Wanawake kuweni makini jikoni

Nguva Jike

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
1,298
Reaction score
1,875
Natumai mmeamka salama Tanzania yote!
Nimegundua mchezo hatari unaoleta mkanyagano na kung'atana katika mahisiano.

Mwezi uliopita niligombana na shemeji yenu kiasi cha kunyofoana nguo kabisa.Sikupata jibu kwanini tuligombana kiasi kile kwakuwa huwa hatugombani kijinga jinga.

Jana asubuhi akaja mtoto wa kike kagonga getini nikamfungulia akasema ametumwa moto na mama yake eti kibiriti chao kimelowa.Nikamwambia ingia jikoni kachukue.

Alivyotoka tu kuchukua moto mume wangu akaja nje huku anawaka maji yako wapi nikaoge sijajibu karusha kofi Mara teke nikaanguka chini nilikuwa na kanga tu uchi ukaonekana house boy alishuhudia.

Nikajiuliza hii balaa gani siku ya pili.Nikaingia jikoni nakuta harufu isiyo ya kawaida kuchunguza naona kipande cha ngozi kinaungua jikoni.Nikakitoa nikakizima moyo ukatulia.

Nikaenda mpaka kwao yule mtoto aliyekuja kuchukua moto.Nikamuita akaja nikamuuliza wewe jikoni uliweka nini akakana.Nilivyo mbana akasema nilipewa na mama nikiweke kiungue baada ya kuchukua moto.

Nikapitia Kwa mganga wa jirani nikamuonesha ile ngozi akasema ngozi hiyo mbaya ni ya kufarakanisha nyumba nzima.Nilipo mwambia mume wangu hakuamini alivyo mfuata yule jirani polisi walikuja gombea ugomvi huo.Polisi walimhoji yule jirani akakiri kweli alimtuma.

Ndugu zangu kuweni makini sana jikoni na majumbani kwenu Kwa wageni wasio wema.
 
Du Pole sana sister , ila sidhani kama kulikua na ulazima wa kusema Uchi ulionekana na house boy , ingetosha tu kusema kwamba ulibaki mtupu, au nguo zilivuka , tafsida ina ladha yake katika kiswahili
 
Haha pole, si ungeziba uchi wako na mkono usionekane
 
Kawaida kwangu huwa sina mazoea ya kuazimana iwe chumvi au kiberiti. Kila mtu kivyake kwsbb licha ya kusababisha mambo km hayo pia ni vitu vinavyogombanisha sana majirani.
 
Pole sana.
Hayo mambo yapo sana.
Kumwomba Mungu nako kuhusike kwa kiasi kikubwa jamani ili aingilie kati baadhi ya mambo yetu.
 
Pole sana kama ni kweli. Ila kwa upande mwingine we pia unamatatizo sababu ulishawahi kuona wapi mtu anahitaji moto kisha we mwenye jiko lako huendi kumpa eti unamtuma aingie mpaka ndani achukue moto. [emoji15] [emoji15]

Walishajua madhaifu yako na ndio waliyoyatumia kufanya walichokifanya. Pia nadhani kama ni wa kujifunza umeshajifunza hapo.
 
Sawa ila uache ushirikina, mambo mengine yanaepukika tu ulipokuwa unamtuma huyo mtoto jikoni maana ni mzoefu na jiko lako usirudie tena mtegemee Mungu katika yote wala hayo ya house boy wako kuona uchi yasingekukuta Nina uhakika siku house boy akiusifia uchi wako namna alivyouona utamtunuku
 
Ila wana JF ipo shida inatuandama..
Mana kilicho letwa na kinacho jadiliwa ni vitu viwili tofaut kabisa.
Duu[emoji119] [emoji119] [emoji119]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…