Wana Jf, ni jambo ambalo naona kama ni kero kwa wanaume wenye tabia kama hii. Unakuta mwanaume ambaye ni baba wa familia mwenye watoto wakubwa wa kiume na kike ambapo wakike baadhi wameolewa na wakiume pia baadhi wameoa. Sasa unakuta mwanaume kama huyu anapanga kuoa mke wa pili jambo ambalo ni hiari kwa kila mtu. Lakini cha ajabu na cha kusikitisha sana ni kwamba baba kama huyu anamuoa mtoto mdogo ambaye ana umri wa miaka 16 ambaye ni rika ya mtoto wake wa wa nne hivi na kimuweka ndani kama mke wake. Hapa nashindwa kuelewa mwanaume kama huyo anakuwa anawaza nini kufanya jambo kama hili. Kwa upande mwingine pia nawalaumu wazazi wa mtoto anayeolewa maana sijui ni tamaa ya mahari ama nini kukubali mtoto wa umri huo kuolewa na baba mzima kama huyo mwenye mke na watoto na wajukuu. Endapo ingekuwa ati mtoto alitoroka na akakataa kuwa yeye anaolewa na huyo licha ya wazazi kukataa basi wasingekuwa lawamani lakini sasa ni jambo ambalo limepangwa na mahari kutolewa kisha kupanga siku ya kwenda kwake na kufuatwa rasmi. Hili nimelishuhudia bila kusimuliwa na mtu yeyote. Nawasilisha kwenu wana Jf.