Wengine wanaoa wake wengi kama ufahari fulani tu ni kama vile Wamasai wanaona fahari kuwa na ng'ombe wengi wa kienyeji ambao hawawauzi wala hawatoi maziwa mengi ila anaona raha kuwaona wakiwa wengi tu...Kuna kisa kimoja mtoto wa kwanza wa baba mmoja mwenye wake wanne alianzisha mahusiano na mke wa mwisho wa baba ake hadi kufikia kuzaa naye na haikujulika mapema sababu mtoto aliye zaliwa alifanana copy na mume halisi wa mke sababu Baba na mtoto wake wa kwanza nao ni copyright...Mama kubanwa sana akasema nilijiingiza kwenye uhusiano na mtoto wa mume wangu...maana mume wangu hata ikiwa zamu yake kulala na mimi hanifanyi kitu najikuta kwa miezi 2 napata haki ya ndoa mara moja...Ndo shetani akanishinda lakini naomba msamaha sintorudia tena..