Wanaume wenzangu tunakumbushana

Itovanilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
5,158
Salaam jamiiforums

Kila mmoja amechagua maisha fulani ya kuishi ili mradi havunji sheria, lakini juu ya yote, unaweza kuwa unashusha uanaume wako bila kujijua. Leo tukumbushane taratibu kadhaa zenye kuweza kukufanya heshima yako isishuke.

1. Lugha za matusi,
Sina maana kwamba unakuwa umegombana na mtu, ila Kuna Yale mazoea ya kuitana na washikaji au wadau wako kwa lugha za mitaani au uswahilini , hapa hapakufanyi uwe mtoto wa mjini bali mtu usiyejielewa.

2. Kulakula vyakula ovyo.
Njaa haina masaa wala ratiba, muda wowote waweza kula, lakini epuka kula barabarani mbele za watu, umeona muwa unatafuna, Mara karanga unazo, hii haifai Tenga eneo tulivu pata msosi wako endelea na ratiba zingine . Labda kama Kuna dharula ya kufanya hivyo.

3. Mavazi
Mwanaume mwenzangu, punguza kuvaa vitu visivyo na ulazima, kama cheni, mikufu , Pete n.k,unakuta cheni siyo ya silver wala gold lakini mtu haimtoki shingoni.

Pia kama siyo mtaalamu wa lugha, epuka kuvaa nguo zenye maandishi, maana unaweza kuwa kituko mbele za watu. Pia nguo za kubana mwanaume hazimpendezi

4. Kutongoza ovyo.
Wengi wetu tumekariri kuwa kuwa na mademu wengi au kutongoza Kila demu ni uanaume, si kweli.
Hapa Mara nyingi unashusha thamani yako na heshima pia,na epuka kutongoza majirani zako hata wakikushobokea, onesha msimamo wako, hii itampa heshima hata mwanamke wako

5. Malalamiko
Mwanaume punguza kulalamika sana, sijui unalipwa mshahara mdogo, sijui mdeni wako hakulipi, mwanaume unalalamika Kodi ya nyumba inakaribia kuisha n.k

Kuwa na kifua, pambana kimya kimya washirikishe watu muhimu tu siyo Kila mtu.

6. Punguza ujuaji.
Kwenye mpira upo na unajua Kila mchezaji wa kutoka ligi mbalimbali, kwenye muziki hupitwi, kwenye siasa ndiyo kabisa unaijua hii nchi vizuri.

Usiwe hivyo, hata kama unajua hivi vyote lakini Kuna muda ni Bora kuwa msikilizaji, hii itakupa fursa ya kujifunza na kuwianisha mambo.

7. Kuazima azima vitu.
Kuazima kitu ambacho huna siyo dhambi lakini ni bora kuazima vitu vya umuhimu na vyenye ulazima, Kuna watu wanaazima hadi earphone za buku , hii itakufanya ushushe brand budda haijakaa poa.

8. Kulala wanaume wawili au zaidi.
Kuna ulazima wa kufanya hivyo, aidha umetembelewa na mdogo wako, kaka yako au mtu ni mgonjwa sana unahitaji kuwa karibu yake.

Kinyume na hapo si vizuri vidume kulala sehemu moja, ukiuliza eti ni washikaji, pia kuazimana mageto kwaajili ya mademu acheni Mara Moja.

9. Punguza ubabe.
Kitu kidogo unataka kuzipanga, hata kama utampiga opponent wako lakini haikupi sifa nzuri, kwani Kuna siku unaweza kuyakanyaga pia kwa waliokuzidi, ukaaibika.

10. Fanya mazoezi sana.
Siyo kibaka mmoja , dogo tu anaondoka na vitu vyako kizembe eti unaogopa kufa, labda kama ni wengi kama vile panyaroad n.k

Lakini pia mazoezi yanakusaidia kuwa mwepesi, siyo unatembea kilomita mbili tu na miguu, halafu unachoka Hadi unabebwa. Kuwa imara gari yako inaweza kuharibikia porini pasipo na msaada na Kijiji kipo mbali. Utafanyaje.

11. Punguza ulevi.
Siku moja moja siyo mbaya ukamwagilia moyo, lakini usiwe na addiction kupita kiasi, dhibiti matumizi yako ya pesa, matumizi yasiyozingatia nidhamu huanzia kwenye ulevi, pia mademu wasio wa lazima huanzia kwenye ulevi.

12. Salamu za kukumbatiana,
Kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo, mnaweza kupeana mikono tu freshi, siyo kuiga Kila kitu. wanaume mnakumbatiana huku mnaangaliana usoni.ni hatari sana

NB: Ishi utakavyo kwakuwa huvunji sheria za nchi na maisha hayana kanuni.
 

Pia kuna aina za vyakula mwanaume hutakiwi kuonekana unakula..! Vitu kama ice cream, chocolate, pipi kijiti nk. Hata chipsi ule kwa shida shida tena kwa siri
 
Namba 12 nimecheka sana,
Ila maisha yana kanuni bro!ukitaka kufsnikiwa,kuwa maarufu,kufikia ndoto zako kwenye nyanja ya dini,michezo,Elimu,nk lazima Kuna kanuni za kufuata,
Huwezi kula kula kama nguruwe harafu uwe na afya Bora kwenye miaka 90 kama Mzee Mwinyi,
Mo,Dangote,Diamond,Eron musk,Bill gate,bila shaka wanakanuni zao wanazifsta hawaishi kama sie,wiki nzima ni kushabikia mpira,na mademu
 
Pia kuna aina za vyakula mwanaume hutakiwi kuonekana unakula..! Vitu kama ice cream, chocolate, pipi kijiti nk. Hata chipsi ule kwa shida shida tena kwa siri
Nakazia
 
Pia kuna aina za vyakula mwanaume hutakiwi kuonekana unakula..! Vitu kama ice cream, chocolate, pipi kijiti nk. Hata chipsi ule kwa shida shida tena kwa siri
Hapo kwenye Chips iwe siri mficho, tena ule ukiwa umejifungia sirini.
 
Diamond yupi?
 
Pia kuna aina za vyakula mwanaume hutakiwi kuonekana unakula..! Vitu kama ice cream, chocolate, pipi kijiti nk. Hata chipsi ule kwa shida shida tena kwa siri
umesahau ndizi mkuu!
 
Ndizi mbivu mwanaume ukila inabidi ukishaimenya unavunja sio unaiingiza mdomoni [emoji1]

Tango pia sharti liliwe baada ya kukatwakatwa
Siyo unakula kama ....... [emoji23][emoji23][emoji23] Dah all in all nyuzi ya maana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…