Habari wanaJF
Hii itawasaidia sana wanawake ambao wapo tayari kwenye ndoa na mahusiano ya kawaida ambapo kuna mahala wanawake wanajisahau na kuwatamkia wanaume wao maneno yasiyo na hekima, kwa mfano utamsikia mwanamke anamwambia mwanaume wake kuwa ‘’Wanaume wenzako wanajenga, wewe kila siku ahadi tu" [emoji16][emoji16]. Kauli kama hii ni kosa na kasoro kubwa.
Ukiachilia mbali kwamba hiyo ni lawama, lakini kauli kama hiyo inajenga hisia kwa mwenzako kuwa mwanamke huyu kumbe anapenda kuwa na wanaume kama hao hivyo wanaume wengi hawapendi kushauriwa bila hekima na kudhani kuwa wanawake hao wanaodhani wanaume wao siyo wa maana hivyo mwanamke ukitumia maneno yasiyo na hekima huwezi kuwa sumaku kwa mwanamume wako bali mwibaa mchungu[emoji17]