajui kuoa wala kuolewa, bali yanajua kuzaa basi, kwani hata Mungu alisema "muende mkazaane muijaze dunia" na hakusema muende mkaoane...................

Mhhhhhhhhhh! Babuuuuuuuuuuuuu! Naona siku hizi unafunguka jumla jumla mweeeeee! Hapo kwenye red, sijui niseme ni busara, hasira au ndo gari limeshika kasi likafungua na turbo kabisa!
 
"4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo."

Men! men..tukinyamaza kimya ni shida,tukisema ni tabu..and yes stop acting like a child and you will not be treated like one. :ranger:
Sashel hilo la kudeka kama watoto hawawezi acha, mi kuna kipindi nilikuwa najiuliza hivi ni makusudi au ni kweli?? nimegive birth to twins, nipo busy na watoto, yaani huwezi amini, ananuna na kulalamika kuwa simjali tena, nimemtelekeza, na mambo kama hayo, so ilibidi nijitahidi akiwepo watoto kwa dada zao, wananyweshana maziwa huko na kubembelezana, mpaka labda husby alale au atoke! ndio nitaendelea na wao!
 
Last edited by a moderator:
afu ndo ukurupuke kumwambia mtu 'hujanifikisha'
nyie acheni kutudanganya eti 'muwe mnasema'

kama tu kuvaa ukikosolewa napo ishu?
 
he ! jamani yaan sisi wanawake tu , ,mbona watu wanajitahid kwa waume zao ila ngumi hugonga ukuta ,japo kuwa kuongea na mwandani kiustaarabu ni vizur ,na sio mwanandani tu mm nahis mtu yoyote yule ukitumia kauli kali inakuwa sio ustaarabu ,sawa kaka massage imefika
 
Naomba nikupe mfano hai.....mume amerudi kutoka kazini amefika sebuleni anavua socks anaacha hapo chini anaenda chumbani anavua suruali anaweka chini(na tenga la nguo liko hapo chumbani analijua,analitambua na kuliona) akiingia kuoga anavua c.h.upi anaweka chini

kama kweli kuna mwanaume anafanya hivyo basi atakuwa ni bonge la kimeo... suruali na chu'pi zinawekwa chini ili iweje sasa?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom