Alola
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 476
- 300
Salaam wanabodi,
Nimeona nitumie fursa hii kuwafunulia dada na mama zetu jambo moja ambalo wengi wao hawalielewi au hawataki kulielewa.
Kwa kawaida wanaume wengi huwa hawaingii mazima (committed) miezi ya kwanza ya mapenzi. Jambo ambalo
hutafsiriwa vibaya na wanawake wengi. Ukweli ni kwamba wanaume wengi huwa wanapenda baadae sana. Kwa mfano unaweza kuona mtoto wa kiume anavyo kua, kuanza kujitegemea, n.k anaanza kukuza sana mapenzi yake na mama kwasababu akianza kufikiria yale malezi yote aliyotendewa anasema 'loh nakupenda sana mama'.
Hii haimaanishi watoto wa kike hawawapendi mama zao lakini ukweli ni kwamba watoto wa kiume wengi huwapenda sana mama zao na watoto wa kike wengi huwapenda sana baba zao. Nadhani ni suala la uwiano wa hasi na chanya. Na mama anawakilisha mwanamke, kwahiyo kuna baadhi ya malezi ambayo mwanaume aliyapata kwa mama yake angependa pia kupewa na mwanamke wake.
Kwenye mapenzi ya mtu na mwenza wake ni kawaida kwa wanawake 'kuzimika haraka kimapenzi' kwa mwanaume lakini huchukua muda sana kwa wanaume wengi kuthamini na kuanza kumpenda mpenzi wake wa kike kwa moyo wote.
Hivyo basi mwanamke usiwe mwenye papara ya kutaka 50/50 mara unapoanza mahusiano na mwanaume. Usimpe vikwazo vya kutaka abadilike kwanza ili muwe wapenzi. Unapaswa kumkubali kama alivyo halafu baadae waweza kumshauri abadilike vile wewe unavyotaka, lakini pia kumbuka katika mapenzi ni lazima kukubali kuishi na baadhi ya tabia za mwenza.
Haitowezekana aishi utakavyo wewe kwa 100%. Na yeye hatakiwi kukushurutisha wewe uishi atakavyo yeye. Ni suala la kukubaliana na kuamua kuishi na tofauti zenu. Kwa hiyo usiseme "ah mtu mwenyewe hajui kuvaa" au "jamaa halipigi simu kutwa nzima..siwezi date na mtu wa hivyo mimi":smile-big:. Mkubali kwanza kama alivyo na hayo mengine yatafuata taratibu.
Tumia jinsia yako uliyopewa na muumba. Kama ni jambo jema na ni mtu muelewa anaweza badilika vile utakavyo. Tumeona mashababi, matajiri, wababe na majambazi katika dunia wakiwa watiifu kwa wanawake zao. Tumia jinsia yako vizuri na kila kitu kitakuwa shwari.
Nawasilisha.