Wanawake acheni kuposti mitandaoni mnapokasirika, wife aliwahi kujuta

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,485
99,217
Ni story ya zaman kdg, inaweza kua funzo kwa KE na ME walio kwenye ndoa au mahusiano serious .

Ni hivi,
Ilkua ndo kipind kifupi tangu nmemuoa mke wangu kipenzi MAMAG A.k.a Mama wawili, na ndo katoka kajifungua salama tumepata Mtoto wetu wa kwanza.

Sasa kipindi icho kichanga chetu ndo kimefikisha miez 6 tu, usiku nmetoka safari Tuko kitandani namwonesha mke wangu picha za mizigo niliyopakia uko nilikotoka, Kuna limchepuko flani lipumbavu sn nilikutana nalo uko Safari basi likanitumia sms ya mapenz usiku ule ule,ile sms inaingia tu, nikajaribu kuiskip haraka kumbe wife nae kaiona.
 
Zikaanza sarakasi kitandani kuigombea ile simu, Aisee tukagombana Sana nikagoma katakata kumpatia ile simu, wife akanuna karibu siku 3 mfulurizo.

Nami nilipochoka kumbembeleza,nikampotezea, sasa alipoona simbembelezi tena, akampost jamaa fesibuku na kusindikizia ile picha na Maneno ya kimahaba yakionesha kwamba yule mwamba Ni mpenzi wake.

Sikuziona zile picha, nikaja kustuliwa na dada yangu akiniuliza Kama tumeachana na MKE wangu, nikamuuliza kwa Nini? Akasema Kuna mwanaume kampost fesibuku na kasindikizia Maneno ya kimahaba mno. Ikabd nami niingie fesibuku kujionea.
 
Zikaanza sarakasi kitandani kuigombea ile simu, Aisee tukagombana Sana nikagoma katakata kumpatia ile simu, wife akanuna karibu siku 3 mfulurizo.

Nami nilipochoka kumbembeleza,nikampotezea, sasa alipoona simbembelezi tena, akampost jamaa fesibuku na kusindikizia ile picha na Maneno ya kimahaba yakionesha kwamba yule mwamba Ni mpenzi wake.

Sikuziona zile picha, nikaja kustuliwa na dada yangu akiniuliza Kama tumeachana na MKE wangu, nikamuuliza kwa Nini? Akasema Kuna mwanaume kampost fesibuku na kasindikizia Maneno ya kimahaba mno. Ikabd nami niingie fesibuku kujionea.
Mwamba alikua anampelekea Moto Shem?
 
Wife akawa anabubujikwa machozi akisisitiza niwaulize hata ndugu zake, Ni Kaka yake yule, sio mpenz wake, alimpost ili nipate wivu maana nilichomfanyia kilimuuma, alitaka nami niumie vile vile. Aisee, hata sikutaka kumskiliza zile ngonjela zake maana Kaka zake wote nnaowajua sijawai kbs kutambulishwa kwa Kaka yake Kama yule mwamba.

Baba mkwe alivonipigia nikamweleza, akaomba, nimtumie zile picha, baada ya kuziona akanambia habar zile zile kwamba Ni Kaka yake yule, alipoanza kujieleza Sana, nikajua uyu keshapangwa tayar, apa wanataka kunichota akili Ili kuokoa TU ndoa ya binti Yao ili niendelee kulea bao la yule mhuni. Nae bamkwe sikutaka kumsikiliza sana,nikamkatia simu.

Ule ugomvi ulifika mpk nyumbani kwetu, Wazazi pande mbili wakakutana kuyazungumza ila nilichokomalia mimi Ni Kwamba nataka kumuona uyo jamaa aliepostiwa face to face,nna maswali yangu binafsi ya kumhoji.

Ukweni wakasema hawez kuja, Yuko mbali sana ,kigoma uko kikazi, anafanya kazi kwny makambi za wakimbizi. Nikajua hii mbinu ya kishamba Sana ya kunilaghai, nikajisemea kimoyomoyo "hawanipati".
 
Wife akazidi kusisitiza kua Mimi pia nna makosa, ndo nmepelekea apost vile kwa usaliti nilomfanyia, mama mkwe akamkata kilimi binti yake, kwamba Kama Hana la kuongea akae tu kimya, Hakuna linaloweza kuhalalisha ule upuuzi alioufanya mitandaoni. Mwanamke mpumbavu uvunja ndoa Yake mwnyw, Ni aibu gani hii kaileta Kwny familia yake. Ma mkwe akaanza kulia, Ikabd wife akae kimya.

Mzee wangu akanisisitiza niyamalize,Nikawaambia mzee kua kupost fesibuku nishamsamehe wife,ila icho kichanga chake bila uyo jamaa kuja nimuone nisikione kbs Kwny mazingira yangu, vinginevyo ntakiua na msije kunilaumu. Wakasema Sasa nmefika mbali.

Nikawapa option 2, Either kichanga kibaki ukweni, atakua anakuja kukinyonyeshea uko uko, au akakipangie chumba mtaa wa jirani, atakua anaenda kukinyonyesha na kurudi kwangu. Wakasema haiwezekani, nami nikasimamia Kama haiwezekani Basi Hii ndoa haipo Tena, siwataki wote wife na mtoto. Kile kikao kikawa kimeshindwa kufika muafaka,nikaondoka zangu.
 
Walikaa Kama wiki hivi wanaleta story zile zile na mwamba hata haletwi, nikaona usumbufu gani huu, wote wife na wakwe zangu nikawablock, nikawa naishi kivyangu vyangu.

Baada ya kuwablock, sjajua walimshawishi Nini wife, nmerud jioni kumbe wife kajificha ukutani, ile nmefungua tu mlango niingie ndani, wife nae kazama ndani anasema Kama kumuua nimuue TU,humu ndani haondoki hata kwa greda. Kweli tulivutana hakutaka kutoka Wala kumtoa Mtoto nje. Nami nikavunga Kama nmesalenda. Nikamuacha ndani.

Alilala usiku wa kwanza, usiku wa pili nikawa nyutro Kama maisha yamerud upya na ilipofika siku ya tatu asbh nikamtuma anifatie vocha na mkate dukani ili ninywe chai niende kazini, Alivorudi tu alimkuta mwanae na mabegi yake yote nje kibarazani.

Alivonipigia nikamwambia wazi msimamo wangu bado Ni ule ule, nmefunga nyumba yangu mpk jamaa uliempost fesibuku aje nimuone face to face, ujaridhika na maamuz yangu basi kanishtaki mahakamani. Akabeba mizigo yake kurudi na kwao.
 
Nami nikaona kuendelea kukaa pale, atakuja kunivizia nmerudi ang'ang'anie vile vile kuondoka ndani, ikanibidi kupakimbia kwangu na nikaamia nyumbani kwa mzee.

Nmekaa kwa mzee siku ya 3, nashangaa asbh kumuona wife Yuko na mama angu jikoni Sijui wanapika pika Nini. Nikaona na Hawa wazazi wangu nao miyeyusho, washaanza kuniletea Mambo ya ajabu ajabu

Pale nyumbani nako nikahama mazima na kuanza kukaa gesti, Mzee akanisihi sana nirejee nyumbani, uko gesti nnakoishi nisije jikuta nmefanya maamuz magumu nmejitundika. Nikamwambia mzee asiwe na wasiwasi,uku Niko salama Sana.

Mzee akasisitiza kua uyo jamaa alopostiwa keshasema Yuko njiani anakuja, nikamwambia mzee " uyo jamaa akifika mtanijulisha, ila siwez kulala paa Moja na uyo mwanamke ibilisi mkubwa na usingizi ukaja, vinginevyo mnanitafutia murder case wazazi wangu". Basi mzee akakubaliana na mimi.

Nikiishi zangu gesti na kuendelea na shughuli zangu, wife akawa anawatumia rafiki zangu kuniomba msamaha na kuomba Ela za Matumiz, nikasema sitoi maana Hapa Hakuna tena ndoa, na hata Kama Ni Matumiz ya Mtoto, bado Sina uhakika Kama kweli Ni damu yangu.

Rafki zangu wakanambia sio vizuri kutelekeza familia, nikawaambia ambae hajaridhika na maamuz yangu basi akanipeleke mahakamani kunishtaki nmetelekeza familia yangu, na anaedai yule Mtoto Ni damu yangu alete ushahidi mezani. Vinginevyo Msimamo wangu ndo huo huo,siwezi kubadilika.
 
Baada ya siku 5 nikaitwa na mzee kwamba jamaa keshaletwa, wake zangu wote wapo na ananihitaji nifike nyumbani tuyazungumze. Kweli Nmefika,utambulisho wa jamaa umefanyika. Kumuangalia vzur mwamba, kimoyo Moyo sura ikawa Kama inanijia kichani ila skumbuki vzur niliwai kumuona wapi.

Mwamba yeye akasema ananifahamu sana hata kabla sijamuoa rasmi wife, anasema mpk naoa hakuepo, alikuaga kikazi uko kigoma.

Akanikumbusha kwamba Kuna siku tuliwai kuchimbana biti kubwa kwenye Simu niachane na mdg wake kwa namba inaishia na flani alikua anaitumia wife kuchat na Mimi,zote ilakujua Ni Kaka yake yupi maana Kaka zake wengi walikua wananiandama Sana enzi hizo . Iyo memory kweli nikaikumbuka.

Mwamba akanikumbusha pia kwamba kipind tushakua wachumba, niliwai kumlipa Ela ya boda Mara 2 alipombeba wife kumleta kwangu nikidhan yeye Ni bodaboda. Nikakumbuka kweli wife aliwai nambia yule nisimuite boda Ni Kaka angu ananipaga lift tu, usimlipe Ela, sema sikutilia maanani, maana nilipokua Nampa Ela jamaa alikua hazikatai.

Basi kikao kikaisha na ugomvi ukawa umesuluhishwa vile kifamilia. Wife na Mtoto wakarud nyumbani Ila tangu Apo sijawai kuona wife kapost tena upumbavu Kama ule.

Baada ya Apo Yule mwamba alikuja kua miongoni mwa shemej zangu tulioelewana Sana na Bahat mbaya mwaka juz mola alimchukua, figo zilimsumbua Sana,hakuchukua round tukamzika. R.i.p

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom