Wanaume wenye magari kuweni makini

Wanaume wenye magari kuweni makini

Lisa

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
1,549
Reaction score
1,075
Habari za leo wana MMU,
Kaka zangu na wanaume wote kwa ujumla naomba niwape tahadhali hii nimeiona imetokea,
siku hizi machangu wanavaa vizurii, halafu wanakwenda kama maeneo ya mbezi, makongo, buza, halafu anajisimamisha barabarani , kisha anaangalia kama ndani ya gari zinazopita kuna mtu, akiona yupo mwanaume peke yake anasogea karibu na kukuomba lifti kuwa amechelewa, kwa tamaa za wanaume unakuta umempa lifti, kisha anakwambia anapitia magomeni au kinondoni, kwa wema wa kaka zetu , anampitisha hapo akifika kinondoni pale au magomeni anakwambia yeye anashuka.
akiwa anashuka anashuka nusu, nikimaanisha kuwa anafungua mlango anatoa mguu mmoja nje, kisha anaanza kukudai pesa, utabaki unashangaa na anadai umelala naye usiku kucha iweje hutaki kumlipa.
tena wanaangalia na jinsi ulivyo ndivyo atakapokutajia dau, na kwa uoga wa magazeti na kuibiwa na vibaka na fedheha unakuta jamaa anazama mfukoni anatoa alichonacho bila kulala na msichana huyo.

TAFADHALI WAKAKA NA WANAUME ACHENI KUTOA LIFT KWA WADADA MSIOWAFAHAMU.
 
Hii mbona Zecomedy walishaigiza hii...
Ni kweli umakini unahitajika....
 
mbona hizi gia za mwaka arobaini na saba??
anyway umewasaidia wakina ushiboy
 
Last edited by a moderator:
Kama hii story umepewa na mumeo,umedanganywa
si kwamba hayatokei but.....mostly haiwatokei watu completely innocents...
 
^^
Tahadhari njema hii.
Wenye magari kaeni chonjo,
Mi na ka mkokoteni kangu najituma sina vishawishi.
^^
 
Wanaume wenye magari au wanaume wanaondesha magari? Wengine wanayo ila wamewapa madereva Lisa
 
Ndo maana mm lift kama nipo alone nabeba wanafunzi tu mchanganyiko maana ukichukua wa kike tu wanaume huvumilivu huwa unatushinda unakuta topic imeanza.
 
ni kweli hii story ya kitambo ila mjue sio watu wote wanapata taarifa kwa wakati mmoja maana watu wanakufa na kuzaliwa na kukua.The commedy walishaigiza hii kitu kama alivyosema mdau mmoja ila ujue kama ukikoma kujifunza angalia anguko linakukaribia.
 
Hvi mbona mnakua hvo jamani??? Kama we uliiona ze komedy, cjui google,cjui u tube ni wewe wengne hatukujua so shut up read and vamusss.asante mwaya kwa ujumbe ngoja nimjuze mpenzi wangu.
 
Back
Top Bottom