Wanaume yatupasa kuzingatia haya....

Wanaume yatupasa kuzingatia haya....

Duh wewe mwanaume au? Naona unatuita kila majina ya dharau japo ujumbe wako upo mzuri. Lakini hizi dharau za nini kuitana mjinga na ********? Tuombe radhi kabla ya kukupeleka mahakamani na kupewa faini ya milioni 7[emoji12] [emoji1]
Hiyo nlikuwa namjibu dada pale juu....mie pia ni mwanaume lakini soma post vizuri utanielewa na usiweke maana nyingne tofauti na mada iliyopo...mwanaume daima ukiwa unamsaidia mkeo kwa wanaume wenzako utaonekana mjinga, lakini hawajui kuwa unatengeneza furaha ndani ya nyumba yako
 
Wanawake hawako kama unavyowajua,wako kama usivyowajua,chukua hii
 
Ujumbe mzuri sana mungu akubariki sumu ya mahusiano ni mashindano na ubishi pamoja na ubabe lkn ukiwa mjinga mambo lazima yaende!barikiwa sana
 
Tatizo vijanga wengi tunataka kuogopwa na wake zetu na sio watuheshimu....mke wako akikuheshimu daima ndoa utaiona nzuri lakini ukiweka ubabe tu ndo tatizo linaanzia hapo
 
Bora mkutane wote wajinga kila mmoja adate kwa mwenzie ila kukiwa na imbalance ndio dah, usiombe maana utakutana na vituko ambavyo hujawahi kushuhudia ulimwenguni toka kwa kiumbe kinachoitwa mwanamke...
Nasema hivi due to real life experiences,mwanamke ni kiumbe kidhaifu mno katika mazingira halisi na ameumbwa ili aongozwe katika njia sahihi na mwanaume ndiye atatakiwa kuwa kiongozi wake maisha yote.

Udhaifu mkubwa wa mwanamke ni kuwa ana akili nyingi mno ila hushindwa kufanya matumizi sahihi ya hio akili especially reasoning before acting. Sio wote ila, majority wanaendeshwa kwa tamaa na hisia (fantasies) kuridhisha nafsi zao zaidi kuliko akili. At times mwanamke hujua kabisa kwamba anachofanya sio freshi ila anawaza current benefits na wala hatojali future time impacts. Kwa kuwa mwanaume amepewa akili kidogo na uwezo mkubwa wa ku reason before acting ameambiwa na mungu aitumie ile loophole ya udhaifu wa mwanamke ili amtawale vyema na kumuongoza katika njia sahihi muda wote na si kumuangukia.

Hivyo mtoa mada ni sawa kabisa kuwa karibu na wake zetu ili tuweze kutawala vyema hisia na akili zao ila si kusubmit kwao kama ulivyopendekeza! Pia utajua namna nzuri ya kuishi na udhaifu wao ukitumia akili na busara zaidi!
 
Wanaume wengi ambao hujifanya wajinga huwa waerevu daima na wanaume wengi ambao hujifanya wajanja huwa wajinga daima,sababu kuna ukubwa wa mwili na udogo wa akili ,harafu kuna udogo wa mwili na ukubwa wa akili .Mwanaume mjinga machoni pa wanaume wajanja ni yule anayewahi nyumbani kukaa na familia yake ,kucheza na watoto wake na kufanya home work na watoto wake ,na kumsaidia mke wake kazi za nyumbani.

Mwanaume mjinga aingiapo ndani hata mtoto akiwa ananyonya ziwa la mama yake asikiapo sauti ya baba yake huliacha ziwa la mama yake na kumkimbilia baba yake ,sababu baba yake ndio hazina ya furaha na faraja .Kuna wanaume bora ambao hujinyima furaha yao na kuikimbia starehe na kuipa familia kipaumbele kwa kila jambo,mke wake mwanaume mjinga humfanya mke wake muhasibu wake na rafiki wake wa karibu ili kutengeneza familia yenye upendo na mshikamano.

Daima palipo na mwanaume mjinga ambaye ni mwerevu nyuma yake huwa kuna mwanamke bora mvumilivu mwenye upendo na faraja kwa mume wake,wanawake bora wenye mapenzi ya dhati na waaminifu wapo wengi ila hawaonekani kama wanawake wazuri wasio na sifa za kuwa mama bora na wake bora,wanaume bora wamejaa kila kona wakihaha kutafuta wanawake bora na waerevu.

Utamu wa ndoa ni kuwa na mwanamke mnyenyekevu na muadilifu na kuwa na mwanaume mjinga , mwerevu na msikivu kwa mkewe .Daima mtoto huwa na afya ya mwili na afya ya ubongo kwa tabasamu la baba yake na kicheko cha afya cha mama yake.It is easier for a father to have children than for children to have a real father.
#GedsellianTz
Na siku mwanaume mjinga anapofulia huweje????
 
Daima mwanaume unatakiwa kuwa kichwa cha familia...ujinga ni usemao hapa ni kuwa karibu na familia yako na kumsaidia mke wako dats y nkasema mke wako atakuwa na heshima na mnyenyekevu kwako
 
Hiyo nlikuwa namjibu dada pale juu....mie pia ni mwanaume lakini soma post vizuri utanielewa na usiweke maana nyingne tofauti na mada iliyopo...mwanaume daima ukiwa unamsaidia mkeo kwa wanaume wenzako utaonekana mjinga, lakini hawajui kuwa unatengeneza furaha ndani ya nyumba yako
Kuna mbeba box mmoja alikuja tz na kuoa sasa akafanya kama unavyosema kumsaidia mke. Matokeo yake mke kutwa yupo na luninga hata jiko halitaki tena.

Sent from my SAMSUNG-SM-G900A using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom