Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea

Ujumbe mzuri sana
 
Kweli uzee plus ulofa una shombo mbaya sana kuhusu wanawake baadhi ni mama zetu na wake zetu hawa viumbe licha ya sisi kutowasoma na kuwajua mbaya zaidi hata wao wenyewe hawajijui.Yupo mmoja alishirikiana na hawara yake kumuua mume kisha akamrithisha hawara baadae hawara akamdhulumu mali yote
 
Uzee wa mtu unalindwa na matendo ya mtu ya ujana wake tena Yale ya sirini na rohoni, wewe kuwa mtu mwenye haki na Umuombe Mungu akusaidie utende haki na Umuombe Mungu awe mtetezi wako na ufanye wajibu wako Wala huo uzee hautakuwa na shida, Mungu amesema mkumbuke ukiwa kijana na yeye atakujali ukiwa mzee, tatizo wengi wanatenda mambo mabaya sana katika ujana wao na wakiwa wazee wanalipwa mabaya yao ndo Sasa unaona mtu anahangaika kusema alipewa watoto na mke mbaya wakati analipwa ubaya wake kupitia hao watu, kikubwa pale unapoacha kutenda haki jitahidi ulie sana kwa Mungu Ili akusamehe na ujutie na maisha yako ya uzee yatakuwa mazuri kabisa.
 
Kwani hakuna wanaume wenye kutenda hivyo? Mwanadamu ni mwanadamu tu tunapojisahau nikuruhusu tuoe au kuolewa na watu wabaya, jamii inatakiwa kuambiwa ukweli kwamba awe kiumbe mke au kiumbe mume wote wanatakiwa kuwa wema na wale wabaya wafichuliwe na watengwe huko jela au wasipewe ruhusa ya kuoa au kuolewa Ili ubaya yao usiumize wengine.
 
Hii inaukweli. Nikimcheki fadha alivojichokea hamna hata mwanaye mmoja atamwambia baba njoo uwatembelee wajukuu zako. Yaani yuko solid hatoki.
Ila Maza sasa leo yupo kwa mwanae Arusha kesho Dodoma mara Morogoro.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi lkn nini nafasi yako kama mwanaume na baba wa familia?
Ukweli famili nyingi mama anafanya kila kitu kwny family to the extent that kids wana amini mama ndo sponsor na sio baba, mfano wanaume wangapi na mara ngapi,
1.tunatoka na watoto wetu kuwafanyia shopping?
2.tunatoka kula bata na watoto wetu?
3.tunakagua madaftari ya watoto wetu?
4.tunafatilia maendeleo ya watoto wetu wawepo shule au nyumbani?
5.tuna shiriki kazi za nyumbani na watoto wetu?
6.tunakua nao pamoja na kuwatia moyo watoto wetu wanapopitia changamoto mbalimbali?
7.tuna piga story na sio kukalipiana mara kwa mara?
Hivyo vyote juu mama anadili navyo sisi wanaume visingizio vingi japo na kili tunabanwa kwny utafutaji ila ukijipanga angalau utapata muda japo mdogo kua na watoto wako.
Mimi najita baba mnoko, nafatilia kinoma maendeleo ya wanangu na inanisaidia sana kuzuia na kurekebisha issues kabla hazijaharibika mazima.
Mfano1. Kuna siku nilimwita kijana wangu nikamuuliza umevaa boxer? akasema ndio, nikamwambia toa shati na suruali. Nilistuka na kuumia sana kuona makovu makubwa mwilini mwa mwanangu. Kumbe mwalimu kampiga. Kweli kijana wangu ni mtundu lkn napinga adhabu yoyote itakayomuacha mtoto na alama za kudumu japo mimi ni muhumini mzuri wa fimbo. Nilifika shule nikaongea na waalimu kwa uchungu bila kuwafokea wakaniomba msamaha na tukaendelea kua marafiki.
mfano 2. kuna shule ya mission nilijua mwanangu wa kike hawezi kupata wastan wa marks zinazotakiwa kujiunga nayo japo yupo vzr. Siku ya tatu baada ya usaili, nilimfata sister mkuu nikamwomba mwanangu apewe upendeleo akaniuliza maswali mengi sana kuhusu binti yangu nikayajibu nikiwa comfortable baadae akaangalia na matokeo ya interview yakalandana na baadhi ya maswali niliyoulizwa. Sister akaniandikia barua ya admission hapo hapo sbb kuu alisema shule yao japo ni kongwe lkn ni nadra kukuta baba anashughulika na watoto wake. So binti akapata nafasi akanishukuru sana na namshukuru Mungu hakuniangusha mpaka sasa japo ndo hivyo tena shule ya kibabe anapata 92 lkn bado anakua wa 135 class.
Wanaume tuwajibike japo kidogo tu tutawaokoa sana watoto wetu
 
Nina story nyingi za kuelezea kuhusu watoto sbb na dili nao squarely sitaki story za kuambiwa tu kutoka kwa mama yao au waalimu wao, nasonga front mwenyewe.
Ukiwa nao karibu wanakua huru kufunguka na hasa ukiwa mjanja kuwadadisi. Wewe mpe chakula mtoto lazima atakua rafiki yako tu. Juzi kati kijana wangu kaniambia "baba naomba niishie form four" nilifikiria fasta nikamwambia fresh hakuna noma lkn njoo na plan, unataka ufanye nn ukiishia form four? akasema nipe muda ntakupa plan yangu. Nikamwambia tena "kumbuka chochote utakachotaka kufanya baada ya kuishia form4 lazima watakutaka uwe na cheti cha form 4 chenye ufaulu mzuru" Akajibu haina shida ntafaulu.
Kusema ukweli niliogopa mtoto mwenyewe ndo kwanza form two anafikiria kuishia form four. Najiuliza nisingekua karibu nae anganiambia biashara ya kutaka kuishia f4? So nasubiri plan yake mezani tudiscuss najua kuna vitu flan anavipenda na mimi napeleka nguvu huko.
 
Itakua forex hiyo, je utakubaliana naye?
 
Daah mkuu umegusa mle mle

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Wazee wengi waliofanya Kazi serikalini zamani tena kwa uaminifu na uadilifu wa hali juu Sana wanachekwa mtaani wengine wanajutia Sana uadilifu wao,wanategemea pension mbuzi ambayo hata mbunge haifikii hata hela ya mbunge kwa siku.
Serikali ingewajali waadilifu hawa Ili kuwatia moyo waliopo makazini.
 
Hii inaukweli. Nikimcheki fadha alivojichokea hamna hata mwanaye mmoja atamwambia baba njoo uwatembelee wajukuu zako. Yaani yuko solid hatoki.
Ila Maza sasa leo yupo kwa mwanae Arusha kesho Dodoma mara Morogoro.
Sasa huyo anayedhurula kwenda kukaa kwa watoto na kumuacha mume wake mwenyewe ndo hajielewi ila na huyo mume wake naye Kuna vitu hakutengeneza ndo maana unamuona ameboa, Sasa kwa vile ni baba yako musaidie kumfanyia mji wa kisasa aliotakiwa kuundaa akiwa kijana kwaajili ya uzee wake, mfano muwekee mashine ya kufua nguo na kukausha wakati huyo mtembezi hayupo yeye awe anafua kwa mashine nguo zake, choo kizuri cha kukaa, vitu vya rahisi vya kutumia jikoni kama jagi la kuchemsha maji na chai yaani hakikisha vitu rahisi kutumia vya kisasa na wakati mwingine mpe hela aende kutembea na kulala hotel hata siku mbili na kurudi kwake kwenye mazingira mazuri hata huyo mtembezi atamuonea wivu.
 
Mengine majaaliwa tu!so kila mwenye hekima ashibae chakula!!unaweza ukawa navyo vyote na mateso ukapata!!fedha si jawabu la yote mkuu!Walee wanao kwa upendo huku ukiwataja mbele za muumba wako kila siku!
 
Shida hapa na yy anaungaunga mwana haelewi usishangae nA yy anaishi hapo hapo
 
Upumbavu nikukosoa mpango wakati huna solutions.
Una uhakika sina solutions? Nilikuwa najaribu tu kutoa maoni yangu. Ila kama solutions zipo nyingi tu kwa kijana ambaye a aniandaa na maisha ya kustaafu. Ningelazimika kutoa solutions iwapo ingekuwa mahala husika. Asante
 
Itakua forex hiyo, je utakubaliana naye?
hapana mkuu, ndo maana nimesema kuna vitu anavipenda na mimi napeleka nguvu huko maana yangu niko tayar kwa zaidi ya 100% kuviendeleza vipaji vyake ili hatimaye aje chagua wapi aende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…