Wanaume wenzangu tuwe makini

Wanaume wenzangu tuwe makini

Mgirik

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
13,258
Reaction score
13,368
Ilikuwa mwaka 2004 nilipokuwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondary Matema beach iliyopo wilayani Kyela. Katika shule hiyo nilipokuwa nasoma nilibahatika kufahamiana na dada mmoja alikuwa anafanya biashara ya kuuza chai na maandazi mbali kidogo na eneo la shule.

Alikuwa ni dada mwenye heshma na nidhamu ya hali ya juu sana na alikuwa mpole sana. Kama ilivyo kwa vijana wengi tunapokuwa kwenye umri huo nilitokea kumpenda na ikabidi nimtongoze. Lakini yule dada alikuwa anasita sana kunikubalia, mimi nikazidi kumganda na baadaye akakubali kuwa wapenzi.

Ikaanza shughuri ya kutaka kufunua utupu, huyu dada alikuwa mbishi sana kuniachia utupu, sikukata tamaa nikazidi kumganda ili anifunulie utupu lakini dada alikuwa mbishi sana.

Sababu yake kuu ilikuwa ni" mdogo wangu ipo siku nitakupa penzi ila nakuomba soma kwanza sitaki nikuchanganye wewe bado mdogo sana mama yako atanilaumu sana siku nikikupa. Mimi nipo kwaajili yako hiyo ndio ilikuwa sababu yake kuu ya kunakatalia utupu.

Alizidi kuwa karibu yangu zaidi na alikuwa ananipa kila ninachokitaka isipo kuwa kunivulia nguo tu. Siku zikaenda na miaka ikapita hatimaye nikamaliza masomo yangu huku dada Sophie akiendelea na biashara yake. Hatimaye nikaondoka na kuja kanda ya mashariki kimasomo.

Kule Mbeya yule dada akaanza kuugua wakazunguka naye katika hospitali mbambali lakini hakupata nafuu. Siku moja nikaenda likizo nikaenda moja kwa moja kwa yule dada kwenda kumpa salam nikamkuta anaumwa lakini alikuwa katiak hali ya kawaida.

Baadaye nikarudi masomon toka kipindi hicho cha mwaka 2008 sikurudi tena mpaka nilivyorudi mwaka huu wiki iliyopita. Ndipo ilipopatwa na mshangao nilipoenda kumsalimia dada Sophie ambapo nimeoneshwa kaburi lake na kuambiwa kuwa amefariki kwa UKIMWI.

Sijaamini kwa kweli. Kumbe yule dada alikuwa na siri nzito sana moyoni mwake, Alinipenda zaidi mpaka aliweza kuniepusha na kiama cha ugonjwa huu.

Nmeoneshwa picha zake ni alikuwa anatisha. Jamani wanaume sio kila mwanamke anayekukataa hakupendi, mwingine anakuokoa na hatari.
 
ndo hivyo somo :wanaume tuache kuwa ving'ang'anizi.
 
Ndio uache ufataki kijana mdogo unapenda vya wakubwa hafu na hilo baridi ka huko Mbeya nadhani rate ya maambukizi ipo juu.
 
somo nzuri wengine kututukana kumbe tunawaepushia mengi... pole kwa kupoteza kipenzi chako
 
^^
Kumbe mimi nimekosa mengi mazuri na nimeepuka mengi mengi kwa pamoja.. Kanuni yangu ni moja tu, sijui kubembeleza
^^
 
dah...! itabidi niache kulilia sasa....
 
Ndio uache ufataki kijana mdogo unapenda vya wakubwa hafu na hilo baridi ka huko Mbeya nadhani rate ya maambukizi ipo juu.

mkuu sio ufataki ila ni hisia tu. Huyu dada hata ungekuwa ww ungefanya kama nilivyofanya mm
 
aiss!alikupenda kuliko ulivyompenda wewe!

mpaka sasa inaniuma sana kumbe sikujua kuwa ananipenda zaidi. Nataman hata angekula matunda yangu japo hata sh 10
 
Hayo ndio mapenzi ya kweli mungu amlaze mahala pema
Utaenda kumfaidi siku ya ufufuo wake mtakapo jumuika peponi
Kazana na ibada na fuata amri za mungu ili uwe na uakika wa kujumuika naye siku ya ufufuo.
 
^^
Kumbe mimi nimekosa mengi mazuri na nimeepuka mengi mengi kwa pamoja.. Kanuni yangu ni moja tu, sijui kubembeleza
^^

bila shaka umeepuka mengi japo hujakosa mengi
 
Mkuu wa Matema Beach umshukuru mungu wako, vp lkn unmjua mwalimu, Koga, au Kava??
 
Siyo wanaume tu,
hata sie wanawake siyo kila mwanaume
akikuton.goza wewe ni YES tu......... you will go soon......
 
Ni nani aliyekudanganya kuwa mbinguni kuna ndoa?
Hayo ndio mapenzi ya kweli mungu amlaze mahala pema
Utaenda kumfaidi siku ya ufufuo wake mtakapo jumuika peponi
Kazana na ibada na fuata amri za mungu ili uwe na uakika wa kujumuika naye siku ya ufufuo.
 
pale matema ukimwi nje nje
ni noma sana pele
 
Back
Top Bottom