Wanaume wa DAR hawakuanza juzi

Wanaume wa DAR hawakuanza juzi

LaplaceTransformation

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Posts
776
Reaction score
679
Ngoja niwarudishe nyuma miaka kadhaa. Ni hivi, kipindi tajwa nilikuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ya jogging kutoka upanga - kariakoo - Stesheni - posta - Diamond I jubilee - home.
Siku moja nilipofika kariakoo nikaenda mpaka kituo cha Daladala cha shule ya Uhuru enzi hizo. Nikaamua kuweka pozi pale. Kidogo akaja mama mmoja analia akisema Dunia ya sasa imeharibika. Akaonyesha mfuko wake wa rambo umechanwa na kiwembe na pochi yake imechukuliwa!!! Baadhi ya kina mama pale kituoni wakamfariji na kumpa nauli ya kumfikisha kigogo alikokuwa anakwenda.
Haikupita muda DCM ya buguruni ikaingia, kama kawaida watu wakakimbilia kuwahi seat. Wakati watu wamebanana pale mlangoni jamaa mmoja akapiga vidole kwenye mfuko wa mwanaume aliyekua mbele yake akaibuka na bahasha ya khaki iliyokuwa imeshiba vya kutosha. Kumbe mwenye ile bahadha kamstukia na akawa amemdaka mwizi wake mkono huku akipiga kelele za mwizi mwizi mwizi !!!! Lakini wanaume wa DAR tuliokuwepo pale tukabaki tunaangalia tu!!!!. Yule mwizi baada ya kuona mpango umebumburuka aliachia ile bahasha ikadondoka chini na mwenye nayo akaiokota wakati yule mwizi akisepa taratibu huku akitoa maneno ya kejeri kwa muhanga wake akimwambia, " wewe mshamba una bahati, leo ungelala njaa pumbavu". Haya yoote yanatokea wanaume wa DAR tuliokuwepo pale tunaagalia tu.Na nafikiri yule jamaa aliyepigwa finger atakuwa alitokea mkoani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwenyew ulikuwepo so ulitakiwa uwe mfano yan ni kwamba unajizarau ww mwenyew [emoji4][emoji4]
 
IMG_0616.JPG
 
Anamaanisha kuwa hata walipomuona mgambo tu wala sio polisi akimshambulia mtu kwa lirungu la kuulia fisi walikimbilia kuchukua video badala ya kumnyang'anya mgambi lile lirungu wamsulubu na hilo hilo lirungu hadi bashite aje kuokota maiti yake. Mwizi anachekewa??
 
Back
Top Bottom