Wanaume wengine bwana

paparaz

Member
Jun 3, 2012
30
1
Habari zenu wana JF. Jamani siku hizi kuna wanaume ambao hawana hata busara kabisa. Utakuta mvulana uliyekuwa na uhusiano nae kipindi cha nyuma anaendelea kukufuatafuata kwa kutuma message za ajabuajabu kwa msichana ambaye walishaachana nae hapo zamani na anajua wazi kabisa tayari upo na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye mnapendana sana.

Hivyo kutokana na wivu alio nao ataanza kukufuatilia kwa maneno ya ajabuajabu, ili mradi tu akuvurugie uhusiano wako na mwanaume uliye nae.

Jamani wana JF naombeni ushauri wenu kwa wanaume wa namna hii wafanyweje?
 
mweleze wazi ajue na pia mwambie mpenzi wako mpya kuwa kuna mtu anakuharass ili isije leta kasheshe kama ni muelewa.
 
mhm well hapo mara nyingi inatokana na nyie wawili mlivyokuwa mnaishi katika uhusiano wenu....hapana na maanisha kuwa kuna mmoja kati yenu ali raise matumaini ya aina fulani na mwisho wa siku kuto yatimiza. hii uleta hasira ama dissapointment kwa yule ambaye anaona ameonewa kwa namna moja au nyingine. sasa watu wana ichukulia hili kwa njia tofauti...wengine wanakubali na kupotezea na wengine wanataka some kind of revenge na ndio hao ambao wanatuma sms za ajabu ajabu
 
Isije ukawa nataka-staki, mara chache sana unakutana na mwanaume kauzu. Otherwise, kama una mahusiano mapya, mselemelezee kwa bf wako.
 
Utakuaje na uhusiano 'Mvulana'...??? Unategemea nini ? Tegemea drama kama izo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mweleze wazi ajue na pia mwambie mpenzi wako mpya kuwa kuna mtu anakuharass ili isije leta kasheshe kama ni muelewa.

usije jaribu hii solution yako itakula kwako....kwani wale unaowakubalia huwa unamwambia,au wale ambao sio wasumbufu huwa unamwambia??kwa kifupi unakuwa umemwekea alarm tayari na kuwa makini na ww.
 
Wanawake walivyo wengi bado unamlilia mwanamke nyie ndo mnaharibu dhana ya kuitwa mwanaume
 
hiyo kitu ni simple badilisha namba uanze upya...kuna baadhi ya watu wana hiyo tabia
MTOTOWAMJINI Nilikuwa na hilo wazo la kubadilisha namba za simu, lakini nimeona hakuna haja kutokana na kwamba kwa sasa namba zangu zinatumika kazini, hivyo nitawachanganya na watu wa muhimu ambao wana namba zangu tayari. Nashukuru kwa ushauri mzuri.
 
Mwambie humtaki la sivyo tutaamini unatuzuga
SAMSTEVIE huwezi amini hata huyo mtu mwenyewe sijamfahamu mpaka hivi sasa. Kila nikijaribu ku-trace hiyo namba, haitoi jibu lolote. Pia nisingeshindwa kumeleza hayo kwakuwa huwa sipendi kujibu message hovyo kwa mtu nisiyemfahamu.
 
mweleze wazi ajue na pia mwambie mpenzi wako mpya kuwa kuna mtu anakuharass ili isije leta kasheshe kama ni muelewa.

GFSONWIN Yah offcourse hili swala nilishamweleza Mpenzi wangu. Pia namshukuru Mungu kwa kuwa yeye ni muelewa na ana busara.
 
usije jaribu hii solution yako itakula kwako....kwani wale unaowakubalia huwa unamwambia,au wale ambao sio wasumbufu huwa unamwambia??kwa kifupi unakuwa umemwekea alarm tayari na kuwa makini na ww.

POINTERS Ahsante kwa ushauri, but kwa upande wangu kumweleza Mpenzi wangu naona ni busara zaidi kuliko kukaa kimya.
 
Kwakuwa umemdhulumu penzi mrudishie penzi lake uone kama atakufuata tena

KAKAKIIZA Yani hiyo ni NEVER coz penzi huwa halilazimishwi. Pia kama haukuwa mpango wa Mungu wa mimi na yeye kuendelea kuwa pamoja, asidhani kwamba akitumia mbinu hiyo ndipo penzi litarudi. Akae tu akijua kwamba penzi langu kwake liliisha siku nyingi sana. Hivyo anajisumbua tu.
 
Habari zenu wana JF. Jamani siku hizi kuna wanaume ambao hawana hata busara kabisa. Utakuta mvulana uliyekuwa na uhusiano nae kipindi cha nyuma anaendelea kukufuatafuata kwa kutuma message za ajabuajabu kwa msichana ambaye walishaachana nae hapo zamani na anajua wazi kabisa tayari upo na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye mnapendana sana.

Hivyo kutokana na wivu alio nao ataanza kukufuatilia kwa maneno ya ajabuajabu, ili mradi tu akuvurugie uhusiano wako na mwanaume uliye nae.

Jamani wana JF naombeni ushauri wenu kwa wanaume wa namna hii wafanyweje?

Tatizo lako unajisahau kuwa mapenzi huwa hayaishi kwa mwanaume, wanaume ni tofauti na wanawake, wewe vumilia tu, ila jiulize kwa nini huyo mwanamke alimwacha huyo mwanaume
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom