Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Wanauchumi wawili David Anderson na Shigeyuki Hamori wanasema kwamba wale wanawake ambao wanapotongozwa kwa mara ya kwanza huwa wagumu hata kama wanapenda, huwa wanaonekana kuwa na thamani kwa wanaume wanaowafuata ukilinganisha na wale ambao huwa hawana kujivuta –vuta kwa aina fulani. Wanauchumi hawa hata hivyo huenda hawajui kwamba jambo hilo lilikuwa linafanyika kwa miaka mingi huku Afrika. Kwa mila za Kiafrika mwanamke hatakiwi kumkubalia mwanaume kirahisi, hata kama anampenda. Hata katika mafunzo ya unyagoni wasichana huwa wanafundishwa kuwa ‘wagumu' wanapofuatwa na wanaume, bila kujali kama wanapenda au hawapendi. Hali hiyo ndiyo ambayo impelekea wanawake wa Kiafrika kushindwa kuwaambia kwanza wanaume kuwa wanawapenda, badala yake husubiri kwa maumivu hadi pale wanaume wanapowaambia.
Wataalamu hawa wanaunga mkono mila zetu za Kiafrika kwa kusema kwamba, iwe ni Ulaya, Asia au Afrika, mwanamke kukubali haraka ombi la mwanaume huwa kunashusha hadhi ya mwanamke huyo. Wanasema hii ni kwa sababu kwa asili watu huwa wanahisi kwamba, bidhaa ambazo ni adimu au zenye bei kubwa huwa ndizo zenye thamani zaidi. Hisia kama hizi haziishii kwenye bidhaa, bali huenda hata katika uhusiano. Kwa mfano unapokwenda dukani kutaka kununua bidhaa fulani ambayo huijui vizuri, kigezo kitakachokuongoza kwenye kujua ubora wake kinaweza kuwa bei. Ile ambayo itakuwa na bei kubwa, itakushawishi kwamba ndiyo imara zaidi. Kwenye suala la mwanamke kufuatwa na mwanaume, wataalamu hawa wanasema mwanaume huwa anaangalia kitu ambacho naweza kukiita, ‘kiwango cha uwanauke' wakati akimtaka mwanamke kwa mara ya kwanza.
Kama mnunuzi wa bidhaa anavyoongozwa na kiwango cha bei kukadiria ubora wa bidhaa, mwanaume naye huongozwa na ‘ugumu' wa mwanamke kutambua kwamba mwanamke huyo ana thamani au urahisi wake kutambua kama hana thamani. Hata hivyo inatahadharishwa kwamba mwanamke anapokataa kwa sababu tu ya kulinda thamani yake, lakini akiwa anapenda, awe na kiwango. Kukataa kwa namna fulani kunaweza kuwafukuza wanaume kabisa hadi mwanamke kudhani ana nuksi………….