Wanawake mkiendelea hivi hamtoingia peponi

Wanawake mkiendelea hivi hamtoingia peponi

Enzi izo katika zululazula zangu Facebook nikapataga Manzi anamkwanja balaa sababu alikuwa ananitoa toa vivocha na vijicent. Siku akasema nikamtembelee kwao about 120 Km ivi, nikamwambia hapa sina hata Mia, akatuma nauli ya kwendea ya kurudi akasema atanipa nikifika.

Ile Nimefika tukakutana sehem tukaenda Garden kanunua kahawa tukawa tunakunywa tunainjoi wenyewe.Ghafla akatoea kajamaa fulan kametupia kinoma kapo na Subaru Mara nashangaa Yule dem ananitambulisha Huyu ni Baby yangu Anaitwa Frankie.

Pia akamtambulisha jamaa yake kuwa mim ni Best wake wa Facebook.. Nilitamani nikiwashe ile nikakumbuka sina hata mia ya nauli kurudi home nategemea kwa manzi ikabidi niwe mpole tu na ka-fake smile kwa mbali. Basi tukawa tunapiga story tukaagiza msosi pale wa maana jamaa akalipia kila kitu.

Basi jamaa akawa ananisimulia jinsi alivyo kutana na yule manzi, walivyo anza ku deti na mbaka kufikia walipo fika nikawa nasikiliza yanaingilia kulia yanatokea kushoto..

Ikawa jion mida ya saa kumi na mbili ikabidi nianze kuaga kuwa nataka kuwahi Gari (Busi) ingawa lengo ilikuwa ni kulala ila ndio ivyo movie imeharibika.

Tukapanda Subaru ya jamaa wakawa wananisindikiza standi njiani wakaninunulia Mananasi na Maembe. Tulivyo fika standi Jamaa akanitoa na buku tano nauli tukabadirishana namba za simu kwa ajiri ya mawasiliano zaidi pia nika muadd facebook basi ndio ikawa ivyo Day wasted.

Bad news Mananasi na maembe niliyasahau kwenye basi nilivyo shuka sababu nilikuwa nimesha vulugwa.

Wadada muwe mnatumbia ukweli kuwa mna watu wenu uko tunako wafata..
Habari za Dar?[emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu wakaona isiwe taabu walau upate hata mananasi upoze uchungu..

Utakuwa ulienda ki-LOCAL sana... vile ile kibaharia kupewa mananasi na machungwa ni jambo la kufikirisha sana heheheheheheheh
 
Huyo msela sio jamaa yake na Demu.
Demu alimtumia kukuondoa/ kukurudisha home na kukupiga chini.
IPO namna Demu alifikiri uko- kimwonekano, kichwani au vyote Kwa pamoja, lakini mlipoonana Hali ikawa tofauti.
Ikabidi huyo aliyekununulia mananasi atumike kukuondoa.
Bila Shaka hii ilikuwa Challinze?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom