Wanawake Hawajiamin kwa nin?

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,726
19,874
Utakuta mkeo kawaagiza mashosti na ndugu zake anatafuta binti wa kazi wa ndani wakiletwa zaidi ya mmoja anachagua asiye na mvuto kuliko wengine eti ili asije akamuibia mumewe.Yaan hawa viumbe hawajiamini kabisa hii nimeona kwa dada yangu alipoletewa wasaidiz zaidi ya watatu
 
Huwa natafakari ni siku gani mambo haya ya kutupiana mipira yataisha.Mara huyu mwanamke ndo wa hovyo mara huyu mwanaume ndo wa hovyo!
 
Aaah mkuu dada yako alikwambia hivyo? kuna wengine wanachagua wasio na mvuto kwa kuamini watachapa kazi kuliko warembo........
 
kila kazi ina type zake bwana.

Tuheshimu kazi zao, mbona kwenye muvi majambazi wana sura fulani za kazi yet sexy?

Kumbe imepitishwa kuwa mabeki tatu wengi wanapendeza kuwa mazombie
 
Mkuu imenenwa mwanamke mwerevu hujenga nyumba yake mwenyewe na mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake mwenyewe (nisamehe kama sijaweka vizuri kauli yenyewe) lakini kifupi ni kwamba mwanamke atakuwa ni mjinga akikubali kuwa na housegirl aliyemzidi uzuri, au aliyemzidi hekima au aliyemzidi busara-ni muhimu mama mwenye nyumba akawa mbele tena kwa mbali kwa kila kitu dhidi ya housegirl
 
naunga mkono hoja kwa asilimia 100%.
 
mhm wanaume sie bwana kusema kweli akili zetu twazijua wenyewe....unaweza ache mke wako mzuri kabisa uchi kitandani ukaenda kwa beki tatu....hivyo bora tuu wachukue atua za kupunguza matamanio yetu
 
Kwanini niweke mwanamke mzuri zaidi yangu as housemaid, ili iweje. Kumbuka housemaid huyo anaangalia nyumba, watoto, kupika, pakuwa na awe mzuri, mume wangu amtamani. Sasa mimi nina umuhimu gani ndani ya nyumba?

Mimi nikiweka housemaid, Im considering someone above 45yrs hata kama hatakuwa very efficient as long as can perform most of basic chores. Hawa wasichana headache.
 
Huu usemi wa mwanamke mwerevu sijui mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe nadhani unaapply na kwa wanaume pia! Kwani nyumba haijengwi na mwanamke peke yake.

Usemi huu mie nauchukuliaga kama ukandamizaji kwa wanawake! Yaani kumtaka awe mvumilivu tuuuu no matter what kisha asiivunje nyumba na kuitwa mpumbavu!!
 
Na kwa nini uichukulie negative billie? Huoni kama mkeo anakupenda sana na anamsaidia Mwenyezi Mungu kukuepusha na majaribu?

Ingawa siamini katika uzuri
 
Mie hgeli asiekuwa na mvuto simtaki! Tena sharti akiamka afanye usafi afu aoge ndo apike chai. Nikipishana nae anukie uturi. Kama mwenza wangu atamtamani shauri lake, his loss!

Hivi mnafikiri mwanaume kukutwa anatembea na hgeli ni aibu yake ama ya mkewe? I'd rather have an affair na boss wangu than mlinzi wa nyumbani kwangu. Zero grazing ni dalili ya uvivu wa kufikiri and that kind of a man nam_dispise!
 
Utakuta mkeo kawaagiza mashosti na ndugu zake anatafuta binti wa kazi wa ndani wakiletwa zaidi ya mmoja anachagua asiye na mvuto kuliko wengine eti ili asije akamuibia mumewe.Yaan hawa viumbe hawajiamini kabisa hii nimeona kwa dada yangu alipoletewa wasaidiz zaidi ya watatu

hapo kwenye red..... ukiona hivyo ujue shemeji yako kicheche.....
na siri ya ndoa wanaijua wanandoa wenyewe......
sidhani kama jambo hilo lina uhusiano na kutokujiamini...
ukizingatia unapochagua msichan wa kazi unaangalia vigezo vingi sana, kumbuka huyo ndo atashinda na watoto usipokuwepo, huyo ndiye atakayewapikia watoto nk nk
 
mmmmh ni wajibu wa mke kumlinda mume wake dhidi ya majaribu na vishawishi vyote vya ibilisi...mimi housegirl wangu kakaa kisemenya hivi...nipo single lakini sijui kwa nini napenda wenye mvuto ziro....mwenye mvuto sipendi...
 
Huu usemi wa mwanamke mwerevu sijui mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe nadhani unaapply na kwa wanaume pia! Kwani nyumba haijengwi na mwanamke peke yake.

Usemi huu mie nauchukuliaga kama ukandamizaji kwa wanawake! Yaani kumtaka awe mvumilivu tuuuu no matter what kisha asiivunje nyumba na kuitwa mpumbavu!!
@Mbu anaendeleaje?
 
Sasa kama mwanaume mwenyewe hamjengei mke wake confidence huyo mwanamke atajiamini vipi?inawezekana huyo shemeji yako ni gubegube lilishoshinda mitume sasa hapo dada ako atatoa wapi confidence ya kuajiri housegirl mzuri??
 
Back
Top Bottom