Tumejua una gari wiyelele mashauzi yote haya ukute una kiusafiri cha Vitz au Duet au Swift!!! Kuna kijana mwenzetu nae alikopa bank banaaa akawa anatufungia vioo kituoni kama hatuoni! Sie hatuna iyana tunapanda dala twaenda!!!!!!
Mungu si Lara 1, hamad siku kimkweche chake kikazima mbele kidogo ya kituo baada ya kutupita! Akarudi kutusalimu na miguu na kutuomba tumuangalizie gari aende ATM hadi fundi aje! Kila mtu akageuza shingo pembeni kama hatumjui vileee! Hamna aliejibu, dala ikaja hao tukaishia zetu! Alijambajeee sasa, kwenda ATM kurudi wamekwapua power window, taaa, site mirror, taa acha kabisaa! Chezea Kino usiku!