Newcreation
Member
- Jun 3, 2014
- 31
- 32
Bila shaka umewahi kushuhudia au kusikia kwamba:
wanawake [wa zama hizi wakiwa wanaongoza] wanavutiwa kimapenzi na wanaume wenye uwezo [i.e wenye kazi nzuri, wenye fedha za kutosha, wenye mwelekeo mzuri kiuchumi na wenye akili za maisha] huku wakiwapuuza ama kuwakataa wanaume ambao "hawana mwelekeo" wa maisha mazuri.
Unajua ni kwa nini wanawake wana hulka hii?
Nitakudokezea kidogo! Ukisoma Mwanzo 2: 7-25 Utaelewa kuwa Mungu alipomuumba mwanaume alimpa vitu VINNE (4) kwa vipaumbele vifuatavyo:
Kwanza alimuumbia roho ya kuabudu;
pili akampa kazi(kutunza wanyama, kuitunza na kuihudumia bustani ya Eden kwa ajili ya chakula n.k);
Jambo la tatu akampa maarifa (Kipi cha kufanya na kipi cha kutofanya pale bustanini).
Baada ya hayo matatu ndipo akampa [jambo la nne] nalo ni msaidizi, yaani mwanamke.
Nini maana yake?
Hii ina maana kwamba Mungu alitambua kuwa ili mwanamume amudu kuishi na mwanamke pasipo matatizo anatakiwa:
1) awe na uhusiano mzuri na Mungu,
2) awe na kazi inayotosheleza mahitaji na
3) pia awe na maarifa na akili za maisha na za kumuongoza mwanamke(ambaye Mungu anamtaja kama kiumbe dhaifu).
Ndani ya kila mwanamke kuna "king'amuzi cha asili" kinachokazana "kusaerch" mwanaume mwenye vigezo hivyo vitatu.
Kwa hiyo wanaume (hasa msiooa bado) msipoteze muda kunung'unika, kulaani na kulalamika inapotokea wanawake "wakali" wanawakataa kwa sababu hamna hivyo vigezo.
Anachoangalia mwanamke ni usalama wake kiuchumi, kimaamuzi, kiroho na kihisia pindi atakapokuwa chini yako [yaani atakapokuwa mkeo] Hivyo nawashauri mhakikishe mnamtafuta Mungu kwa bidii, iweni na mitazamo, maono na mipango inayoeleweka kuhusu uchumi wenu[wa sasa na wa baadae] na tatu tieni bidii katika kujifunza mambo mbalimbali kuhusu maisha:
Ndipo "VING'AMUZI" vilivyomo ndani ya "WAKE WEMA" vitawanasa mlipo pasipo ninyi kulazimika kutumia nguvu nyingi na maneno mengi.
Na kwenu wanawake; ukiolewa na mwanaume asie na sifa hizi tatu jilaumu mwenyewe!