SoC02 Wanaume walaumiwe biashara ya ukahaba

Stories of Change - 2022 Competition

YahilimaPaul

New Member
Jul 27, 2022
3
2
Kwanini wanaume?

Ni kwa sababu wanaume ndiyo wanunuaji (Wateja)

Kwa kawaida biashara ikikosa wateja muuzaji hubadili bidhaa au kuachana na biashara hiyo kabisa.

Kwenye jamii wanaume ukiwakuta vijiweni hukemea kwa 100% na kupinga ukahaba lakini ukweli ikifika usiku ndiyo kwanza wanakuwa wateja halisi wa kununua biadhara haramu.

Nani alaumiwe hapa?
Muuzaji anayeliona soko? Au mteja anayetaka bidhaa...

Ukweli ni kwamba mnunuzi(mteja) ndiye huifanya biashara iendelee kutamba sokoni.

Siku wanaume wakiacha kuwafuata makahaba ndiyo siku ambayo ukahaba utakoma na si vinginevyo.

SABABU ZINAZOFANYA WANAWAKE WAJIUZE.

1. Ufinyu wa Utambuzi

Kuna wale wanona kazi hiyo ina leta pesa badala ya kutambua changamoto za kazi hiyo na mwishowe majuto yake. Maana wengi hujikuta wakiwa na maambukizi ya UKIMWI,kuzaa watoto nje ya mpango au kutoa mimba na wengine kutupa watoto.

2. Tamaa
Kuna wanawake ambao wanapenda pesa sana huku wasitosheke na pesa ambazo wanapata za kila mwezi, wanaona hamna haja ya kukaa nyumbani wanajiunga na kazi ndogo ndogo hivyo huamua kufanya ukahaba na ili kupata pesa.

3. Hamu ya kuridhika

Wanawake wengi hujipata kuwa hawawezi kutosheka na mwanamume mmoja wanaamua kutumia mwili wao vibaya na kufanya ngono na wanaume wengi ili apate kuridhika.

4. Kuishi maisha ambayo hawayawezi
Wapo baadhi yao huhitaji maisha ya juu ambayo ni ngumu kuyapata kwa kipato cha kawaida hivyo huamua kujiuza.

KIPI KIFANYIKE KUKOMESHA UKAHABA.

1. Wanaume ambao ndiyo wateja wa bidhaa ya mwili waache mara moja na si kulaumu tu kuwa wanawake wanakosea kujiuza ikiwa wanaume ndiyo soko la hiyo bidhaa. Kama bidhaa inakosa wateja sokoni bidhaa hiyo huondolewa sokoni.

2. Serikali iweke sheria zitakaowabana wanaojiuza ( wanawake) na wanaonunua ( Wanaume) .Mara nyingi wanaokatwa kwenye hili jambo ni wanawake tu na kuwaacha wanaume ambao ni wateja wakiwa huru.

3. Elimu itolewe kwenye jamii juu ya madhara ya ukahaba kuanzia ngazi ya familia,hadi taifa.

ATHARI ZA UKAHABA


1. Maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI. Kaswende na kisonono.
2. Ongezeko la watoto wa mitaani
3. Utoaji wa mimba kiholela
4. Umasikini hasa kwa wateja maana kila mara mteja atahitaji kununua.
5. Kuporomoka kwa maadili kwenye jamii

Lakini licha ya yote Wateja (wanaume) wasiponunua biashara inakufa
 
Acha kuendeleza tabia mbaya ya jamii kila kitu kulaumu wanaume
 
Back
Top Bottom