Ni kero ambayo iko kwa asilimia kubwa kwa wanawake wenye wapenzi/wachumba/waume ambapo mwanamke anaomba umtumie vocha kwenye simu lakini ukishamtumia akiwa na tatizo saa hiyo hiyo anakubip ili wewe(mwanaume) umpigie. Sasa haieleweki hizo vocha anazoomba atumiwe kwenye simu yake anatumia kuwasiliana na nani. Hebu akina dada tuambieni ni kwa nini inakuwa hivi maana ni vijimambo vidogo lakini vinakera kweli kweli.